Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Kwa level ya ujasiri walionao wapinzani hapa nchini sioni kama wapo wa aina hiyo Afrika Mashariki.Mkuu 'General', umeyasema mengi, baadhi yake nikikubaliana nayo.
Lakini niseme tu kwamba,'It is more complicated than that'!
Tundu Lissu ni jasiri, ndio, lakini watu hata kule kuvaa T-shirts' tu za kumwombea apone, watu waliogopa.
Leo hii, akifanya jambo la kijasiri na kuwekwa ndani, utamwona nani akisimama nyuma au mbele yake kutetea ujasiri huo?
Mbowe, umemtaja kama mfano hapo; lakini hata hukumbuki yaliyompata hapo Kinondoni kwenye mkutano wa uchaguzi mdogo? Hivi unajua kilichotokea hapo? Unataka ujasiri wa namna gani?
Labda niseme tu kwamba waTanzania hawajampata kiongozi anayeamsha mori na ari zao kiasi cha kutaka kufa au kupona.
Siwezi kamwe kuwalaumu waTanzania na kuwaita 'wajinga' au 'waoga', ni swala tu la apatikane kiongozi wanayemwamini na kusimama naye katika aina yoyote ile ya vitisho na misukosuko.
Mtu huyu, kwa bahati mbaya bado hatujampata, ingawaje najua wapo kadhaa ndani ya nchi yetu hii.
Wanaosema Mbowe ni muoga wanamkosea heshima Mbowe, Mbowe kawalaza ccm na viatu toka mwaka 2005 mpaka leo kakoswa Bomu( Arusha) akakoswa Risasi (kinondoni) akatekwa na Jeshi 2011.
Chini ya Utawala wa Magufuli aliyoyapitia Mbowe angekuwa mwanasiasa mwingine angehama nchi lakini Mbowe yupo tu anafikia hatua ya kuwindwa nyumbani kwake na mkuu wa wilaya lakini yupo. Tunataka ujasiri wa aina gani ?
Kilichopo hapa wananchi ndiyo hatutaki au tunaogopa kuwaunga mkono moja kwa moja na hii imesababishwa na utawala wa awamu ya tano kuanza kuwateka watu individually majumbani mwao na risasi juu wananchi wanaogopa haswa.
Lakini kwa viongozi wa upinzani tulionao ni majasiri na wenye weledi mkubwa wa kuongoza mapambano. Mistake aliyofanya Mbowe ni kumteua Mnyika kuwa katibu mkuu wa chama this is a Mistake.
Mnyika anaonekana amechoka siasa.