geezerlad
Senior Member
- Dec 31, 2017
- 182
- 195
Hili lilokutokea limenitokea na mimi katika mazingira hayo hayo ilikuwa Health Center. Piga kazi sana mabosi wanaelewa kazi, na ushauri nini cha kufanya kuongeza mapato. Punde si punde majungu yakaanza, sasa walichokosea wale mabosi kwanza walikuwa sio watanzania na hawakupata mshauri mzuri wa kuwashauri jinsi ya kuterminate mikataba. Wao wakanipa termination kwa mihemko yao kilichofuata hadi leo hawana hamu [emoji3][emoji3][emoji3]Nakumbuka 2021
Nimeanza kazi boss ananipenda sana basi kila idea za michongo naropoka tu aamue yeye kuzifanya au kuacha, nikiona wazo zuri la kuboresha clinic yake namfungukia tu bila wasi wasi .....
Miezi michache baadae wateja/wagonjwa wakawa wananikubali basi jina lina kuwa kwa kasi ya ajabu kupita wale nilio wakuta hapo nna miezi mitatu boss ananiita pembeni na kunifanya kuwa mkuu wa idara
Mimi natumia nafasi hiyo hiyo kubanana tuongezeane mshahara nae bila hiyana anafanya ivo .... shida inakuja baadae nilianza kuuza vifaa tiba nikiwa eneo la kazi then ikaleta conflict of interest... ikumbukwe kuwa mwanzoni nilileta wazo kwa boss ila hakulifanyia kazi.....
Wiki mbili mbele nkachukua faida kidogo na kilie kiji akiba kwenye mshahara nikachanga ninunue ka vitz bhana wee..... songo mbingo likaanza
Kazini nashinda asubuhi mpaka jioni nnahitaji leseni kwaajili ya baby walker nikatenga muda ijumaa baada ya kazi nikimbie TRA mara moja Kisha nirudi, loooh!
Mke wa boss (mpare) ananambia umetoka kazini hapa sio getto kwamba ujiingilie na kutoka.... kwa heshima na kuepusha migogoro nilirudi mchana ule nikabadilisha uniform na kutoka kazini ili nirudi kesho hali ikiwa imetulia.
Kumekucha nirudi kazini nakutana na work mate mwenyeji wangu (mfipa) ananambia hapa boss kasema ukija usiguse chochote mpaka yeye atakapo sema.
Haya nimekaa home week nzima siitwi nampigia cm boss ananiambia Kwan nn kinaendelea kima yule kama hajui...
Akanipa appointment tuonane j3
Nimefika akanipa sababu za kipumbavu za kukatisha mkataba
1.umemjibu vibaya mkurugenzi wako (mke wake)
Sikufaham kuwa mke wake ni mkurugenzi maana sikutambulishwa wala hakuhusika katika mchakato wa kuniajiri pia siku tambua majukumu yake wala kwenda ku report kwake.
2.natangaza kuwa nnalipwa mshahara mkubwa. Sikuwahi fanya ivo....
Pili kwani kuna ubaya kujivunia matunda ya ujuzi wako kuna sehemu yoyote katika mkataba inayo zuia kufanya ivo?
3. Eti nauza vifaaa ili hali kuwa nayeye pia anauza vifaa .... lakini muda huo hakuwa na stock yoyote na hakuweza jua ni vifaa gani vilivo kuwa na uhitaji kwa muda ule ndio maana tukavileta.
Nilicho jifunza
1.usiwapende na kuwaamini wote kazini
Boss nilimwona kama baba [emoji777]
2.usioneshe mafanikio yako we walilie shida tu hata kama unacho hii itafanya boss pia ajiamini kuona atakutawala milele
3.marafiki wa kazini ni wanafiki tenga muda ujifunze unafki pia ila usiwe mfitini.... hii itasaidia kuweza kuzichapa ki intelijensia ukiwa hapo hapo kazini
4.fanya kazi masaa ya kazi tu hizo extra hours nenda kafanye kazi kwingine fanya kazi zako vizuri na kwa ufanisi wa hali ya juu ila usiifanyie zaidi taasisi .... hii itasaidia hata siku ukifukuzwa usipate maradhi ya moyo au sonona.
5.usiwe na mpenzi/wapenzi kazini.... maana hii huleta wivu hata kwa wafanyakazi wenzio kama kuna mwanamke anakukubali ataanza kuleta wivu au kama kuna mtu alivutiwa na huyo ulie nae atakuletea shida pia ( hapo juu kipindi jina limekua nilitafuna piss kali sana kias kwamba mpare mmoja MD alifurahi sana alipoona nmeachana na ile yule dada) sema tulio soma Cuba tukaelewa shida yake ilikua nini maana hata tulipo kuwa tukienda kulewa na jamaa alikua anampigia cm yule dada niongee nae mbele yake kima yule.
6.Marufuku kunywa pombe na work mates wako hii itakusaidia sana kufanya wasikujue.