Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Mmeoana lkn
 
Natamani ningekuona ukifanya yako huku machozi yakikutoka Mkuu, bila ya shaka uliwatoa machozi wengi sana pale ukumbini. Poleni sana Wakuu wote Mwenyezi Mungu ni mwema sana.

 
Ashukuriwe Mungu kwa ushuhuda wako tusiache kufanya mambo ya kumpendeza
 
Kuna siku moja wakati natokea Moro Na Abood.Ghafra magari yakawa yamesimama kuulizia eti.Kuna gari do go limeingia chini ya semitela.Tukashuka baadhi kwenda kuangalia.Aiseee kweli kama hukupangiwa kufa hufi.Ni nini ??pamoja Na gari kufinywangwa Dereva pekee aliyekuwa ndani ya gari alitoka nzima kiasi cha watu kuanza kumpigia vigeregere Na yeye asiamini kilichotokea.Nakumbuka nilienda Kumpa mkono.Na sio kwamba aliruka wkt ajali inatokea.Alikuwemo ndani Na watu kumtoa.( Hallelujah)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani ningekuona ukifanya yako huku machozi yakikutoka Mkuu, bila ya shaka uliwatoa machozi wengi sana pale ukumbini. Poleni sana Wakuu wote Mwenyezi Mungu ni mwema sana.
Ahsante kk,ilikua kitu live wee acha tu aisee [emoji16][emoji16]
 
Reactions: BAK
Duh Mzee una majanga......hata hivyo inaonyesha sio dereva mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hallelujah amen
 
Poleni kwa wote mlionusurika kupata umauti baada ya ajali hizo mbaya, poleni sana na hata Mungu azidi kuwalinda na kuwapa uzima maradufu.
 
Mh,mshana daraja linahamaje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uuuuph, sitakaa nisahau, kwanza nitangulie tu kusema Mungu yu mwema, ilikuwa ni sa2 natoka mwenge kwa pikipiki naendesha mwenyewe, pikipiki BAJA cc250, Chuma kimekolea na njia ni nyeupe, naendesha kuelekea ferry kwenye pantone, ghafla nafika maeneo ya palm Beach kwenye mgawanyiko wa road, sijui ni nini kilitokea, pikipiki ilikataa kukata kona nikaparamia kuta ama kingo za bara bara, sawa Mimi ni mtundu wa pikipiki lkn kwa pale sijisifii ujinga, ni Mungu pekee, sijui nihadithie vipi maana kila aliekuwa karibu alilia kwa anavyojua yeye, basi mwisho nilidondoka na pkpk yangu, waliokuja kutoa msaada walidhani nimeshasafiri kwa baba but steel nilikuwa mzima, nikaliamsha japo ilivunjika, nikawasha ikawaka, sasa kosa wale jamaa waliniruhusu kuondoa, ilhali bado Nina mawenge, nili loose direction kabisa, akili iliruka na nilikuja kushtuka nipo uwanja wa NDEGE, usicheke!!! Dah,,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwanja wa ndege kivipi tena..ulikuwa wapelekwa nje kwa matibabu nini
 
Weka uliyopata wewe hiyo aje boy friend wako asimulie hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2005 nilianguka na baiskeli kwny mteremko wa kilima cha kinyonga huko Maneromango nilipata homa na "mtoki" juu...mpk leo nina makovu[emoji52][emoji52]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…