Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Mi niliona kwa jirani yetu miaka ya elfu mbili nikiwa na miaka 3 au minne hivi mshikaji mzee wake alinunua lichogo jeupe akawafundisha wanawe kuandika na kuprint akawa anawalipa laki moja na kret la soda mzee alikuwa na pesa sana enzi hizo ko mimi nikawa naangalia nisije shika au kugusa kitu kiharibike wakat ome kwenyew tv haipo ...... sema wana hawakuwa na mood ya IT walisoma mambo mengine r.i.p huyo mzee
 
Mkuu computer yako itakua ilikua na Shida,2008 computer zilikua nzuri tu,Mimi nilikua natumia laptop Dell 6400,
Ilikuwa na virus au na uchafu kibao kwenye temporary files, au kwenye registry keys.
Wakati huo computer zilikuwa faster kuliko alivyo elezea.
Kweli usemacho Soma post yangu niliyo quote.
 
Hapana, wala siyo wa kishua.

Ni vile tu ukiwa mtoto mara nyingi unaambatana na wazazi wako kule ambako pilikapilika za maisha zitakowapeleka.

Utayokutana nayo huko yatategemea na wewe jinsi ulivyo.

Mimi kwa asili ni mtu mdadisi sana. Pia niko observant sana. Halafu nina kumbukumbu nzuri.

Kwa sababu Amstrad ndo ilikuwa brand ya kwanza ya kompyuta ambayo nilikutana nayo, ndo maana mpaka leo bado naikumbuka licha ya kampuni iliyokuwa ikizitengeneza kufa.
HAhahah kweli kabisa
 
Miaka hiyo Magomeni Mapipa jirani na kwamacheni ndani ya Sea boys internet Cafe.
Watu tunachezea computers au pale jirani na round about ya Uhuru Kariakoo kulikuwa na Internet Cafe kubwa tu.
Maisha haya wajameni sasa hivi kila kitu kiganjani mwako..))
 
Back
Top Bottom