Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Watanzania tunajua CCM imeshinda kwa kishindo, hayo mengine mtajua wenyewe na mtahukumiwa kila mtu kwa wakati wake.
3Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha. 4Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako."
 
Inawezekana Hujajielewa bado ila nakwambia neno moja tuu kama wa kusikia basi sikia :-

DHAAALIM
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Pole sana na karibu JF...

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Mi siamini kwenye hilo. Kuna mengi mazuri yanakuja. Tutarajie kuona mafanikio mengi. Nchi hii ni yetu sote. Kama wapinzani ndio walikuwa wanakwamisha maendeleo naamini sasa ndio mda wa kuangalia visingizio vya wakati uliopita kama vitakuwa vilevile wakati ujao. Tuendelee kuwa wavumilivu kaka. Mda utatuambia
Ndugu, tuombe afya na uzima tuone. Wapinzani hawakuwahi kuwazuia kufanya watakalo, kwa wingi wao bungeni na kwenye mabalaza ya madiwani wao ndo waamuzi. Wapinzani wanasingiziwa tu.
 
Imeshindikana kumwajibisha Kwasababu ya idadi ya wabunge, upande wake wako wengi sana,

kukiwa na uwiano sawa hata yeye anawajibishwa ,

kwasasa haitaweza kumuajibisha mkuu, ila wa chini mnalalao nao mbele vizuri tu
Sasa katiba mpya itazuia wizi wa kura?

Maana sasa hivi tatizo CCM wameharibu uchaguzi kwa ballot stuffing, mpaka upinzani unepata wabunge wachache sana.

Sasa, katiba mpya itazuiaje hilo?

Hilo tatizo halikubaliki hata kwa sheria na katiba ya sasa.

Na upinzani umeshindwa kutumia katiba na sheria za sasa kulimaliza.

Katiba mpya itasaidia vipi hapo?

Tuulizane vizuri tueleweshane, tusije kusingizia katiba mpya kama ufumbuzi wa matatizo ambayo hata katiba ya sasa haiyakubali.
 
Nilisema juzi humu sisi wananchi watanzania ni wapumbavu na matahira,kila kitu tumewaachia viongozi wa upinzani nao wamechoka maana hawapati sapoti yoyote kutoka kwa wananchi.

Hata leo hii tukabadilishiwa katiba tukapewa ya USA,kama Rais ni magufuli atafanya against ni hatutafanya chochote.

Ngoja tuungane na wenzetu waganda na Rwanda kuhalalisha upumbavu wetu wa kiafrika.
Mkuu, nisingependa kutumia lugha kali kama yako.

Lakini, point hii ya wananchi kukosa muamko naipigia mstari.

Nimeuliza, kama katiba ya sasa hatujaitumia kukataa maovu ya serikali, kwa mfano Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa kinyume cha katiba, hiyo katiba mpya itatusaidiaje?

Magufuli akipitisha katiba mpya, halafu akaivunja, watu watafanya nini?

Watu wanafikiri kwamba, kuwa na katiba nzuri ndiyo kunaleta mabadiliko.

Wakati, ukweli ni kwamba, muamko wa kisiasa wa watu ndio unaleta mabadiliko.

Na kama hakuna muamko wa kisiasa wa watu, katiba mpya hata ikiletwa, itavunjwa tu, na watu wataendelea kulalamika kipembeni na kusema hewala hewala.

Kwa sababu, hicho ndicho kinatokea sasa hivi hata kwa provisions na guarantees zilizo katika katiba ya sasa.

Naona kama tunasingizia katiba mpya wakati hata ya sasa hatuitumii.
 
Ccm huu wizi wa kijinga na kipumbavu hata mimi mme akilewa huwa siibi hela zote asije kushtukia mchezo sasa nyinyi mnaiba hadi mnapitiliza nimeona matokeo ya ubunge shinyanga mjini na urais yaani havina uhusiano kabisa
point nzuri sana, hawajui kula na kipofu mpaka wanamshika mkono,mfano jimbo la kawe, total votes za magu zimeshinda mpaka total votes za ubunge wa gwaji & halima,ina maanisha kawe kuna watu walipigia raisi tu bila kupigia mbunge na diwani
 
Uko makini mkuu .kenya mwamko mkubwa balaa wanasiasa ndo wanaogopa wananchi
Watu wanafikiri kwamba katiba mpya ndiyo inaleta mabadikiko, kumbe watu wenye muamko ndio wanaoleta mabadiliko.

Flow iko hivi.

Watu wenye muamko wa kisiasa-> Katiba mpya -> Mabadiliko.

Hapo ndipo unapata mabadiliko.

Sisi tunataka kuruka stage ya kwanza.

Tunataka kuanzia hapa

Katiba mpya->

Hapo katiba mpya hata ikivunjwa, kama watu hawana muamko wa kisiasa, hakuna wengi watakaopinga.
 
I concur! Pia binadamu ni mbinafsi akisha kuwa na uhakika wa mkate ,kitanda na nguo anajitenga na wengine .
Nchi yetu kwa sasa haijakabwa vizuri bado utayari utaletwa na:
1.Uchumi au uonevu ukizidi
2.Elimu

Watawala waejua kucheza navyo vyema.misri maisha yalikaza mpaka degree holder alikuwa anauza ma apple wakayamwaga akajipiga kiberiti from hapo hakuna jeshi lililouweza umma
Watu wanafikiri kwamba katiba mpya ndiyo inaleta mabadikiko, kumbe watu wenye muamko ndio wanaoleta mabadiliko.

Flow iko hivi.

Watu wenye muamko wa kisiasa-> Katiba mpya -> Mabadiliko.

Hapo ndipo unapata mabadiliko.

Sisi tunataka kuruka stage ya kwanza.

Tunataka kuanzia hapa

Katiba mpya->

Hapo katiba mpya hata ikivunjwa, kama watu hawana muamko wa kisiasa, hakuna wengi watakaopinga.
 
Acha unafikiiii chadema imeanguka kiuhalalaiiii we mamluki hujasimamia popote Kwanza unasimamia unakula kiapo inakuaje unatoa Siri kama sio shoga, but mi nilikua wakala wa chadema nilikuwepo na barua nikaruhusiwa ktk kuhesabu nikona chadema kweli tumepigwa vibayaaaa
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Wewe ni wakutafutia dawa Ili ujasiri ukukae!! Tulia hivyohivyooo!!!
 
Na wengi wa WASIMAMIZI walkua Waalimu wa shule za sekondari na za msingi

Hii laana itawatuna Kizazi chenu chote[emoji3525]
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Mlikuwa na nafasi ya kujitoa ili msiwe sehemu ya kupitisha CCM kama mlivyofanya. Pesa mmepata lakini dhambi hii mnastahili kifo cha aibu
 
Kaka ukijifanya ngangari hao jamaa wanakuchapa risasi, hao watu wameshaamua kubaki madarakani kwa gharama yoyote ikibidi kumwaga damu za watu wasio na hatia!
Kwa hiyo na wewe ulikuwa wakala sayo??😂😂😂
Unajua ... Sisi wabongo, Cheka Cheka nyingi na masikhala mengi
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Umwogope Mungu au uogope mamlaka ya mwanadamu mwenye mwili ambaye atakufa tu. Kwa dhambi hiyo uliyotenda katubu tu bado mda ungaliko otherwise huwezi kumwambia Mungu siku ile ya hukumu niliogopa mamlaka. Mwenye kutenda dhambi na atende tu lakini huko mbele kuna moto wa kutisha. Furaha ya maisha haya si kitu. Kumbukeni kuna milele.
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Ili toba ikamilike, toka hadharani uombe radhi watanzania, wakikusamehe ndipo Mungu atakisamehe. Soma Mathayo 5:23-25. Hapo utakuwa umetenda haki.
 
Kituo nilichopigia kura mawakala wa upinzani hawakuwepo walifukuzwa kabisa kisa hawakupewa barua ya utambulisho na mkurugenzi, sehemu nyingine walitishiwa maisha la sivo wanauliwa, mawakala ikabidi wasepe tu.

Yohana 8:44​

Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.
 
Wakishinda wapinzani haki imetendeka, ila wakishindwa hakuna haki, tulia sindano iwaingie
Na iwaingie kisawasawa ili wakumbuke pale walipojikwaa ili wasirudie tena ujinga na makosa yao ambayo pamoja na:-

1. Kushupalia ushoga ambao ni laana kwa mila na desturi zetu,
2. Kutegemea ufadhili, misaada na maelekezo kutoka ughaibuni kama nyenzo ya uongozi,
3. kubeza na kupuuza mambo yote mazuri yaliyofanywa na serikali, dharirisha Viongozi wenye mamlaka, kuheshimika au hadhi katika jamii, bila staha, jambo lililo kinyume na maadili, ustaarabu wetu na uungwana.
 
Back
Top Bottom