Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Mm nimeshauriwa nimrudie Mungu kiukamilifu....ajari nimepata nyingi sana tangu mwaka juzi...ila cha ajabu mm nimesalimika zote. Dom ajari mbili, Arusha 1, Mara ajali 1, Moro ajali 1, Singida ajari 1. Kila siku nashauriwa nikae kwa Mungu na nipunguze kusafiri
 
Mimi naisikiaga ajali tu kwenye TV!!!
Sijawai pata ajali serious ya kumkwaruza mtu...
Nashukuru Mungu.
Poleni kwa waliopata ajali, ila namshukuru Mungu kwa kuwaponya na kuwapa nafasi ya kushuhudia leo!
 
Nakumbuka miaka ya 2005 natokea babati naenda tarangire nilikuwa nimelewa sana nasukuma PUMA TD6 mvua ya hatar kuna vikona havieleweki hapo kati wanapaita kona S hahahah nikakutana na nusu mkate ka RAJU wahind flan waliokuwa na magari ya usafir babati, Jamaa akanibana kaganda katikati ya bara bara mbuuuuuula nakujakustuka naona naserereka pombe ikakata kwa muda mungu bariki tuligonga ngema ila Raju bofla kalianguka kabisa,
Ila sikomi napiga pombe na kuendesha ila tokea ile ajali nimekuwa makini sana nikilewa hata vipi wewe niweke tu kwenye staring nafika kabisa sema kushuka ndio kitendawili sasa
Fikiria maisha ya wengine mkuu!
Kuendesha ukiwa umelewa ni hatari sana
 
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa saba natoka dar na CITY BOY tulipokaribia manyoni basi likagongana uso kwa uso na CITY BOY ya kutoka mwanza zaidi ya watu 30 walipoteza maisha nashudia Mungu saidia skuumia hata kidogo.sitaisahau sku hyo maishani
Muongo
 
Ajali Zote Huwa Natoka Mzima Niliingia Mtaroni Na Ist Nikawakosa Kosa Wauza Matunda Wanaopanga Pembeni Mwa Barabara Ya Pili Suzuki Carry Ilifeli Brake Nimkosa Bibi Wa Watu Nikaparamia Mawe Ya Tatu Pikipiki Ilinishinda Kuiongoza Nikawakosa Wanywa Kahawa Nikaparamia Mitungi Ya Ges Dukani Kwa Mangi Ya Tatu Toyota Carina Nataka Kuondoka Kwenye Makutano Watoto Wamejibeba Kwenye Bike Wakajaa Mlangoni Ila Hawakuumia Hata Kidogo Nilishawahi Kuzama Na Mtumbwi Ila Wote Tulitoka Salama Mungu Mkubwa
 
Poleee mzeee. Lakini darajaa linahama ulikuwa ushafanya uchenjuaji wangano au ulipigwa mambo ya ozanga na nefunefuu!!!! Yani daraja linahama kabisaa???

Hahahahaaa., nimecheka sana hiyo sentensi.
 
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa saba natoka dar na CITY BOY tulipokaribia manyoni basi likagongana uso kwa uso na CITY BOY ya kutoka mwanza zaidi ya watu 30 walipoteza maisha nashudia Mungu saidia skuumia hata kidogo.sitaisahau sku hyo maishani

Duh, pole sana na ninaamini ulifanya ibada ya shukrani. Ajali ile ilikuwa kati ya ajali mbaya sana kupata kutokea.
 
nimepata ajali nyingi ikiwemo za pikipiki na sababu kubwa ni ulevi!ila ajali iliyonitia akili ni mwaka huu siku ya juma3 ya pasaka niko na mshkaji wangu tumelewa ile chapachapa baada ya kuendeleza gambe toka pasaka!tuko na haria kufika sehemu flani ilikuwa mida ya saa 8 mchana jamaa alikosa kumgonga mtu wa bodaboda mi sikuwa na habari ya chochote wakati huo nimelala kwenye siti wale bodaboda wakaanza kufkuza gari huku wamebeba mawe ili wavunje vioo jamaa wangu akapata wenge na zile akaweka mafuta ya kutosha ilikuwa spidi 130 hivi kwa mbele kuna gari inaingia upande wa kulia yaani basi tukaigonga ile gari kishindo ndo kikanishtua usingizini nikaona gari imepaa mara miti inazunguka huku kurudi naona mawingu juu angani na sikuwa nimefunga belt.nikawa naskia kelele watu wanasema itakuwa wamekufa hawa,nilivyoskia hvyo nikasema embu niinuke nijue km nimekufa nikajiona mzima nikamvuta mshkaji miguu hadi nje akaamka tukaondoka eneo la tukio tukaenda baa ya jirani tukaendelea kunywa hadi askari walivyotufata tukalala nondo.ila mungu mkubwa hatukupata hata skrechi na gari ilipinduka zaid ya x7 gari hakuna fundi amesema itafaa tena hata irudishwe japan ni skrepa tu
Kusemaa vyaukwelii pombee na garii tenaa spid safari ndefuu haifaii. Niwatuu wanajikutagaa manunda et nikilewa nakuwa makini [emoji23][emoji23][emoji23]unakuwa makini kablaa haijachanganyaa lakini ikikufikaa hapaa ujue umeishaa.

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom