NAPITA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,077
- 2,246
wewe hujawahi kukimbia?
Sijawai kukimbia hata siku moja mpaka nimebahatika kufunga ndoa sikuwa na mtoto wa nje ya ndoa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wewe hujawahi kukimbia?
Sitasahau kisa hiki, kipindi hicho nimemaliza shule ya msingi na kubaki mkulima tu kijijini kwetu, nikaanza kutembea na mtoto wa shule, hamadiii!! akapata mimba, siku hiyo mida ya jioni naona wazee wameongozana na yule binti, wakagonga hodi baba katoka, nikajua msala huu, nikapitia dirishani na kupotea, kesho yake nikatimkia kijiji cha jirani kwa mjomba wangu, nilikaa huko takribani miaka 3 ndo nikarudi nyumbani nikakuta nina katoto kabinti kazuuuriii. Najutia kosa hili. Karibuni wenzangu tuliowahi kukututwa na mkasa huu, ilikuwaje siku hiyo na kwa nini ukimbie? Mimi niliogopa kufungwa wakati huo sheria ilikuwa kali sana.
Hivi wewe hujawahi kimbiwa kabla sijkuona..??? Maana inasemekana wanawake walio wengi, wanaowaita watoto wao wa kwanza, si wa kwanza... WENGINE NI WATATU, WENGINE WA SITA... etcbaada ya kurudi mama mtoto ulimuoa au.............
Ndo group gani hiyoo..??Mimi Siwezi telekeza mtoto..tuna damu ya uongozi na utajiri...kila damu yetu tunaithamini
Ndo group gani hiyoo..??
Hivi wewe hujawahi kimbiwa kabla sijkuona..??? Maana inasemekana wanawake walio wengi, wanaowaita watoto wao wa kwanza, si wa kwanza... WENGINE NI WATATU, WENGINE WA SITA... etc
Tatizao mna siri sana... Si unamuona yulee aliyemuweka mtoto kwenye box... Utadhani alitaka kumsafirisha kama mzigo..hapana ningeshakueleza kila kitu
Itakua group O nadhani
Kaka zangu nawahusia msikimbie mimba nina mfano hai kuna jamaa alikimbia mimba kwenye ujana wake na kumkana mwanamke kwamba jamjui basi bi dada kasepa jamaa kamaliza shule zake umefika wakati wa kuoa manake tayari kazi nzuri na mambo kibao ya kuvutia sasa kaoa huu mwaka wa kumi na tano no mtoto wala nini lol inasemekana bidada alimwambia jamaa unakataa damu yako? Basi mungu atakupa wengi kama nzige , jamani hili ni la kweli. My Take bora ufanyr DNA ujiridhishe kuliko kupata huzuni kama hii ni mbaya.
Halafu mnasema wanawake wakatili wanatupa watoto jalalani. Kama hakuwa na a good support system (familia nk), kama hao wangemfukuza unadhani yeye angeleaje huyo mtoto muda wote huo wewe umekimbia? Wanaume wana luxury ya kukimbia na kuendelea na maisha yao kisha kurudi baada ya miaka 3 na kukuta "ana katoto kabinti kaziriiiiii"! Mfikirie huyo mwanamke ndani ya hiyo miaka 3 kachakaa vipi, na wengi wao shule ndo basi tena
Hii tabia sio nzuri kabisa,sasa umeisha oa au bado? What goes around comes around hivyo bado majibu mengine utayapata...Ili kupunguza ukali anza kujikomba mapema na ubebe majukumu yako kama baba.
Jamani najuta, tayari nakatunza kabinti kangu kazuuriiiii.
Ha ha ha ha haha, unalo hilo group nije nichanganye mbegu?
Ujue zombie ana grupu A-, linaambatana na majanga tu.
asante mkuu, ulipambana nao vipi na ilikuwaje?
Kukimbia mimba hodari!ndo nyie mwisho wa siku mtoto kawa na mafanikio hamkawii kujisogeza na kujitambulisha kuwa wee ndo baba yake!nina chukia sana wanaume wanaokimbia mimba.