Tuliopata ajira za ualimu 27 Novemba 2020 tukutane hapa

Habari Watanzania wenzangu

uzi huu ni maalumu kwa walimu tuliopata ajira za serikali zilizotangazwa tarehe 27 novemba 2020

Napenda kumshukuru rais wa awamu ya tano, rais wa wanyonge, rais wa masikini, rais msikivu, rais anayeahidi na kutekeleza...Asante sana rais kwa ajira hii..
Kwa hakika sitakuangusha nakuhidi utendaji kazi uliotukuka

Pia nikipongeze chama chetu cha CCM, kwani kimetupigania sana sisi vijana wake kupitia UVCCM kuhakikisha tunazipata ajira hizi

Wanajf,, napenda kutumia nafasi hii pia kuwakaribisha mkoani Mtwara kwa wamakonde, wanyeji wa huko naomba ukarimu wenu tafadhali
Wee mwongo kabisa! UVCCM wamefanikisha nini? acha majungu! kwani kuna sehemu uliambatanisha kadi ya UVCCM? au una lako jambo?
 
Nianze kwa kukupa pole, Nashangaa sana kuona unashadadia eti kupata ajira, Kama kuna kitu unatakiwa kusikitikia ni kitu kinachoitwa Kazi ya Kuajiriwa, hasa Ajira za kwenye nchi yetu hii chini ya utawala wa ccm, hakuna watu wana matatizo ya maisha kama wafanyikazi (watumishi), hawa ndio watu ambao wanaishi kwa madeni maisha yao yote, kwa malipo (mishahara) wanayolipwa humfanya mtu kuwa na shida muda wote, madeni na maikopo ndio maisha yao ya kila siku, wewe unakuja hapa unaandika eti tukutane hapa !!m yaani unashangilia kuingia matesoni, ?, Kuajiriwa kwenye nchi hii ni kukubali kuwa fukara na maskini, usitarajie kupata ahueni yeyote, kati ya waajiriwa 100 ni chini ya asilimia 10 yao ndio huweza kuwa na ahueni ya maisha, waliobaki ni shida, kuajiriwa ni kosa la kwanza ambalo mtu hulifanya katika maisha, bahati mbaya sana ukishaajiriwa tu huwezi kuacha, ndio maana utakuta mzee anastaafu baada ya muda mfupi anaenda kutafuta kazi nyingine kama ya Ukorokoroni, hapoa ulipo unatakiwa ujiandae, kwani utatakiwa ufanye kazi hiyo kwa miaka 30 au zaidi ijayo ili uweze kuwa na sifa ya kupata malipo yako ya kustaafu, kazi ya kuajiriwa ni ngumu ndio mnaana ina malipo ya mwisho yanayoitwa kiinua mgongo, ambayo serikali dhalimu ya ccm imeamua kuyawekea urasimu na ukiritimba kwamba mtu hawezi kuyapata malipo hayo hata pale anapokuwa ameacha kazi eti mpaka afikishe umri wa miaka 60 napo hapewi yote bali anapewa 30% na asilimia inayobaki anakuwa analipwa kidogokidogo, nimeona waajiriwa wengi wakishindwa kujenga nyumba za kuisha mpaka wanapofikia umri wa kustaafu ndio huvizia mafao yao ya mwisho ili wajenge au wamalizie ujenzi wa nyumba zao, wakati mtu akianzisha biashara ndani ya miaka 5-10 anakuwa amejitengenezea maisha angalau yanayokubalika, hana kusubiri kustaafu, halafu wewe unafurahia kuajiriwa, sisi tulisha umizwa na hili eneo, utakumbuka maneno haya baada ya miaka 30-40 ijayo, leo bado kijana huwezi kuelewa, nikwambie tu kwavile bado una nguvu, fanya kazi kwa bidii ujiandae kuacha hiyo kazi ukatafute shughuli binafsi ya kufanya, wanafurahia Kazi za kuajiriwa wenzetu huko Nchi zenye Utawala Bora na zilizoendelea Ulaya na marekani, mtu akiajiriwa analindwa na kazi yake lakini pia anaheshimiwa sio hapa Bongo, Miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na nafuu, wafanya kazi waliheshimika, walimu na madaktari walikuwa na heshima mbele ya jamii, sasa hivi mwalimu anachanganyikana na walevi wa gongo, daktari anachapwa viboko na DC, Kazi ya kuajiriwa kwenye nchi hii imekuwa kama laana, bahati mbaya sana hakuna njia mbadala, sio hii serikali ya ccm ambayo inasema inataka hela za mifuko ya hifadhi za jamii kufanyia shughli za maendeleo, mnatakiwa mkutane kupeana Pole
Sasa wewe umeongea yote hayo bila kutoa solutions, kazi ya kuajiriwa ni mbaya sawa ila unajua hali za Watanzania mtaani ??? Hali ngumu mnoo ndio maana watu wanashangilia kazi za kitumwa.

Kama umejiajiri ongera sana ila hakuna asiye penda kujiajiri hali ngumu na mitaji hakuna.

MSHUKURU MUNGU KWA NEEMA ALIZOKUJAALIA WALA USIFANYE ISRAFU.
 
Angalau nimefarijika mimi jina langu halikurudi/nimekosa ajira.

Haya mkuu niambie nianzie wapi kujiajiri.....
 
Huajchelewa sana, tafuta mashamba uanze kilimo, kuna manufaa sana, ("kama unataka Mali utayapata shambani")
 
Sasa wewe umeongea yote hayo bila kutoa solutions, kazi ya kuajiriwa ni mbaya sawa ila unajua hali za Watanzania mtaani ??? Hali ngumu mnoo ndio maana watu wanashangilia kazi za kitumwa.

Kama umejiajiri ongera sana ila hakuna asiye penda kujiajiri hali ngumu na mitaji hakuna.

MSHUKURU MUNGU KWA NEEMA ALIZOKUJAALIA WALA USIFANYE ISRAFU.
Tabu yenu nyinyi wana ccm ndio hii, ni wapi nimefanya Israfu ??, ulitaka nisiseme niliyosema ??, kama hayakukupendeza ungekaa kimya, kazi za kuajiriwa zimefanywa kuwa mbaya na serikali, kwa sababu ya sera zake za hovyo, natambua mtaani kuna shida lakini kuajiriwa sio solution, kwa serikali ya ccm iliyochoka ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga
 
Pongezi walimu wetu mlio pata sasa mkaoe wale mademu zenu mlio wahidi kuwa mtawaoa, wengine sisi ni wa panadol 2x3 kwa siku 3
 
Habari Watanzania wenzangu

uzi huu ni maalumu kwa walimu tuliopata ajira za serikali zilizotangazwa tarehe 27 novemba 2020

Napenda kumshukuru rais wa awamu ya tano, rais wa wanyonge, rais wa masikini, rais msikivu, rais anayeahidi na kutekeleza...Asante sana rais kwa ajira hii..
Kwa hakika sitakuangusha nakuhidi utendaji kazi uliotukuka

Pia nikipongeze chama chetu cha CCM, kwani kimetupigania sana sisi vijana wake kupitia UVCCM kuhakikisha tunazipata ajira hizi

Wanajf,, napenda kutumia nafasi hii pia kuwakaribisha mkoani Mtwara kwa wamakonde, wanyeji wa huko naomba ukarimu wenu tafadhali
[emoji3]
 
Duh🙄🙄 hapo ukiwa umewachapa wanafunzi ama? Hatari😀
Kuna wazazi walezi huko vijiji huthubutu kugusa watoto wao, gusa unuke! 😀
Utakutana na vimbwanga hutoamini!

Everyday is Saturday................................😎
 
Habari Watanzania wenzangu

uzi huu ni maalumu kwa walimu tuliopata ajira za serikali zilizotangazwa tarehe 27 novemba 2020

Napenda kumshukuru rais wa awamu ya tano, rais wa wanyonge, rais wa masikini, rais msikivu, rais anayeahidi na kutekeleza...Asante sana rais kwa ajira hii..
Kwa hakika sitakuangusha nakuhidi utendaji kazi uliotukuka

Pia nikipongeze chama chetu cha CCM, kwani kimetupigania sana sisi vijana wake kupitia UVCCM kuhakikisha tunazipata ajira hizi

Wanajf,, napenda kutumia nafasi hii pia kuwakaribisha mkoani Mtwara kwa wamakonde, wanyeji wa huko naomba ukarimu wenu tafadhali
Mshukuru Mhe Tundu Lissu tafadhali. Yeye ndiye aliyeiibua hoja hii ya ajira kwa walimu wakati wa kampeni za urais Uchaguzi Mkuu. Magufuli ameidandia baada ya kubaini inamuangusha. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa wa hovyooo na wa kipumbavu. Hivyo, ajira ukiyopata mshukuru sana Lissu.
 
Back
Top Bottom