Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Kama na wewe ulikua wakala na walikuona kabisa unafaa kuwa jicho lao...

nikiri tu kwamba walichagua wakala mwenye sifa za YUDA ESKARIOTE maana....

haiwezekani uaminiwe,ujiaminishe kwao halafu mwisho wa siku uje utoe sababu nyepesi....

kama pamba,eti umetubu ni sawa umetubu ila wewe ni MSALITI tu kaone kalivyo na kasura kake....
 
jamani .Mi ni mwanachama wa chadema..2015 nilikuwa wakala wa adc jimbo la msalala khm...wakati huo walisema cdm washirikiane na adc kulinda kura za mzee wa monduli hakuna asiyejua upepo wa kipindi kile taarifa ya habari itv ilikuwa kama mechi watu kideoni...kwenye chumba hakuna cha wizi wala nini alipigwa vibaya na atu walijitokeza sana kupiga kura...(ninachotilia mashaka watu huwa wanabadilishwa usiku wa kuamkia uchaguzi nyie mnaenda kulala huku chini wanawashawishi watu kwa fedha )kuna watu wanawajua ni wapiga kura mabalozi hupewa fedha ya usafiri kuhakikisha wanafika kupiga kura wanachama wao.
2020
nimepambana nimekuwa karani mwongozaji kahama mji
kila kitu kilikuwa sawa..Ila watu hawajajitokeza kabisa tulipata mda wa kupiga stry na kula mpaka tukaanza kupiga story za siasa kwenye uchaguzi kituoni wakati watu wameshakuwa wa kusua sua ...kosa afisa uchaguzi aliwaambia maawakala kiutani jamani waiteni watu wenu waje kupiga kura...unajua jinsi ccm walivyo well organised...hahah...vibibi vibabu wazee ambao hawajui sera wala nini wanasema ..tupo nao toka mkoloni chsgus ccm tu...hswamjui hata magufuli ...
nilimaliza kazi yangu saa 10.01 nikasepa ila nikajua tayari wamepigwa pakubwa sana mambo ya ndani au maelekezo ya ndani hapana walikuwa na mawakala wazuri sana wasingefanya kitu...mdakidogo matokeo kuja wamepigwa...wale wasimamizi wa uchaguzi na wagombea walikuwa wanapita kila kituo tukiwauliza vipi huko wanasema hali kama hapa hakuna wateja..
suala la wizi aaah binafsi bado sijaona ...nikiona sawa natilia shaka sehemu hakuna wakala...
 
Kama na wewe ulikua wakala na walikuona kabisa unafaa kuwa jicho lao...

nikiri tu kwamba walichagua wakala mwenye sifa za YUDA ESKARIOTE maana....

haiwezekani uaminiwe,ujiaminishe kwao halafu mwisho wa siku uje utoe sababu nyepesi....

kama pamba,eti umetubu ni sawa umetubu ila wewe ni MSALITI tu kaone kalivyo na kasura kake....
Soma uelewe!Me Sikuwa wakala.
 
KUHUSU mawakala waondolee dhambi kwani wengi walikuwa na akili ya Hali ya juu.
Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika mawakala wengi walitaka wahesabu kwanza vibutu zilikochanwa kura ili wajue wapiga kura NI wangapi then ndo wahesabu kura msimamiz anakataa na kupiga simu police station eti kituo hiki kina fujo polisi wanakuja wanachukua msimamizi na mabox na kutokomea kusikojulikana na kumwacha wakala pale hajui la kufanya mbaya ZAIDI waliambiwa wasiwe na simu
Daaaah. Noma
 
Umetimiza shauku yako ya wewe kuchangia hii thread.
 
Napata uchungu sana pale napokumbuka kuwa vyama vinatumia gharama kubwa sana kufanya kampeni, mfano kukodi chopa sio pesa ndogo! Pia gharama hizi kuna nyingine zinalipwa cash na nyingine yanakuwa ni makubaliano ya kuja kulipa baadae uchaguzi kupitia mafanikio ambayo chama kitayapata!
Sasa inapotokea mafanikio tarajiwa ya chama yakahujumiwa tena pakubwa kama hivi, kiukweli ni hasara sana!
Bora uingie hasara ambayo unajua kabisa kwamba umeisababisha mwenyewe lakini sio hasara ya kusababishiwa na mtu tena katika mazingira ya kulazmisha!
Mwenyezi Mungu akawafariji na kuwarudishia pale walipopungukiwa wale wote walioingizwa hasara za kulazmishwa!
Pia akawalipe mshahara wao wale wote waliohusika kuumiza wenzao! Naamini Mungu wetu ana macho anaona mpaka ya sirini!
Ndio maana ni muhimu Sana kuhesabu gharama kabla ya kuanza mradi wowote ule. Na katika kuangalia gharama lazima uorodheshe associated risks na namna ya kuzi mitigate maana kila risk ina njia ya kukabiliana nayo. Nyingine una mitigate ila nyingine unazimeza jumla jumla kama zilivyo. Am sure waliyaona haya yote.
 
Mawakala waliambiwa hawatopewa barua za utambulisho baada ya kuapa bali tume yenyewe ndo itapeleka barua kwa wasimamizi wa vituo. Kua sehemu nyingine tume ilipeleka na sehemu nyingine haikupeleka kabisa. Na huwezi kuipangia tume
Waliambiwa na......?
 
Hiyo katiba mpya itapatikana vipi bila CCM kuwekwa oembeni kwanz?

Nionavyo ili CCM itoke cha kwanza System ya nchi iwachoke hapa nazungumzia TISS na JWTZ
Na system haiwezi kuwachoka kwa sababu huko wamejazana makada wa chama tawala na wanalipana mishahara mizuri pamoja na marupurupu, so ni mwendo wa kulindana tu. Ili ccm itoke ni lazima sisi wananchi tuamke kutoka usingizini na kuikataa kwa nguvu zote
 
Hata hivyo Biblia inahimiza kutii mamlaka pia.
Je, na huyu Idi Amini Dada Oumee wa Uganda aliyepindua mamlaka iliyokuwa ikitawala kipindi kile (1971), naye kifungu hiki cha Biblia (Warumi 13:1-7) kilikuwa kinamhusu?
 
Back
Top Bottom