Tuliopitia maisha ya "Saidia Fundi" tukutane hapa

Pengine alikua anamfanya kweli, utaitwaje mke na mwanaume mwenzio halafu uchukulie poa!?
Ombea usikutane na fundi alievurugwa πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna saidia fundi alikuwa anaitwa "mke wangu" na fundi, yani haya maisha watu wanapitia mengi sana.
 
Picha linaanza niliambiwa pima ndoo 120 za mchanga jamaa akawasha fegi hapo bado kuchanganya na kuanza kumsogezea,nakumbuka hii siku nilivyopanda kitandani hapo hapo nikasikia jogoo anawika kwamba kumeshakucha siku nyingine inaanza.
🀣🀣🀣🀣🀣
 
Hiyo inaitwa raft foindation mzee... poleni sana!!
 
Uchungu wa nn mkuu πŸ˜…
mkuu kureport site tu engineer anasema saa 12 asubuhi watu wawe wamefika mazingira ya kazi yaaandaliwe
hapo cement tunatakiwa kuleta eneo la kazi kama mifuko 100 ya kuanzia
mashine ikiwaka haizimi mpaka muda wa chakula cha mchana ikiharibika mnasema alhamdulilahπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
yani ni lile zege mnamwaga kwa kasi ya ajabu mchaka mchaka ukiwa slow kulikuwa na wana wametoka mjini wanatukana vibaya sana hizi kazi haziendi bila matusi πŸ˜€πŸ˜€
yani kitengo cha afadhali ni kile cha kuweka cement kwenye mashine ukitoka hapo huwezi kupita road watoto wa shule wanakimbia
tulikuwa site moja kubwa mkuu yani mashine inawaka 12;30 inazimwa 6;30 mchana muda wa kula ugali maziwa
baada ya kula watu wanapumzika kidogo kabla ya kurudi tena muda wa kulala ulimi nje kama kibudu cha mbuzi
 
kuna mafundi wanapenda umwinyi sana muda wa kazi anakupeleka kama fuso la mkaa yupo mmoja kwenye kazi nimeshakimbiza
mpaka nimechoka nimejiinamia mara kobilo imetua kichwani alafu yupo hapo juu anauliza umeumia?
nilivunja lile jukwaa fundi akalala ndani week mimi ndukiπŸ˜€πŸ˜€
 
Dah aisee nakumbuka miaka ya 2013 na 14 hivi nikiwa zangu kusini pande za mtwara huko.

Kwa siku nilikuwa nalipwa alfu saba alafu ikitokea kazi ya kuchimba msingi ni hela mbali na ya saidia,kuna siku nikawa narudi na 10 mpaka 15K alhamdulillaah

Ila bhana kuna siku hiyo maeneo flani hivi tulienda kupiga kazi sasa kulikuwa na ishu ya kujaza zege kama vyumba viwili hivi aisee japokuwa kila chumba ilikuwa tunachukua 15k lakini mziki wake haukuwa wa kitoto aisee.

Nakumbuka narudi nyumbani siku hiyo kudadeki nalala tu naanza kuota ndoto kila tukio la pale site mpaka naamka asubuhi najikuta nimechoka kishenzi mpaka natamani kulala tena ili nipumzike yani nilliona kama ule usiku nimerudi tena site hivi.

Nilipofanya kazi ya usaidia kwa miezi kadhaa nikaenda zangu nyumbani kuna bro wangu alitaka nisimamie nyumba yake,basi nimefika site kwa bro fundi akawa anatafuta saidia wake watatu,nikamuambia fundi tafuta saidia wawili wa tatu ni mie fundi kashangaa wewe safuher si msimamizi ? Nikamuambia nitaplay part mbili hapa usijali.

Nikawa napiga two ndegez at once,ile kazi imwnifunza mambo mengi sana aisee.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Kupokezana zege ilikuwa upuuzi wa hali ya juu. Ni afadhali mgebeba hata kama kidogo kidogo.
 
kuna siku bwana kuna kazi ilitoke homee ya ufundi mimi ndo nkawa saidia fundi fundi nlimpiga udongo mpaka alikimbia kazi akurudi tena na vifaa akaachaa vipo mpaka leoo kibegi chake chenye vifaa mkono bao,pima maji tukamba kamba na kijikoo hahaaaaa

Hii Chai ya rangi. Alafu haina sukari

Ipo kama vile dawa ya Madagascar
 
Pole mkuu.
Nilidhulumiwa 70k na fundi mkuu tangu hapo nikasema sifanyi tena kazi ya kusaidia kwenye ujenzi.
 
Pole mkuu.
Nilidhulumiwa 70k na fundi mkuu tangu hapo nikasema sifanyi tena kazi ya kusaidia kwenye ujenzi.
shukrani sana mkuu bora yako 70k mimi nilipigwa 150k na nikatelekezwa site maana tulipiga kambi kambi pale
nikarudi home na fuso la pumbaπŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…