Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Uzi mzuri ila unantisha pia...maana panapo majaaliwa nategemea kuchukua mkopo next year,kwa ajili ya kujenga na kuanzisha biashara...

Wadau njooni mtiririke mauzoefu zaidi ili tujifunze kutokana na makosa na mafanikio pia.
Hii mpya ukope ujenge . Utachanganyikiwa hata barabara ya vumbi utavushwa na watoto.
 
Mimi sio mkopo wa benki,ila ni hela ya heslb.niliingia kwenye network marketing bila ya kuifahamu vizuri,boom lote nililipeleka huko,nikahamia tena kwenye betting pesa zikaishia huko

Saivi najutia sana,kwani naishi kama jini vile,siku mbili kupita bila kula ni ishu ya kawaida tu.

Pesa kuipeleka sehemu fulani inabidi uwe umetuliza akili na upate ushauri mzuri pia.
 
Mimi nimechukua mwaka huu, lakini ni wa mwaka mmoja. Mwezi wa tatu namaliza deni. Nilichukua ninunue boda boda lakini huyu jamaa niliyempa boda boda badala ya kuleta hela analeta stories. Yaani najuta kwanini nilichukua. Kuna wakati natamani niichukue halafu nipige bei ili nikalipe deni lililosalia lakini nahofia jamaa ni Kachawi kweli na baba yake nadhani ni msaidizi wa Lucifer mwenyewe, asije akanifanya mbaya bure! Basi najikaza kiume hivyo hivyo
Tafuta mteja kubaliana nae halafu mwambie naomba uendelee kumtumia dereva wangu baada ya kukuuzia chombo. Halafu mwambie dereva wako kuwa umepata tatizo hivyo pikipiki unaiuza lakini asijali mama ataendelea kuwa dereva wa hiyo pikipiki...ukishauza kama ataendelea kumpelekea storie tajiri mpya itakula kwake na wewe utakuwa huna lawama nae tena
 
Yan habar hiyo isikie tu kwa mwenko
Kina jamaa alikuwa ughaibuni huko akawa anamtumia baba yake pesa amjengee nyumba na Raman akamtumia
Jamaa akarudi kumuulisa mshua nyumba iko WAP hamna nyumba ndio kwanza amechimba msingi na alishatafuna kama 75mls.
Sasa kama ndio ww utamfunga mzee wako au
Jamaa ucku ule ule aligeuka wakaenda kulala kwa hitel keshokesho yake hao Japan na mkewe
Una mpeleka magereza kwa wizi wa kuaminika
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
Pole Sana, ila Mungu atafanya njia paspo na njia
 
Hilo gari linakuingizia? Namaanisha ni la biashara? Una chanzo kingine cha mapato tofauti na hiyo kazi yako? Kama majibu ni hapana kati ya maswali hayo mawili nakushauri usichukue.
sometime mikopo ya nyumba kwa watumishi haikwepeki, sio kila mtu anaweza fanya biashara. wengi wamekopa biasharab zikaenda kombo kwa sababau usimamizi sio mzuri, so ukikopa ukajenga au kun unua gari pesa yako utakuwa unaiona.
 
Na mwakani nachukua pesa nyingine kama 10 MLS. Hivi nifanye mambo coz nimeshajua wap nilikosea so i jst wanna correct my mistakes so tuzidi kuombeana ntawaletea feedback hapa hapa jukwani waoga endeleeni hivyo hivyo kujifungia chumbani
mwakani ndio hii na imebaki miezi miwili tu tuanze mwakani nyingine,leta mrejesho hapa
 
Juzi kati tu hapo nimevuta milioni 5 na mpaka sasa ishaisha na sioni cha maana nilichofanyia.Nakatwa 800K kwa mwezi kwa mwaka mzima ila nashukuru ni mkopo wa ofisini hauna riba.

Nilikopa kabla ya kufanya tathmini nzuri ya biashara nikajikuta naipeleka kwenye mambo ambayo hayakuwa priority so nimejifunza kitu.
 
Back
Top Bottom