Uuuuph, sitakaa nisahau, kwanza nitangulie tu kusema Mungu yu mwema, ilikuwa ni sa2 natoka mwenge kwa pikipiki naendesha mwenyewe, pikipiki BAJA cc250, Chuma kimekolea na njia ni nyeupe, naendesha kuelekea ferry kwenye pantone, ghafla nafika maeneo ya palm Beach kwenye mgawanyiko wa road, sijui ni nini kilitokea, pikipiki ilikataa kukata kona nikaparamia kuta ama kingo za bara bara, sawa Mimi ni mtundu wa pikipiki lkn kwa pale sijisifii ujinga, ni Mungu pekee, sijui nihadithie vipi maana kila aliekuwa karibu alilia kwa anavyojua yeye, basi mwisho nilidondoka na pkpk yangu, waliokuja kutoa msaada walidhani nimeshasafiri kwa baba but steel nilikuwa mzima, nikaliamsha japo ilivunjika, nikawasha ikawaka, sasa kosa wale jamaa waliniruhusu kuondoa, ilhali bado Nina mawenge, nili loose direction kabisa, akili iliruka na nilikuja kushtuka nipo uwanja wa NDEGE, usicheke!!! Dah,,,,
Sent using
Jamii Forums mobile app