Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa



Hii mpaka leo ipo kichwani mwangu. Siamini hta niliponaje. Niltoka bila hata mchubuko wwte.
 
Bado uko nae?
 
Umenikumbusha 2004 magomeni kwa bibi nyau na basi la sinza-gongo la mboto sitaisahau hii siku japokuwa nilikua mdogo sana
 
Kwa watu sensitive, watu waliopoteza ndugu zao kupitia ajali, huu uzi unaweza kuwa kidonda kibaya.

Poleni wote mliopitia ajali na leo hii mnatoa shuhuda.
 
Ajali nyingiiii ni uzembe wa dereva pamoja na uchakavu wa miundombinu tuwe makin tutumiapo vyombo vya moto
 
Natumai hamjambo wakuu,

Kusafiri imekua sehem ya maisha yetu ajili yakutimiza majukum yetu japo kuna nyakati hugharimu maisha na kusababisha vilema kwa manusura.

Binafsi nimenusurika mara kadhaa but mara ya kwanza nilikua natoka Moro-Dar kwa gari ndogo, tairi ya mbele ilichomoka gari ikabinuka matairi yakawa juu bt mungu ni mwema hakuna aliedhurika sana isipokua majeraha madogo.

Mara ya pili Kigoma-Mwanza kwa bus, basi liligonga ng'ombe wanaokatiza karibu 20 nakupoteza mwelekeo kila1 wetu alisali sala ya mwisho akijua hakuna kupona bt mungu ni mwema tulinusurika gari haikuanguka.

Mara ya tatu, ilikua kwa dala dala gari lilishika moto mbele kila mtu aliruka kujiokoa, hapa nilipata majera kiasi ajili ya heka heka zakujiokoa.

Karibu nawe utupe visa vyako.
 
Nilipata ajali mbili ndani ya week moja, ya Kwanza daladala ya Mbagala - Mwenge, tuligongwa na Fuso, pili Gairo kondoa na mj bus, lilikata break kwenye mteremko mkali bahati nzuri halikuingia korongoni.kifo kimoja na majeruhi kadhaa.
 
Mimi nakumbukuka ilikuwa arusha ndege baada ya kuruka mda kidogo tulisikia muungurumo kwenye engine afu kitu kikashuka chini karibu na mashamba ya burka. Tulipona wote isipokuwa majeraha kidogo kwa waliokaa upande was dirishani✈✈
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…