Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Tuliokuwa tunajua kutumia computer kabla ya Windows XP tukutane hapa, Hofu ya Y2K n.k

Bado hamjasema nilianza tumia super computer miaka 5000 BCE huko
Kipindi hicho ikiitwa
Zenatir Azur hapo nilikua Nippur Shurrupak kabla hatujahamia Mesoamerica na mkuu Quetzalcoatl (Ningshidza)
 

Attachments

  • IMG-20240211-WA0001.jpg
    IMG-20240211-WA0001.jpg
    108.2 KB · Views: 2
Speed ya ku copy files ilikuaje??data mlikua Mna transfer kwa njia gani?? internet speed ilikuaje??

HD disk storage kubwa ilikua na uwezo gani??Ram Storage? Multimedia files mlikua Mna access vipi??

Kulikua na Digital pictures??upige picha kwa camera then uhamishe kwenye Computer??
Mara ya kwanza kutumia computer nilikuwa mwanafunzi huko bara la Amerika kaskazini 1982, unakwenda kuripoti kwa Profesa ambae amekabidhiwa jukumu la kuwagawia wanafunzi 'units 400' kila mmoja kwa ajili ya matumizi yake. Units zikimalizika unakwenda tena kuomba nyingine.

Mimi kwanza kutumia computer hapa Tz ilikuwa 1986 - apple 2e, ilikuwa na floppy disks za 5 1/2 inches. Kwanza unaweka start up disk halafu ndiyo unaweka disk ya kufanyia kazi (I think it was 560 kb). Enzi hizo hakukuwa na mambo ya kuchora magraph wala kuweka mapicha kwenye documents. Kila program ilikuwa inajitegemea wenyewe siyo kama leo unacopy graph kwenye excel unaweka kwenye word. Kitu internet hakikuwepo kabisa.

Baadae nadhani kama 1994 hivi ndiyo ilianza kuja microsoft office ikawa unatengeneza graphs zako kwenye program inaitwa ' 'wyswyg - what you see is what you get' unatuma kwenye word document na unapaste moja kwa moja. By then floppy za 3 1/2 zile ndogo ndiyo zilikuwa zimetawala.

Mara ya kwanza kutumia digital camera na kuhamishia picha ilikuwa ni 2002 na sony digital camera ilikuwa safi sana.
 
Ubarikiwe mkuu,wengine tunasoma primary Kuna windows XP service pack 2
Wakati wa windows 98 hakukuwa na computer yenye hard disk inayofikia 1GB labda taasisi maalum za kisayansi, majeshi Ulaya na Marekani au Hollywood.
Ilikuwa 320MB au 500MB na kushuka chini.
Hiyo 500MB yenyewe lazima ufunge hard disk mbili kwenye computer moja zikiitwa master na slave.
 
Ukiwa na harddisk ya 4 au 8gb inatosha kabisa kufanya installations ya windows na office 97.

Kipindi hiki internet ilikuwa ni cafe ingawa baadae ilikuja tekinojia ya infrared unaweka simu na laptop karibu kwa uwiano ila desktop ilikuwa lazima ununue device pembeni.

Kuhusu speed ya kutuma files kwa wakati huu flash drive chache sana tena kwa wenye pesa hapa ndipo cd rw zilitumika sana unaandika na kufuta lkn kama kazi ndogo kama documents za word, excel nk unarumia floppy tu, na kuhusu cd kulikuwa na program maarufu kadhaa kama nero ambayo ina option kabisa ya kuzima computer baada ya burning. Yani unaweza burn cd moja ikachukua masaa matatu kwa hiyo kama unalala una tick hiyo option then unaacha unalala. Na CD Drive RW zilikuwa deal sana wakati huu maana ilikuwa lazima ununue separate.

Kuhusu games nyingi zilikuwa za dos kama akina prince of persia lkn zingine ni setup lkn unakuta ina mb 40 tu

Digital picture zilikuwepo lkn kwa quality mbovu ambayo wakati huo ilikuwa best

Forest Hill
Mengi uliyo andika hapa ilikuwa Windows 2000, XP na kuendelea.
Kidogo sana windows 98.
 
It wasn’t that bad. I was there.

I made plenty of friends there, some of whom we are still friends to this day!

Matter of fact, I just came back from visiting one of them in Summertown.
ni kweli maana kwa UK ngozi nyeusi hasa kutoka Carribean walikuwepo kwa wingi sana miaka hiyo
 
Kam sijakosea hiyo shule uliyoiandika ya upili iliunganishwa na shule nyingine around 1987. Ndo maana ametabiri mwaka wa nyuma kidogo. My thinking tu.
BK Middle School ilifungwa mwaka 1990.

Sidhani kama middle school ni shule ya upili.

Middle school ni shule ya kati.

BK middle school ilikuwa feeder school ya Cherwell high school.
 
2002 huko nikacheza magemu na kuangalia ma worldsex kwenye ma internet cafe nikiwa form 2
 
Wakati nasoma high school kulikuwa na Comp Lab ya msaada.
Ulikuwa huingii na viatu wala kitu chochote utaleta vumbi utaua computer.
Au viatu vitaleta vumbi lenye virus kumbe computer virus ni software tu ..🤣🤣🤣🤣
Computer Lab zilikuwa full AC na carpert za nguvu mkiingia viatu mnaacha nje na mkimaliza zinavishwa suit/cover
 
Windows 95,98 zilikuwa zinaload tarateeb sana mpaka kufunguka,wakati huo tulitumia sana floppy disk
 
Humu ndani wadogo zetu na Watoto zetu wamekosa uhondo wakati wa ms dos ukiingia computer room ofisin unaambiwa vua viatu unakuta kapeti jekundu na screen ya chogo kubwa unaambiwa computer room AC za kizamani zinanguruma masaa 24 zinatakiwa zisizimwe mwendo wakujaza floppy kuhifadhi 100 kb unajuta screen nyeusi na nyeupe no window aisee .maisha tunatoka
 
Mambo ya DIR/:A
Asikwambie mtu, MS-Dos ilikuwa na utamu wake bwana!
 
Back
Top Bottom