Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
[emoji2] [emoji3] [emoji1]
 
Kulelewa sehemu ambako siko kwa wazazi wangu kulinipa motisha ya kusoma niondoke pale nilipokua nakaa. Sikufukuzwa ila sikua comfortable Na maisha ya pale. Niko radhi nikaishi kwa rafiki ila sio kwa ndugu. Wakati Niko high school nilikua nakaa kwa ndugu basi tu sina jinsi ila roho ilikua haina amani. Sasa hivi hata nikienda kwa ndugu nashinda jioni narudi kwangu. Sina kabisa mazoea mazoea Na ndugu. Naweza kaa hata miaka miwili sijaenda kwa ndugu yeyote Kama tusipoonana kwenye shughuli ndo imetoka hiyo ndugu kumuona
 
Nilikaaga kwa ndugu kipind nasoma!sio ndugu wa karibu saaaaana! Nilichokuwa nakifanya...nilikuwa nafanyakazi km punda hata kule kwetu ckuwa nafanya! Naamka alfajiri nawasha mashine yakufua naanza kufua nguo, machine inaendelea kufua nafanya kaz za ndani, kuaandaa chai ya asbh n.k na kaz nyingine zote nikilala usiku km punda nmechoka + watoto! Mama mwenye nyumba kiguu na njia!
Cku nikifunga shule nakwenda kwetu,shule zikifunguliwa cku ntayoingia ile nyumba naanza na usafi jikoni store ambapo huwa nakutana kumeoza! Yule mama alikuwa Ana chukichuki na watu lkn alkuwa ananipenda ajabu! Akirud safar zake anakuta mambo yote yapo sawa! Lazma huwa anibebee zawadi pesa alinipa n.k! Alifurahia uwepo wangu hata watoto wake walinipenda Sana,!
Nilipomaliza form six alinizawadia cheni ya dhahabu hereni na Pete! Ckuamini!
Jaman hakuna MTU dunia ya sasa anaetaka kukaa na MTU..hata ndugu hawatakani! Tunapokaa na watu inabd tu tujitutumue tujipendekeze ilimradi tusichokwe!
MTU anaenda kukaa ugenini labda anasoma n.k unaleta uvivu jeuri kiburi yaan hapo lazma uchokwe!
Mschna unaenda ugenini unalala masaa yote..ukiamka kaz zote zmefanywa mpaka chai umeandaliwa! Aibu...hata km hakuna kazi..amka tuu! Jifanyishe kitu chochote kile..omba hata viguo ufue tuu utathaminiwa!
Tusilalamike kufukuzwa kuteswa kumbe sisi wageni ndio wenye shida! Japo kuna case nyingine ziko tofaut kidogo

Kweli kabisa cha Msingi tuishibkutokana na mazingira sio kuendekeza ukwenu
 
nilifukuzwa na shangazi yangu .kipindi hicho nipo form 2 .nikaenda kwa brother wangu wa damu kabisa akanifukuzwa asububi asubuhi.nikaenda kukaa na mother chumba kimoja alichopanga yeye analala kitandani mimi chini .nilikaa na mother kwa chumba kimoja mpaka nikamaliza form 4.sasa hivi nimeoa najitegemea ,yule brother yupo yupo tu hana mbele wala nyuma hajaoa .nimefupisha tu ila nina story ya kuhudhunisha sana hadi hapa nilipo fikia
 
Kwa watu hakufai...nimezaliwa miaka mingi iliyopita...ila nilisimuliwa nilipozaliwa mama alikuwa akiishi kwa kaka yake...ile kukojoa kwangu kama kichanga kitandani mama akatimuliwa...nilisimuliwa hadi leo huyo mjomba namwona Hitila....yeye amesahau mimi nakumbuka!
Hii inatolesha machozi
 
KUNA TWO SCENARIOS!
Baada ya wazazi kufariki, mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na baba yetu mkubwa!
Life wasn't tht okey but Yatima hadeki ujue! maisha yakasonga!
Siku moja ilikuwa mkesha wa pasaka, mdogo wangu na watoto wa baba yangu mkubwa (walikuwa wakubwa zaidi yangu)
Wakaenda kanisani mkesha! mi nilikuwa naumwa sikutaka kusali usiku.
Walikuwa wadada watatu,Mmoja akaona ndio wakati wa kwenda kuchachua ,wanarudi nyumbani bila yeye!
Baba yangu mkubwa anamfokea mdogo wangu(ninayemzidi miaka 5, anaaambiwa arudi alikotoka na asirudi mpk atakapompata yule asiyerudi home). Yule baba alifunga mlango ,nje bariki kali nyumba ipo milimani flan hvi!He was asthmatic, hata kama asingekuwa asthmatic ,how on earth unamwambia mwingine asilale mpk aliyeenda kwenye starehe zake arudi!
Nilikaa ndani kama nusu saa hivi nikiwa nalia!
Nilipotoka nilienda subeleni unapokaa funguo haukuwepo!means ameingia nao kulala!
Nilliingia jikoni nikachukua shoka lile nafikir ,Nililinyanyua juuu kushuka chini kishindo kiliamsha mpk sisimizi!
wakaamka, ananitishia kunipiga!NIKAMWAMBIA NEXT STEP AFTER WHERE YU ARE NAKUPASUA!

nilifunguliwa mlango nikamfuata mdogo wangu alipo nikamwingiza ndani!
kesho yake asbh kabla hajasema ondoka au baki nilikuwa nje na mabegi na mdogo wangu namwambia tunarudi kwenye nyumba ya wazazi!

2. Huko kwenye nyumba ya wazazi alikuwepo mama yetu mdogo na wanae!
NAKO MAISHA YALIKUWA YA KIWEHU TU KWA DOGO!!
huko nilifukuza mimi!
Nikamwambia unajua nini, HII NYUMBA NI YA MAMANGU, isingekuwepo wewe ungekuwa unalipa kodi!
SASA FANYA HIVI!
NAENDA KUMALIZA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA! nikirudi uwe umetafuta pa kukaa!
ilikuwa ni likizo ya mwezi wa nne ,pepa ya necta mwezi wa tano!
Niliporudi nilimkumbusha!
MPAKA KESHO I AM THE LAST PERSON KWENYE FAMILIA KUAMBIWA TAARIFA YOYOTE INAYOHITAJI MAAMUZI YA PAMOJA
😁😁😁The Gangstar against the clan
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
Dah umenifurahisha sana
 
Misimamo ya kutokubali kunyanyaswa inafanya wengine tuchukiwe na ukoo mzima😂😂😂 hizi mambo Ni inborn navyowasumbua mababa wakubwa, wadogo mashangazi wajomba na mama wadogo nadhani wanajuta kuzaliwa kwangu,, Basi imesaidia hata wadogo zangu na mama yangu kuogopeka Kwamba Fulani akijua utajuta huo mtiti wake, Ni rahisi kutendwa kimapenzi nikapotezea ila usifanye unyanyasaji kwa ndugu yangu wa damu,,,,,nitakiwasha tu

Nimepitia manyanyaso mengi kutoka kwa ndugu ila kanuni yangu Ni moja siujui unafiki ukifika muda wa kupasua ukweli, napasua usiponisalimia nami sikusalimii imetoka hiyo
 
Duuuh tangu saa 11 asubuhi nasoma comment hadi comments nimeishiaa ya 188[emoji3][emoji3].

Nlipokuwa mdogo nlikuwa napenda sana kutembeleaa ndugu ila saivi nimekuwa , nimeujua ukweli wa mambo.

Nkiambiwa bwana mdogo njooo usalimiee ma uncle huku, naitikia nakuja lakini najua siwezi kwenda.

Kiufupi nikikutembela kama ni mikoani lazima niwe na hela ya kurudia.

Hatuwezi kukwazana then nikuombe nauli ya kuondokeaa.
In short na kera na napenda sana haki ,ilihali najuaa ukiishi kwa familia ya mtu mwingine huwezi kuwa treated the same way kama born inmates wa pale.
 
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
[emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu umenichekesha sanaaa
 
[emoji3]

Hii comment ni balaa.
Nakumbuka ilikuwa Dar mitaa ya Sinza Vatican, nilimtembelea ndugu yangu, asee jamaa alikuwa mkorofi balaa. Akirudi toka kazini lazima aguse li TV lake la uchogo, kama limechemka huo moto wake hata kwa gari la zima moto hauzimiki!!

Siku ikipikwa nyama anahesabia jikoni. Mkishakula lazima ahesabu zilizobaki.

Vitimbi vilikuwa vingi na alikuwa anatusurubu ka vile si ni wafungwa!! Siku moja nilitoka nduki kali, sikuwahi kurudi huu ni mwaka wa 11.

Nilipofika home mkoani nilimsimulia mama, siku hiyo alinipikia kilo nzima ya wali, akapakua kwa sinia kubwa na juu kasimika bakuli kubwa la nyama za kuku! Nilivua shati kuanza kutupia nyali tumboni huku nikijisemea, "ewe ndugu mchoyo wa Dar, njoo uhesabu minyama inayoshuka tumboni"
 
Nikikua likizo kwa ndugu sasa bahati mbaya siku nikasahau sijui ndo kupitiwa sikumsalimia asubuhi akanambia niondoke kwake yaan nilishangaa sana. Na siku zote nlikua namsalimia
 
Back
Top Bottom