Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Pole mkuu...maisha lazima yaendelee
 
Kuna viofisi ukifika wafanyakazi wana hali mbaya sana.

Wenye afadhali ukiachana na boss utakuta ni Accountants na watu wa Procurement.
Kama zile ofisi za almashauri [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hawa no Wala rushwa wazuri hasa kwa wahindi ..hawafai kabisa mkuu. Mimi wakati bado sijatoka bongo niliwahi peleka mashtaka sehemu nlokuwa napiga kazi. Aise hamna kitu hapo watakupiga danadana maana boss no muhindi so anawatoa tu basi hamuna kitu watafanya
 
Kipindi Mkapa anaingia madarakani mabeberu walimshauri apunguze wafanyakazi wa serikali naye akakubali. Pale ofisini kulikua na watu wa IDM Mzumbe, IFM na sisi wa Mlimani (UDSM).
Kulikua na uhasama wa chini chini Kati yetu kwa upande mmoja na wale wa advanced diploma za IFM na IDM.
Waraka wa Chenkapa ukaja idarani kwamba baadhi ya watu wapunguzwe.
Aisee, aliye pewa kazi ya ku earmark watu wa kupunguzwa alikua mtu wa IDM. Hakufanya kosa, barua ya kwanza, ya pili ya tatu Ni yangu. Kipindi kile bar zinauza beer kuanzia saa mbili asubuhi, Basi nilizama bar moja kule mjini karibu na benki ya NMB.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] dah haya mambo bhana acheni tu. Pole mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilipata kazi kwenye kampuni kubwa sana hapa nchini, hii kampuni Ina makao makuu mjini na branch moja Chang'ombe Dar. Basi baada ya kupata Ile kazi nikaambiwa kituo changu Cha kazi itakua branch. Mimi nikachukua taxi mpaka branch kuripoti. Kufika nakuta meneja wa branch Ni jamaa tulisoma nae form five na six, pale nilitakiwa kua assistant wake. Jamaa wa IT Ni mshamba mmoja nilisoma nae UDSM course tofauti yeye computer science. Aisee mnajua fitna, hata Rage Ile fitna haifikii.
Kwanza meneja aliniambia sitapewa gari wakati magari pale yako mawili moja lake jingine la assistant.
Pili kaniambia ngoja akaongee na makaburu halafu atanipigia simu.
Sijui aliwaambia Nini makaburu mwisho wa siku hakunipigia na Mimi sikuhangaika nae. Kipindi kile kazi zinatafuta watu.
 
then ikawaje mkuu/ uliachaje kazi?
 
Kuna mfanyakazi mmoja ameachishwa kazi baada ya kupata msiba watu wameenda kumpa pole kufika wakakuta mjengo wa maana
Alivyorudi kazini anaulizwa hela ya kujenga nyumba kama hii kaipata wapi
Binadamu wana mambo.

Kuna bwana mdogo mmoja alifukuzwa kazi baada ya bosi kuona furniture alizonazo wakati anahamia nyumba ya kampuni. Nakumbuka yule mzee aliongea sana na kuanza kuuliza maswali kwetu bwana mdogo vitu ametoa wapi. Visa vikawa vingi, haukuisha mwezi akapigwa chini ila Mungu mwema dogo akapata kazi in two weeks maisha yakasonga.
 
Nimewahi fukuzwa brack kinyemelaa na wahindi mwak 2013 bila kujipanga vxr nilienda asbh Kama kawa cku ya mshahara na wale wanatoa mshahara cash kwamkono nilipo pokea tu cash yangu hapo hapo nikapewa na ya kutimuliwaa nikarud kijini mda kidg nikapata tanesco cjakah sawa nikatimuliwa Tena na hr kwakumfidhia meneja hayupo bas aliyepewa kukaimu wakanipitisha HV ..kisa na mkazaa hr alisema mm na mzee mmoja tulimpiga majungu kwa kupenda kuajir wapare ndugu zao ambao baadhi. Hawajasom shule ..bas nayey katika sekeseke la vyeti vyeki magufuli akamla kichwa juu kwa juu

Nilirudi Tena kitaah na watu wengi walishajuwa Niko tanesco nilichukia sana ila nimewasamehe ...
Tatu nilifukuzwa kampuni ya Sola kinyemelaa pia kwakufitiniwa na ndugu yangu eti kaenda kuwaambia maboss kuwa portfolio imenishinda bas duh ach kbsa ...
 
Pole sana mkuu. Hope umekaa vizuri now.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…