Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Pole sana ndugu!

Hadi umri huu sina historia ya ajali iwe ya gari binafsi ama magari ya abiria......

Sijajua ni kwasababu sisafiri sana, ama ni uoga wangu nikiwa barabarani ama ni kwakuwa nimejifunzia gari ukubwani...

Naogopa sana ajali.
Nikuombaa MUNGU tuu ajali inakufuata mahali popote pale wakati wowote. Unaweza tembea au kuendesha kwa tahadhar lakin akatokea mtu na yake akakuvaa. Hivii vitu havinaga mjanjaa
 
Mkuu acha tu umeni kumbushs mbali ilifika muda safari za kwenda chanika na kisarawe sitaki kusikia kabisa huko gar zina kimbia sana...nakumbuka mwaka 2015 mwezi wa sita nimetoka zangu chanika (geto) naenda safari msanga chole huko kisarawe mbelembele umapita kijiji cha masaki alipozikwa marehemu mzee ngurumo,safari yenyeww ilikuwa ya kushtukiza tu maana ex wangu alifanya kunipigia simu alaniambia niende huko msanga chole kwa kuwa çhanika na kisarawe jirano safari niliona rahisi basi nikafika kisarawe mwisho picha lina anza gar za kwenda huko zimechoka sana ni kama gari zilienda kupelek askar wetu vita ya kageta uganda ,ukikaa kwenye siti nauli buku nane ukisimama nauli buku tano kwa bahati mbaya nilikosa siti nikaishia kusimama safari ikaenda,asili ya kule ni kona na milima sasa gar ikawa ina changanya mwendo kwenye kona kona aseeee break zika feli na starling ika katika nimesimama nikaiona gari ina poteza mwendo siku paniki nikatulia ila malaika mtoa rohooo nilikuwa na mwona maana gari ina acha njia kwenda kuanguka ghafla gari ikapinduka sikumbuki nguvu nilipata wapi za kupita dirishani baada ya kutua mguu nilikuwa nimeumia watu wengi walifariki kwa ajir ya mshituko eneo tulipata ajar mzee wa pale asbh alikuwa na nauli pungufu konda na dereva waka mzuia kwenda aka wambia mtarud tu hapa hivyo tulivy pata ajar mzde akaja akasema nilikwambia mtarud tu maana tulikuwa tunatak jembe kufukua gari isimame tulikaaa masaa 5 kusubir gar jingine
eee7bbe68f124c9a4642479d031375e5.jpg

duhh km movie aic ,na bora usiruk ungeruka ungekuwa marehem aic,pole sn aic shukuru Mungu
Dah una mbwembwe sana kijana. Mimi nilipata ajali mpaka leo nina kumbukumbu ya chuma mkono wa kushoto.
View attachment 525278 View attachment 525279
Dah una mbwembwe sana kijana. Mimi nilipata ajali mpaka leo nina kumbukumbu ya chuma mkono wa kushoto.
View attachment 525278 View attachment 525279

yaan had nimesisimka aic duh mm hii ningekufa tu kuuangalia huo mshono uwii,,kweli umshuru MUngu dah
 
Poleni sana mliopatwa na masaibu ya ajali mungu atuepushe maana nasoma Uzi mpaka nasisimka ukizingatia sijawahi hata kuona ajali labda kwenye mitandao ,sio kwamba Mimi ni bora au sina dhambi nikwa Neema tuu

yeah sure
 
Ajar ya pili nimetoka gomzi nimepanda daladala za chanika watu tumejazwa wengi sana kukata kona ya pugu gari lika anza kuchanganya mfukoni nina efu

Ajar ya pili nimetoka gomzi nimepanda daladala za chanika watu tumejazwa wengi sana kukata kona ya pugu gari lika anza kuchanganya mfukoni nina efu 50 ya matumiz nimeshika kwa umakini sasa gari mwendo mkali ilikuwa dcm gobole gar lika anza kuacha njia upand wa mbelee jamaa nae gar ika acha njia zika kutana uso kwq uso zika bamizana pahaaaa...gar yetu ika anza kuyumba wamama wana paniki gar ikabiringita nimeshikilia kiti mkono mwingine umeshikilua pesa nilitoa hofu dk kadhaaa gar likapinduka watu baadh walifarik gar ika inuliwa ilikuwa usiku wakai washa starlng imepinda wakatak kupakia watu ikabd watu waingilie kat had police wakaja

hahhaah eti una 50/ hhahah pole aic mie kubiringita gari kwakweli naonaga kwenye muvi dah
 
Mwaka sikumbuki nilipata ajali ya Pikipiki dereva alifunga breki za ghafla na kupelekea Pikipiki kuluka juu na kutuangusha barabarani na kuingia uvunguni Wa pikapu ya upande mwingine ,dereva Wa pikapu alinichungulia kwa halaka chini na kukwepesha taili ya mbele kidogo kwahiyo taili ya nyuma ikasogea kidogo ndipo ikakanyaga nywele za lasta nilizokuwa nimesuka .Watu walipiga kelele za mshangao zile za watu Wa barabarani wanazopenda kupiga sababu ilikuwa shekilango kwenye magereji walifikili nimekanyangwa kichwa, mwenzangu alitupwa upande hulehule Wa barabara na yule dereva Wa pikapu baada ya kunyosha kama alipokuwa anakwenda yeye aliingia mtaani kwakasi alifikili ameua .Nashukulu nilitoka salama ata mchubuko huku nimeshikilia pochi yangu inapesa nyingi kwakweli baadae nilijicheka sana jinsi nilivyodondika huku nimekumbatia pochi yangu .
Watu walitusogeza pembeni sababu tulikuwa na kiwewe na kuchanganyikiwa mwenza wangu alivyoinuka yuko palepale chini anajizoazoa barabarani ananiuliza uko salama ujaumia? Mimi sikujibu nilikuwa na wenge balaaa mpaka hapo akili ivyokaa sawa baada ya kutolewa barabarani .wakatujalia watu na kuniambia wewe ukachinje kuku au utoe sadaka .kwakweli wakati wako kama bado uwezikufa mpaka wakati ufike sio kwa mapenzi yake Bali ajapanga nife siku ile ila nitakufa tu wakati ukifika ukuta.
 
. Waka 2002 TANGA tulikua tuna cheza mpira.Mpira ukapigwa nje kwa kuwa mm nilikua golikipa ili ilinibidi niufate mpira. Eneo tulilokuwa tunacheza lilikuwa na katani.. Kutokana na haraka haraka ya kutaka kurudisha mpira ili tuendelee na mtanange nililose umakini hvyo nikishitukia mwiba wa katani umeingia jichoni wakati nainama kuokota mpira. Nafikiri kwa watu walioishi Tanga na morogoro wanaelewa miiba ya katani ilivyo.. Nilipata maumiv ambayo sikuwah kuyapata na siwez ata kuyasimulia.

jicho lilipona?duh hatari kweli kweli
 
Mwaka sikumbuki nilipata ajali ya Pikipiki dereva alifunga breki za ghafla na kupelekea Pikipiki kuluka juu na kutuangusha barabarani na kuingia uvunguni Wa pikapu ya upande mwingine ,dereva Wa pikapu alinichungulia kwa halaka chini na kukwepesha taili ya mbele kidogo kwahiyo taili ya nyuma ikasogea kidogo ndipo ikakanyaga nywele za lasta nilizokuwa nimesuka .Watu walipiga kelele za mshangao zile za watu Wa barabarani wanazopenda kupiga sababu ilikuwa shekilango kwenye magereji walifikili nimekanyangwa kichwa, mwenzangu alitupwa upande hulehule Wa barabara na yule dereva Wa pikapu baada ya kunyosha kama alipokuwa anakwenda yeye aliingia mtaani kwakasi alifikili ameua .Nashukulu nilitoka salama ata mchubuko huku nimeshikilia pochi yangu inapesa nyingi kwakweli baadae nilijicheka sana jinsi nilivyodondika huku nimekumbatia pochi yangu .
Watu walitusogeza pembeni sababu tulikuwa na kiwewe na kuchanganyikiwa mwenza wangu alivyoinuka yuko palepale chini anajizoazoa barabarani ananiuliza uko salama ujaumia? Mimi sikujibu nilikuwa na wenge balaaa mpaka hapo akili ivyokaa sawa baada ya kutolewa barabarani .wakatujalia watu na kuniambia wewe ukachinje kuku au utoe sadaka .kwakweli wakati wako kama bado uwezikufa mpaka wakati ufike sio kwa mapenzi yake Bali ajapanga nife siku ile ila nitakufa tu wakati ukifika ukuta.

hahhaha lazima una uchaga ndan pichi hukuiaCHIA ?TEH TEH pole sn ,ndo nmaana mwaka umesahau lol
 
Rafiki yangu gari ilipindukia kajimfereji kama ka kakorongo gari ikawa haitizamiki yeye alitoka hakupata hata mchubuko anasema walioshuhudia wakamwambia siyo hali ya kawaida atakuwa amepata majeraha ya ndani kwa ndani Hosp. Akachekiwa alikuwa fit traffic wakamwambia asipookoka au kukaa karibu na Mungu basi atakuwa mwehu gar ilivyokuwa wakamwambia hakuna ajali ya aina ile MTU angepona !!!

hahahah na mara nyingi tunarudi kwa MUNGU wakat huo umenusurika ukipona unasahau,mby sana
 
2014 nilikuwa ndani ya bunda bus ile iliyogonga treni pale Manyoni. Nilishtuka watu wanapiga kelele kabla sijatafakari vizuri nikasikia kishindo na kujikuta nimerushiwa juu ya siti za upande wa pili. Namshukuru Mungu nilitoka salama ila aliyekuwa kakaa siti ya pembeni yangu alifariki [emoji22][emoji22][emoji22]
 
Uzi wa kijinga huu Sijapatapo kuona.

Ajali badala kumshukuru Mungu upo salama nyie mnatangaza hapa.

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliiondokewa na ndugu, jamaa, marafiki, watoto, wazee wao kwenye ajali?

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliolemaa maisha kwa ajali?

Huu uzi ufutwe, ni upumbavu wa hali ya juu kuuwacha hapa.
Mbona waliopata ulemevu nao wamesimulia humu.. Au leo umeamka vibaya?
 
Hamna hata aliyefariki humu?
Wote mlipona duh
Poleni sana kwa yaliyowakuta
Mimi ajali pekee niliyopata ni kujikwaa na kujikata kidole cha mguu mbaka leo kidole changu cha mguu kipo nusu
 
Back
Top Bottom