Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Mimi nimechukua mwaka huu, lakini ni wa mwaka mmoja. Mwezi wa tatu namaliza deni. Nilichukua ninunue boda boda lakini huyu jamaa niliyempa boda boda badala ya kuleta hela analeta stories. Yaani najuta kwanini nilichukua. Kuna wakati natamani niichukue halafu nipige bei ili nikalipe deni lililosalia lakini nahofia jamaa ni Kachawi kweli na baba yake nadhani ni msaidizi wa Lucifer mwenyewe, asije akanifanya mbaya bure! Basi najikaza kiume hivyo hivyo
 
Pole sana.
Ni moja ya changamoto za kimaisha.
Makosa yanafanya tunajifunza .
 
Eti mkuu kuna nyingine ipo FB wanajiita VICOBA FOCUS.

Wanatangaza unaweza kukopa kuanzia 5m-10m kupitia hiyo app yao kwa kujaza fomu inayopatikana FB na kutakiwa ulipe amana ambayo ni10% ya mkopo unaohitaji.

Naomba kuthibitishiwa huo mkopo kweli upo? Maana nina shida ya kuongeza mtaji kama 2m hivi.
 

Unaogopa uchawi bosi, utakufa masikini!! Waloge kabla hawajakuloga teh
 
pole mkuu...
 
Dah pole mkuu ila nimecheka mpaka watu wamesikia nikajifanya nakohoa...[emoji23] [emoji23]
 
Mimi katika vitu sitaweza kufanya ni kununua nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipa deni inanipaka simanzi sana.

Napata hisia si nyumba yangu nakosa uhuru nayo hasa ukizingatia ilipigwa mnada au aliuza bila kupenda.

Kuna jamaa yangu alinunua nyumba iiyopigwa mnada na bank alikaa mwaka mmoja tu baada ya hapo aliondoka na kujenga nyumba nyingine na ile anauza mpaka leo hajapata mtu.

Yule jamaa baada ya kupigwa mnada nyumba yake amekuwa chizi kabisa na familia imesambaratika huwa anapita hapo kwenye nyumba karibu kila siku na kuchorachora chini mambo yasioelewa pia kutamka maneno yasioleweka jamaama akaona isiwe tabu amejenga nyumba nyingine ila ndiyo hiyo nyingine hauziki kila mtu anajua historia yake.

So mkuu kuwa makini jiridhishe kama kweli jamaa anauza kiroho safi na haitamletea msongo wa kimawazo huku mbeleni pia vipi familia yake wanajua hilo?
huko mbele ya safari urafiki wenu utadimu? Jamaa atakuwa huru kukutrmbelea kwenye nyumba yako ili hali labda yeye amepanga?
Nakushauri usichekelee tu faidi ya kwako binafsi, mbona hiyo hela unaweza kupata eneo zuri tu ukaanza ujenzi kwa nguvu zako.
 
Mkuu karne hii unaogopa uchawi aisee kumbe uchawi unatulimit sana akili na maendeleo yetu.

Uza pikipiki au mpe mtu mwenye tija rudisha deni jipange ili next time ukope ukiwa umefanya reseach ya kutosha
 
Ni wazi wale tafuta uzi huku walijadiliwa sana hapa.
 
Ninaposoma hii comment yako ninampango wa kuchukua mkopo nikanunue bodaboda au bajaji, sasa hapa unanipa mashaka kidogo japo wanasema kama ukitaka kufanikiwa ukubali kuwa kuna risk

Pole kwa yaliyokupata, i hope njia nyingine inaweza kufunguka kwako
 
Hakuna Taasis inayotoa mkopo siku hiyo hiyo Labda mikopo ya kwenye Mitandao ya simu
 
Mimi huu ni mwaka wa 6 hati yangu ina hama tu kutoka benki hii kwenda benki hii.

Mkopo huu wa mwisho nilichuwa 10,000,000 unanitesa sana, Kwani sehemu kubwa nilipeka kwenye ujenzi badala ya kwenye biashara lakini nashukuru Mungu hata hivyo nimehamia kwangu tangu Julay 2017. Ingawa sijamalizia vizuri hata hivyo nasave 250,000 ya kodi ya nyumba ya kila mwezi.

Shida sasa ni marejesho kurejesha 1m kila mwezi kwa kutumia biashara si mchezo kwani biashara zimeyumba sana.

Nimejikuta biashara moja inakufa na ya pili inawnda rijojo na hii ya tatu ninayoitegemea sana hali si nzuri sana lakini natumaini nitamaliza marejesho kwani yamebali mawili tu nikamilishe.

Ilifikia kipindi unazima simu nakumbuka siku moja nilichelewesha kama miezi 2 na nusu hivi kiafisa mikopo kikanipiga biti mbele za watu eti tutapiga mnada nyumba yako wee siku hiyo nilimuwakia kidogo nimpige makofi nilifoka pale mpaka wateja wakanisupport hata walipokuja polisi ingawa walinitoa lakini walinielewa. Siku hizi hata nikichelewa hawanipigii simu.

Kwa sisi wafanyabiashara hatuwezi kuendelea bila kokopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…