Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

b70b1db909d4b634aded0a0edf480168.jpg


Hii mpaka leo ipo kichwani mwangu. Siamini hta niliponaje. Niltoka bila hata mchubuko wwte.
 
Ajali nyngne boyfriend wng alipata 2012 alitoka club ananifata mimi nipo sinza katokea posta na kalewa basi mie nampelekesha bwana mie narudi nyumbani kama hutaki kuja yani nikikaa dk 2 sim dk 2 sim jamaa katoka posta mkuku na gari ananiwahi mie bwana we kufika kijitonyama akala mzinga uso kwa uso sasa nimekaa kama 1 hour mtu hafiki napiga sim ipo busy kutwa kumbe yupo hospital mwananyamala wanahangaika kupiga sim yake no yangu hao wasamalia wema ndo kupiga tena nikampata kuongea nao wananiambia jamaa yko kapata mzinga knyama njoo mwananyamala hospital yani sikuamini nikamkuta kapasuka kichwani alishonwa nyuzi kama 10 uso umeumuka madamu kibao nusu nizimie nililia jamani nilikua nimekunywa bia5 zote ziliruka aisee ajali iskie tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado uko nae?
 
Umenikumbusha 2004 magomeni kwa bibi nyau na basi la sinza-gongo la mboto sitaisahau hii siku japokuwa nilikua mdogo sana
 
Kwa watu sensitive, watu waliopoteza ndugu zao kupitia ajali, huu uzi unaweza kuwa kidonda kibaya.

Poleni wote mliopitia ajali na leo hii mnatoa shuhuda.
 
Ajali nyingiiii ni uzembe wa dereva pamoja na uchakavu wa miundombinu tuwe makin tutumiapo vyombo vya moto
 
Natumai hamjambo wakuu,

Kusafiri imekua sehem ya maisha yetu ajili yakutimiza majukum yetu japo kuna nyakati hugharimu maisha na kusababisha vilema kwa manusura.

Binafsi nimenusurika mara kadhaa but mara ya kwanza nilikua natoka Moro-Dar kwa gari ndogo, tairi ya mbele ilichomoka gari ikabinuka matairi yakawa juu bt mungu ni mwema hakuna aliedhurika sana isipokua majeraha madogo.

Mara ya pili Kigoma-Mwanza kwa bus, basi liligonga ng'ombe wanaokatiza karibu 20 nakupoteza mwelekeo kila1 wetu alisali sala ya mwisho akijua hakuna kupona bt mungu ni mwema tulinusurika gari haikuanguka.

Mara ya tatu, ilikua kwa dala dala gari lilishika moto mbele kila mtu aliruka kujiokoa, hapa nilipata majera kiasi ajili ya heka heka zakujiokoa.

Karibu nawe utupe visa vyako.
 
Nilipata ajali mbili ndani ya week moja, ya Kwanza daladala ya Mbagala - Mwenge, tuligongwa na Fuso, pili Gairo kondoa na mj bus, lilikata break kwenye mteremko mkali bahati nzuri halikuingia korongoni.kifo kimoja na majeruhi kadhaa.
 
Mimi nakumbukuka ilikuwa arusha ndege baada ya kuruka mda kidogo tulisikia muungurumo kwenye engine afu kitu kikashuka chini karibu na mashamba ya burka. Tulipona wote isipokuwa majeraha kidogo kwa waliokaa upande was dirishani✈✈
 
Back
Top Bottom