Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Duhh ni kutunga au ni real? Ila mji huu umejaa matapeli asee. I wish huyo mnyeshewa nimpe hata pa kulala Maana leo kwangu kesho kwake. ...ila watu nao hawaaminiki asee
 
Wandugu hamjambo?
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, lengo ni kukutana sisi wajasiriamali na tupeane mbinu za kukuza vipato vyetu kupitia mikopo ambayo tunaipata kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.

Mimi binafsi niliwahi kukopa kwenye taasisi moja ya mikopo inayoitwa VISION FUND, lengo hasa la mkopo huo nilitaka kuongeza mtaji kwenye Grocery yangu. Lakini mambo yalienda vingine kabisa na kusudio na kujikuta mkopo huo ukiwa anguko kuu la biashara yangu!! Iliniuma sana na ukizingatia kabla ya hapo nilikuwa napata pesa nzuri sana kutokana na hiyo grocery yangu.
Mpaka nilijiuliza au mikopo hii ina mapepo? Niliachwa nikihangaikia marejesho ya hela ndefu kila mwezi, Alhamdulillah nimemaliza marejesho hayo mpaka ninaogopa kukopa tena aisee!!

Njooni tuelimishane namna ya kunufaika na mikopo hii.
 
Yawezekana ulichukua mkopo unaozidi mtaji wako , sasa kwenye marejesho ukakuta unarudisha na pesa yako ya awali ! Vipi kuhusu mzungo wa awali na baada ya kuongeza mtaji ilikuwaje?
Awali mtaji ulikuwa kama milioni moja tu hivi lakini nikifunga hesabu kwa wiki faida ilikuwa kama laki mbili na ushee kwa wiki moja,
Baada ya kuvuta mkopo ghafla mauzo yakapungua unreasonably na kujikuta narejesha mtaji directly mpaka nikajikuta mtaji uko mdogo mno aisee mpaka nikashangaa!!
 
Hapa yawezekana ulichukua mkopo unaozidi mtaji wako ! Baadhi yetu waga tunachukua mkopo mkubwa kuliko mtaji wetu na utata unaanzia hapo kwenye return. Mana unakuta kinacholipwa ni tofauti na kilichopo. Tuna kasumba ya kuwadanganya watu wa mikopo ili tupate pesa ndefu lakini mzunguko wetu unakuwa mdogo. Hii mwenyewe ilishanikuta.
 
Naona kuna ukweli ndani yake mkuu!! Maana returns zimekomba mtaji wangu na kuniacha hoi kwenye kagrocery kangu.
 
hahaaaaa mtoa mada niache manina ...umenikumbusha mbali mnoooo""" biashara yangu ilifilisika ...nilidataga kabisaaa yaani "" kuna kipndi nilikuwaga na madeni mpaka Simu kuishika naiona kama inawaka moto ....yaani kila SAA inapigwa tu dadeq ....

nakwambia hiviiii nimepitia kufiwa ..kuumizwa na mapezi lakini na thubutu kusema ...vyote hvyo hakuna hata kimoja chenye uchungu sawa na uchungu wa kufilisika ...sikia tu toka kwa watu kuwa Fulani kafilisika achaaaaa kabisaaaa
 
Asilimia kubwa ya wakopaji wa Tanzania hua hawafaidiki na mikopo kutoka taasisi husika na wengine mikopo hua ni sababu ya kufilisika na kurudi nyuma. Sababu hasa ni wakopaji wenyewe kutokua na elimu ya ujasiriamali na pia kurumia mikopo kwa namna tofauti na ilivokusudiwa

Sababu ya pili ni taasisi zinazotoa mikopo kua chanzo cha watu kushindwa kufaidika na mikopo hiyo. Taasisi nyingi hasa za microfinance zina kua na taratibu ngumu na za gharama kwa wakopaji na hazitoi mikopo kwa wakati. Jambo jingine ni riba kubwa ambazo haziendani na uhalisia wa wa faida inayotokana na biashara inayokopeshwa
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 

Huyo mdogo wako alifanikiwa kwenda shule? if not naomba unicheki
 
niwe muwazi tu kama mimi ndiye ningekuwa muhusika wa hii hadithi aiseee ningekuwa nimeshakufa kwa pressure.... nimepitia hali ya kufilisika naijua ilivyo aiseeeee"""" ila naona huyu kazidi kapitia mambo magumu mnoooo katika maisha Yke ...na kumbuka nilipofilisikaga nilidata kabisaaaa.....akili yangu ilikuja kukaa saw a baada yakukutana nawatu ambao waliwahi kumiliki ml.300 huko then wkaja kufilisika ..walipokuwa wnanipa simulizi zao kidogo zilikuwa zinanipa faraja ...ijapo kuwa wkati huo walikuwa wnanihadithia huku wakiwa tungi bwiiiiiiii kwaajili yakuondoa Mawazo .........maisha yamepoteza ramani lakini bado wanajipa moyo kuwa wtashinda vile vikwazo .....wakati huo nilikuwa naona kama mbingu imeniangukia .....acha kabisaaaaa.....jamani hela inaraha Yke kama hujawahi kuishika huwezi elewa hiki nacho kiongea hapa
 
hahaaaaaa hahaaaa
 
Uzi mzuri ila unantisha pia...maana panapo majaaliwa nategemea kuchukua mkopo next year, kwa ajili ya kujenga na kuanzisha biashara...

Wadau njooni mtiririke mauzoefu zaidi ili tujifunze kutokana na makosa na mafanikio pia.
Kwa mawazo yangu... Nafikiri ni busara zaidi kuanza mapema kidogo kufanya savings kwa ajili ya ujenzi / kuanza kununua baadhi ya materials za ujenzi kidogo kidogo na sio kutegemea mkopo kwa ajili ya ujenzi 100% Unless huo mkopo utakuwezesha kujenga kuanzia msingi mpaka kuhamia katika hiyo nyumba unayotamani kuijenga.
 
Pole sana Mungu atakusaidia yatapita... Jipe mda
 
Angalia usije ukapigwa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…