Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Kama huna usimamizi wa moja kwa moja baba hiyo pesa itapotea kopa mkopo wa muda mfupi kwanza at least 1yr ufanye hizo biashara ujue hasara na faida zake then next year uchukue pesa nzur uiboreshe hiyo business au uachane nayo

Trust me hutajuta
Wee jamaa ndo umeongea point kubwa mnoo 100%
 
Aiseee[emoji16][emoji16][emoji16]Umehongaa zotee
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!
 
Hahaaaa watu mna visa ninyi
 
Mteja gani ataekubali hii idea takataka?
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Peaa ya kutumia tu inaishaa dak sifurii mkuu
 
Kama ni 5mil tena bila riba na unakatwa 800k per month haiwezi kuchukua mwaka mzima.
 
Poleni kwa changamoto za hapa na pale wakuu, kama Mada ilivyo hapo juu katika harakati za kujikwamua unafika Mahali bora ukope ili uweze kufanya shuguli kama vile biashara na mengineyo.

Hata hivyo wapo baadhi ya watu tayari walikopa wakafanikiwa na wapo wakapata hasara hatimaye wakataifishwa Mali zao.

Naomba kwa wale waliokafanya ndivyo sivyo mje mtupe ABC zenu ili sisi tunaotarajia kuchukua mkopo tuchukue tahadhari kabla ya hatari Asante!
 
Tunafanana Mkuu.
2016 Nilichukua mkopo NMB 9,000,000.00
4.5 M Boda boda mbili za biashara.
1 M - Nilituma home kwa wazee kulikua na ujenzi wa nyumba ya washua.
3. 5 M sijui ilipoenda mpaka sasa.
matokeo
boda mbili zilikua za mkataba zilizaa boda moja, baada ya mwaka mmoja nadhani nilikula mtaji, bodi walipoweka makato nikawa napokea 195,000.00.
Naendelea kupambana na hali yangu.
 
Hii mpya ukope ujenge . Utachanganyikiwa hata barabara ya vumbi utavushwa na watoto.
Kuna mshikaji ni mtu wangu wa karbu mwez uliopita kavuta mkopo benk flan hv,,,sasa now hana kila kitu,,juzi kati tupo nae mzgon night,,kaamshwa toka usingizin kakurupuka anataja jina la ile benki,,dah mkopo bila malengo ni shida tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…