Kuna familia naifahamu,
Mdogo mtu alizaa kabisa na Mume Wa Dada yake, tena huyo mdogo mtu alikuwa anasomeshwa na anaishi na Dada yake tumbo moja.
Dada mtu alipogundua alirudi nyumbani kwako(kijijini). Akawaambia wazazi wake , Mume na mdogo MTU wakaitwa ,wakakiri kabisa.
Dada alikasirika sana akasema, basi yeye anamwachia ndoa mdogo wake ili aweke kumlelea watoto wake (walikuwa 3). Mdogo na shemeji wakakubali, shemeji akapigwa faini ya kimila wakarudi zao mjini kuendelea na maisha.
Dada akaanzisha maisha mkoa mwingine, ila pasipo na mawasiliano yoyote na mdogo mtu, na wale wazinzi wakaiendelea na maisha yao,wakaongeza na watoto wa2, jumla wakawa na watoto 6. Ikawa ni story kubwa huko nyumbani. Ila aibu alikuwa anaona dada mtu,, mdogo mtu wala hakuonesha kujutia kile kitendo.
Baada ya miaka kadhaa wale wakajakuathirika VVU Waliumwa kupita maelezo, baadaye wakafa kwa kupishana 1 year.
Hivi ninavyoandika hapa yule Dada mtu anaendelea na maisha yake, huku akiendelea kuwalea ,kuwatunza wale watoto japo wengine ni wakubwa wana maisha yao. Ila amegoma tena kuolewa, anasema hana imani tena na wanaume. Pia ni mtu mzima anasema bora tu alee ujukuu alioachiwa.
Baadhi ya wanaume wanavuruga sana familia, na hao wadogo zetu wakati mwingine tamaa, uzinzi, na ujinga vinawaponza.