Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Duuh! Mkuu kweli maisha ni darasa
 
Mkuu kuna mengine yanaitwa "Bitcoon"huku.Natilia shaka yatakuwa ndiyo matapeli yenyewe haya
 
Hahahahaha.....Mkuu wewe kiboko, ila wakati unamkabidhi chombo hukua unajua hayo yote? Au ulijitoa ufahamu?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu usikate tamaa. ukifuatilia matajiri wote walipitia shida kama hizo
 
Mbona hujasema hutamani na wanaume.??
 
We learn through mistakes. Haya maisha philosophy yake ni nguumu muno.Kuwa maskini na kufa maskiini Ukiwa mtumishi wa Umaa inawezekana. Na kwa uzoefu wangu Uwe Mwl.au Kada nyingne wote hatuchekani.Labda uwe mpiga dili ndo utacheka.

Hizi habari za mikopo hasa hasa mkopo wa kwanza hasikwambie mtu wanao ufaidi ni wachache saana.
Tumekumbwa na Haya majanga ila yanatufundisha na maisha yanaendelea. Bora umechukua umeona ulikosea wapi Imagine ndo pension... Unakufa na pressure. Tu wengi victims na hakuna cha ohh mara Mwl. Labda wapiga dilii.

Nashukuru kutufariji hata sisi tuliochemka .
 
Uchagani ukikopeshwa laki tano halafu ukafilisika inabidi Moshi uisikie tu kwenye vyombo vya habari maana utatengwa na kijijini kizima
Mkuu yani kama kwetu ukienda bila pesa wanakudharau wanaanza kukuambia si bora ubaki hapa nyumbani tu sasa unawekwa chini unaambiwa cheki yule fulani yupo kijijini lakini ana nyumba nzuri ww umeenda mjini kutafuta wanawake na starehe tu watakusimanga ukiondoka usipo zipata itabidi urudi kwenye sanduku tu
 
Mikopo si mibaya ndio maana utaona wengi waliopata changamoto ni kutokana na kupoteza pesa kupitia watu wengine waliowaamini. Pia kitu kingine kinachofanya watu washindwe kulipa ni tabia ya ku-divert fund ,yaani mtu anakopa mil 50 aziingize kwenye biashara lakini unakuta nusu ya hizo anapeleka kwenye matumizi mengine kama kununua gari mfano... Ila amini nawaambia mkopo ukiutumia kwa malengo yaliyokusudiwa sio rahisi ukashindwa kulipa. Hata hivyo uzi mzuri unafundisha japo hapa nilipo mbavu zangu zinauma kwa kucheka
 
Mmmh mkuu mbona hatar
 
hahahahhah nimechekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa sana. JF never boring kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…