Restless Hustler
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 5,150
- 20,025
Habari za muda huu
Haya yalinikuta kwenye kazi yangu ya kwanza nilipokuwa bado sijafunzwa na Ulimwengu
1. Chuki ya kwanza nilijisababishia mwenyewe baada ya kutongoza wafanyakazi watatu kwa nyakati tofauti wote walichomoa na kumbe walihadithiana ndipo nikaanza kupitia sarakasi na vitimbi hadi nikaona Ofisi Ni chungu.
2. Chuki ya pili nilikuwa na mshkaji alikuwa anapenda kunitembelea, siku moja alikuta kifaa kinachofanana sana na cha Mradi wa Taasisi, akauliza tu friendly umekitoa wapi, nikamjibu nilinunua dukani. Kumbe alienda kumuambia boss kuwa nimeiba kifaa Cha Mradi! Boss na yeye mwanamke, badala ya kuniita na kunihoji, akachukua uamuzi wa kunipunguzia 75% ya majukumu ikwemo ya site kwa hoja ya kwamba nimekosa uaminifu(japo hakuniamba directly, ila aliongea kwa mafumbo).
3. Nilifiwa, wakateuliwa wawakilishi wa taasisi wanisindikize msibani, baada ya msiba wakarudi kuhadithiana Hali ngumu ya kijijini kwetu. Niliposikia kuwa wamehadithia, nikachukua uamuzi wa kumpiga makofi yule dada. Kumbe ilikuwa ni Mali ya Boss, boss akazidisha vitimbi Hadi nikaona nikubali yaishe nikaacha kazi.
Namshukuru Mungu nilipata kazi Nyingine ambayo Ndiyo naifanya Hadi Sasa. Jambo la Msingi nililojifunza ni PRIVACY& CONFIDENTIALITY Ni muhimu Sana wakati wa kujumuika na workmates. Lingine ni KUTOKUMUAMINI YEYOTE KWA WAKATI WOWOTE kwani sehemu kubwa ya Chuki na vita makazini husababishwa na mtu kuwa na DETAILS zako.
Karibuni tushirikishane matukio ya Chuki na Vita tulivyowahi kupitia kazini.