Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Mkuu 'General', umeyasema mengi, baadhi yake nikikubaliana nayo.

Lakini niseme tu kwamba,'It is more complicated than that'!

Tundu Lissu ni jasiri, ndio, lakini watu hata kule kuvaa T-shirts' tu za kumwombea apone, watu waliogopa.

Leo hii, akifanya jambo la kijasiri na kuwekwa ndani, utamwona nani akisimama nyuma au mbele yake kutetea ujasiri huo?

Mbowe, umemtaja kama mfano hapo; lakini hata hukumbuki yaliyompata hapo Kinondoni kwenye mkutano wa uchaguzi mdogo? Hivi unajua kilichotokea hapo? Unataka ujasiri wa namna gani?

Labda niseme tu kwamba waTanzania hawajampata kiongozi anayeamsha mori na ari zao kiasi cha kutaka kufa au kupona.

Siwezi kamwe kuwalaumu waTanzania na kuwaita 'wajinga' au 'waoga', ni swala tu la apatikane kiongozi wanayemwamini na kusimama naye katika aina yoyote ile ya vitisho na misukosuko.
Mtu huyu, kwa bahati mbaya bado hatujampata, ingawaje najua wapo kadhaa ndani ya nchi yetu hii.
Kwa level ya ujasiri walionao wapinzani hapa nchini sioni kama wapo wa aina hiyo Afrika Mashariki.

Wanaosema Mbowe ni muoga wanamkosea heshima Mbowe, Mbowe kawalaza ccm na viatu toka mwaka 2005 mpaka leo kakoswa Bomu( Arusha) akakoswa Risasi (kinondoni) akatekwa na Jeshi 2011.

Chini ya Utawala wa Magufuli aliyoyapitia Mbowe angekuwa mwanasiasa mwingine angehama nchi lakini Mbowe yupo tu anafikia hatua ya kuwindwa nyumbani kwake na mkuu wa wilaya lakini yupo. Tunataka ujasiri wa aina gani ?

Kilichopo hapa wananchi ndiyo hatutaki au tunaogopa kuwaunga mkono moja kwa moja na hii imesababishwa na utawala wa awamu ya tano kuanza kuwateka watu individually majumbani mwao na risasi juu wananchi wanaogopa haswa.

Lakini kwa viongozi wa upinzani tulionao ni majasiri na wenye weledi mkubwa wa kuongoza mapambano. Mistake aliyofanya Mbowe ni kumteua Mnyika kuwa katibu mkuu wa chama this is a Mistake.

Mnyika anaonekana amechoka siasa.
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Hiii ni Laana isoyo TAKASIKA
 
Kwa level ya ujasiri walionao wapinzani hapa nchini sioni kama wapo wa aina hiyo Afrika Mashariki.

Wanaosema Mbowe ni muoga wanamkosea heshima Mbowe, Mbowe kawalaza ccm na viatu toka mwaka 2005 mpaka leo kakoswa Bomu( Arusha) akakoswa Risasi (kinondoni) akatekwa na Jeshi 2011.

Chini ya Utawala wa Magufuli aliyoyapitia Mbowe angekuwa mwanasiasa mwingine angehama nchi lakini Mbowe yupo tu anafikia hatua ya kuwindwa nyumbani kwake na mkuu wa wilaya lakini yupo. Tunataka ujasiri wa aina gani ?

Kilichopo hapa wananchi ndiyo hatutaki au tunaogopa kuwaunga mkono moja kwa moja na hii imesababishwa na utawala wa awamu ya tano kuanza kuwateka watu individually majumbani mwao na risasi juu wananchi wanaogopa haswa.

Lakini kwa viongozi wa upinzani tulionao ni majasiri na wenye weledi mkubwa wa kuongoza mapambano. Mistake aliyofanya Mbowe ni kumteua Mnyika kuwa katibu mkuu wa chama this is a Mistake.

Mnyika anaonekana amechoka siasa.
Hizi unazoita 'mistake' nadhani ni vigumu kuziepuka. Zinatokea kwa nia njema ya kupanua wigo wa chama; mfano ukiwa uteuzi wa Mashinji.

Sijui kama Mnyika kachoka..., ni nani ndani ya chama angeweza kushika nafasi hiyo vizuri zaidi?

Bila Mbowe, CHADEMA ingekuwa ilishasambaratishwa siku nyingi sana. Tungekuwa tunaikumbuka tu kuwa ilikuwepo, na hata kuwa chini ya hadhi iliyonayo NCCR-Mageuzi sasa hivi.

Sisemi kuwa hakuna uhitaji wa mabadiliko ndani ya chama wakati huu, mabadiliko yasiyolazimishwa na wasiokitakia mema chama, bali mabadiliko yatakayoamriwa na wanachama wenyewe bila ya shurti kutoka nje ya chama. Wanachama na wapenzi wakisema kwa kauli moja kumpumzisha Mbowe, basi pasiwepo na maswali zaidi juu yake. Wakiamua kwamba bado wanahitaji uongozi wake, hilo liheshimiwe na wasiohusika na chama hicho.
 
Kalamu1 acha malalamiko kesho tukutane barabarani
Sina "malalamiko " mkuu, ila kusema kweli sitakuwepo kimwili hapo kwenye maandamano.
Nikuhakikishie mkuu, lolote linalofanyika kupinga uharamia huu unaofanywa juu ya taifa letu nitauunga mkono. Majadiliano haya ni kupanua wigo na akili zetu kuhusu njia mwafaka zinazohitajika kuutokomeza ukoloni huu mpya.
 
Mlitumikia kafiri ili kupata mradi wenu nyani. Laani sana nyie wasimamizi woote.
 
Hata hivyo Biblia inahimiza kutii mamlaka pia.
Kwa mujibu wa Biblia ni Mamlaka halali tu ndiyo tunapaswa kuzitii. Ndiyo maana kina Omar Bashir wa Sudan na akina Hitler na Benito Mussolini waliondolewa na nguvu ya UMMA ya wananchi.

Soma vizuri Biblia usipotoshe, mamlaka zingine ni za SHETANI kama hii iliyomuweka MAGUFULI. Musimsingizie Mungu kuwa ameshiriki kuchapisha kura za uwongo, hiyo ni kazi ya Shetani.
 
Majuto ni mjukuu. Sasa mmeturudisha kwenye utawala wa Chama Kimoja. Sio peke yenu. Hata mawakala wa vyama vya upinzani wamechangia haya

Magufuli atasema ameshinda ila CCM na TANZANIA kwa ujumla tumepoteza
Mawakala wamechangia kukubali kukatwa mapanga na kutekwa au ?
 
Mimi ni mwalimu,sikufanya huo ujinga wa kuomba hiyo kazi ya kusimamia, moyo wangu kabisa huwa hauko tayari kufanya uonevu kwa mtu,sikuwa tayari kulipwa pesa haramu na niliumia sana kuona walimu waliusika pakubwa kutekeleza ule uharamia ni watu waliopata shida sana kwa kunyimwa haki zao wakati wa utawala ule mpaka sasa huwa nawashangaa walimu wenzangu wana akili au matope kichwani. Nilimzuia mke wangu asifanye hiyo kazi akanigomea lakini iliniuma sana na nilitaka niachane nae kabisa.
 
Mawakala wamechangia kukubali kukatwa mapanga na kutekwa au ?
Comment yako ipo out of context. By then yule wakala aliyekuwa kasimamishwa na CHADEMA anasema aliruhusu na kukubali uporaji ufanyike ndani ya chumba cha kupigia kura kwa kile alichokiita “kufuata maelekezo kutoka juu”
 
Hivi unajua mawakala wa CHADEMA waliogoma hata kutoka kwenye vituo tu vya kupigia kura walipoamriwa kutoka wengi mpaka sasa wana majeraha ya kudumu na wengine wanakesi mahakama za kubambikiwa ?

Unashangaza sana karibu nusu ya mawakala hata viapo walinyimwa na wakurugenzi hawa nao walichangia vipi chama kubiwa kura ?
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Jisemee nafsi yako. Uliiba? Wapi? Wahusika hawakulalamika mbona? Tujuavyo sisi tundulissu na CUF walikuwa wanaiba kura huko nyuma ila safari hii tukawabana,
 
Jisemee nafsi yako. Uliiba? Wapi? Wahusika hawakulalamika mbona? Tujuavyo sisi tundulissu na CUF walikuwa wanaiba kura huko nyuma ila safari hii tukawabana,
LGF, unachosahau ni kuwa malipo ya uovu ni hapa hapa duniani. Dhalimu mwendazake hadi familia yake hivi sasa inapumua baada ya yeye kupewa haki yake mapema mwaka huu. Watanzania wenye uelewa katu hawawezi kutoa maneno ya kifedhuli kama haya yako wewe, LGF.

Jaribu kusoma historia uone kilichowapata watetezi wa udhalimu hapa hapa duniani. Na hicho kilichowapata ni kama mvua za rasharasha tu, za kivuli zitakuwa zinawasubiri ahera huko alikotangulia mwendazake!
 
Back
Top Bottom