Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Kweli ndo maana jicho lako moja dogo
 
Nilikuwa nimechukuwa likizo ninaenda kuoa mkoani Kigoma.

Siku niliyoenda kukabidhi ofisi ili kesho yake nianze rasmi likizo yangu nikiwa njiani nilipata ajali mbaya sana nilikuja kustuka siku ya tatu nikiwa hospital ya Muhimbili ,taya imevunjika mpaka leo siwezi kula muwa.

Nililala Muhimbili miezi mitatu kabla ya kuruhusiwa nikiwa nimewekwa nyaya kwenye meno ili kuzuia kinywa kisifunge kuruhusu mifupa ya taya kuunga vizuri na jicho langu la upande wa kushoto ni dogo sana .

Yaani nilipozinduka nilikuwa kwenye wodi ya SEWAHAJI pale Muhimbili nikaenda chooni kujisaidia haja ndogo nilipojiangalia kwenye kioo cha kule chooni sikuamini kama ile ni sura yangu maana ilikuwa imevimba sana na jicho langu la kushoto halioni kabisa.


Sipandi pikipiki mpaka leo kwa jinsi nilivyonusurika.
 
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa saba natoka dar na CITY BOY tulipokaribia manyoni basi likagongana uso kwa uso na CITY BOY ya kutoka mwanza zaidi ya watu 30 walipoteza maisha nashudia Mungu saidia skuumia hata kidogo.sitaisahau sku hyo maishani
 
Inasikitisha poleni Ila nimecheka sana
 
Pole sana
 
Mi nakumbuka tukiwa njiani hamadi semi trela hii hapa! Hadi leo sijui kilichoendelea...
 
Ilikuwa mwaka 1997 tunasafirisha maiti toka Dar kwenda Iramba mkoani Singida tulifika salama Dada akaniambia tushukuru tumefika salama pale pale nikawa mnyonge sana nikajikuta namwambia ila wakati wa kurudi tutaanguka na gari sijui kwa nini nilisema hivyo Dada akanikataza nisiseme hivyo Mimi nikamjibu kweli Dada. Tukazika na kuanza safari ya kurudi ile tunaanza safari nikamwambia Dada laaaah tunakwenda kuanguka masikini sijui tufanye nini? Dada akaniambia usimsemee hivyo nikamwambia kweli. Kutoka Singida tukafika pale ambapo ukinyoosha unakwenda Arusha ukikata kulia unapitia Dodoma mkuu wa msafara akamwambia driver nyoosha tupite ya usandawe ilikuwa ni jioni Mimi nilikuwa kiti cha pili nyuma ya driver nikamwambia driver kwa sauti kata kulia pita ya Dodoma, driver akauliuliza nimsikilize nani? Nikamwambia Mimi, mkuu wa msafara akasema nyoosha halafu akaniuliza kwanini umesema hivyo ile sauti ya kufoka nikamjibu Barabara zote mbili tutaanguka hii ya Dodoma tutapata msaada hii ya usandawe nani atatusaidia? Kanijibu hoja dhaifu driver nyoosha, nikamwambia Dada naogopa ajali Mimi nalala nisione tunavyoanguka, Dada akasema usiseme hivyo mdogo wangu nikamwambia kweli dada, nikalala muda mrefu baadae nikastuka nikamuuliza Dada hatujaanguka? Akaniambia wewe, nikamuomba nikae upande wa dirishani aliponipisha nikamwambia nalala Mungu atunusuru jamani, nikalala kama saa tatu usiku hivi nikastuka usingizini gari inayumba vibaya sana mara tukaanguka ni kiza kinene, mvua inanyesha na tupo porini peke yetu watu wakatokea madirishani maana mlango upo kwa chini Mimi nikawa nimebanwa kidogo na kiti cha mbele yangu halafu na ule usingizi nikaamua nilale tu, kule nje wakagundua sipo ikabidi waanze kuniita kuchungulia Giza nikawaambia sitoki wakanibembeleza nikatoka nina hasira ile mbaya siongei na mtu. Mkuu wa msafara akamfuata driver anataka kumpiga Mimi nikamwambia nilikwambia tukiwa Singida ukanidharau hakuna msaada hapa nyanyueni gari tuondoke, ikabidi wafanye hivyo huku wanalalamika maumivu Bahati nzuri iliwaka tukaondoka kweli Mungu ni Mkubwa yaani ukiona hiyo gari huwezi Kuamini kama itatembea na haikuua Ila majeruhi, kufika Dodoma tukabadilishiwa usafiri. baada ya muda nikawa na maumivu ya mgongo, hizi zingine ambazo ni mbaya zaidi kwangu nazihifadhi Ila Mungu ni Mkubwa kisichokuwa kikupate hakikupati
 
nimepata ajali nyingi ikiwemo za pikipiki na sababu kubwa ni ulevi!ila ajali iliyonitia akili ni mwaka huu siku ya juma3 ya pasaka niko na mshkaji wangu tumelewa ile chapachapa baada ya kuendeleza gambe toka pasaka!tuko na haria kufika sehemu flani ilikuwa mida ya saa 8 mchana jamaa alikosa kumgonga mtu wa bodaboda mi sikuwa na habari ya chochote wakati huo nimelala kwenye siti wale bodaboda wakaanza kufkuza gari huku wamebeba mawe ili wavunje vioo jamaa wangu akapata wenge na zile akaweka mafuta ya kutosha ilikuwa spidi 130 hivi kwa mbele kuna gari inaingia upande wa kulia yaani basi tukaigonga ile gari kishindo ndo kikanishtua usingizini nikaona gari imepaa mara miti inazunguka huku kurudi naona mawingu juu angani na sikuwa nimefunga belt.nikawa naskia kelele watu wanasema itakuwa wamekufa hawa,nilivyoskia hvyo nikasema embu niinuke nijue km nimekufa nikajiona mzima nikamvuta mshkaji miguu hadi nje akaamka tukaondoka eneo la tukio tukaenda baa ya jirani tukaendelea kunywa hadi askari walivyotufata tukalala nondo.ila mungu mkubwa hatukupata hata skrechi na gari ilipinduka zaid ya x7 gari hakuna fundi amesema itafaa tena hata irudishwe japan ni skrepa tu
 
Mungu ana mipango na maisha yako mshukuru amekupa kilema cha jicho ila kuna wengine walikatika mikono wamepata strock ila wanamshukuru Mungu kwa uhai
 
nilicheka sana siku moja deiwaka kapewa akalaze hiace mida ya saa 4 usiku.
kapiga kona kubwa kuingia kushoto kumbe bodaboda inakuja ikagonga upande wa kushoto pembeni dereva ile helmeti ikachomoka ikaingia ndani ya hiace kwa wenge dereva akajua kichwa cha bodaboda kimekatika na ile helmeti ilikuwa nyekundu afu usiku jamaa akapata mawenge kila akiangalia pembeni yake anajua kichwa anazidi kukanyaga mafuta hadi mafuta ya gari yakaisha akaona haitoshi akashuka akakimbiaa hahaha
 
Mwaka 2002 TANGA
Tulikua tuna cheza mpira mtaani. Mpira ukapigwa nje ya uwanja kwa kuwa mm nilikua golikipa ili ilinibidi niufate huo mpira. Eneo tulilokuwa tunacheza lilikuwa na katani.. Kutokana na haraka haraka ya kutaka kurudisha mpira ili tuendelee na mtanange nililose umakini hvyo nikishitukia mwiba wa katani umeingia jichoni wakati nainama kuokota mpira. Nafikiri kwa watu walioishi Tanga na morogoro wanaelewa miiba ya katani ilivyo.. Nilipata maumiv ambayo sikuwah kuyapata na siwez ata kuyasimulia...Wenzangu walinipeleka Hospital na mechi ikaishia hapo hapo
 
mkuu sintosahau siku nilipo kuja dar kwa mara ya kwanza barabara ya mandela road nilipogogwa na gari nikapoteza mguu wangu mmoja daaah kwa kweli sintosahau .
Mkuu ulivyotoka mkoani kuja Dar hukuwa na mwejeji?
 
Mimi leo nipo hai ni Mungu tu amependa niwepo hai, nimenusurika katika ajali mara mbili ndani ya mwaka mmoja. Ajali ya kwanza ya pkpk ya pili gari yangu aina ya Noah mpka leo gari iko juu ya mawe but mimi natembea nikiwa mzima na viungo vyangu vyote, isipokua nina makovu mawili matatu. Hakika ninamrudishia Mungu shukurani za moyo wangu na ninampa sifa na utukufu kwa ajii ya uzima wangu. NARUDIA TENA NI MUNGU BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO AMEPENDA MIMI NIENDELEE KUWA HAI....I glorify you The Most High God in the name of Jesus Christ!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…