Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Tuliowahi kupata ajali na kunusurika tukutane hapa

Me wakati naanza kujifunza gari mwaka 2003,nilikurupua gari yangu baada yakumaliza kuoshwa ilikuwa ISUZU JOURNEY MINIBUS, ,,,BASI BREAK ya kwanza nilimgonga mtu then nikaenda kuvaa Fensi ya mtu,,,,gari ilichakaa na jamaa alivunjika mkono na mimi mwenyewe nilizimia kwenye stering nikaenda kuzindukia lockup sina leseni wala chochote ,,, sitoisahau Ile ajali, ,,,,,,,,
 
Me wakati naanza kujifunza gari mwaka 2003,nilikurupua gari yangu baada yakumaliza kuoshwa ilikuwa ISUZU JOURNEY MINIBUS, ,,,BASI BREAK ya kwanza nilimgonga mtu then nikaenda kuvaa Fensi ya mtu,,,,gari ilichakaa na jamaa alivunjika mkono na mimi mwenyewe nilizimia kwenye stering nikaenda kuzindukia lockup sina leseni wala chochote ,,, sitoisahau Ile ajali, ,,,,,,,,


nimejikuta nacheka jaman hahahaha pole!hahah had kuzima nimecheka sana
 
Nakumbuka miaka ya 2005 natokea babati naenda tarangire nilikuwa nimelewa sana nasukuma PUMA TD6 mvua ya hatar kuna vikona havieleweki hapo kati wanapaita kona S hahahah nikakutana na nusu mkate ka RAJU wahind flan waliokuwa na magari ya usafir babati, Jamaa akanibana kaganda katikati ya bara bara mbuuuuuula nakujakustuka naona naserereka pombe ikakata kwa muda mungu bariki tuligonga ngema ila Raju bofla kalianguka kabisa,
Ila sikomi napiga pombe na kuendesha ila tokea ile ajali nimekuwa makini sana nikilewa hata vipi wewe niweke tu kwenye staring nafika kabisa sema kushuka ndio kitendawili sasa
Mbuuuulaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikua na BM ya Morogoro Arusha December 2014.Basi aina Ya Yutong lilitaka kuovatake magari madogo na bahati mbaya kukawa na nyingine unakuja ikabidi arudi.Kurudi kwenye line yake na kona ghafla na imebaki gari ya gasi.ikabidi aliingize porini.Liliturusha na kuyumba sana ila likatulia.ilikua hatare
 
Nilikua na BM ya Morogoro Arusha December 2014.Basi aina Ya Yutong lilitaka kuovatake magari madogo na bahati mbaya kukawa na nyingine unakuja ikabidi arudi.Kurudi kwenye line yake na kona ghafla na imebaki gari ya gasi.ikabidi aliingize porini.Liliturusha na kuyumba sana ila likatulia.ilikua hatare
Alafu BUMIJA
 
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa saba natoka dar na CITY BOY tulipokaribia manyoni basi likagongana uso kwa uso na CITY BOY ya kutoka mwanza zaidi ya watu 30 walipoteza maisha nashudia Mungu saidia skuumia hata kidogo.sitaisahau sku hyo maishani
Hii ajali ilikuwa mbaya sana sana...
Pole sana na muweke muumba karibu yako.
 
Ilikuwa mwaka 1997 tunasafirisha maiti toka Dar kwenda Iramba mkoani Singida tulifika salama Dada akaniambia tushukuru tumefika salama pale pale nikawa mnyonge sana nikajikuta namwambia ila wakati wa kurudi tutaanguka na gari sijui kwa nini nilisema hivyo Dada akanikataza nisiseme hivyo Mimi nikamjibu kweli Dada. Tukazika na kuanza safari ya kurudi ile tunaanza safari nikamwambia Dada laaaah tunakwenda kuanguka masikini sijui tufanye nini? Dada akaniambia usimsemee hivyo nikamwambia kweli. Kutoka Singida tukafika pale ambapo ukinyoosha unakwenda Arusha ukikata kulia unapitia Dodoma mkuu wa msafara akamwambia driver nyoosha tupite ya usandawe ilikuwa ni jioni Mimi nilikuwa kiti cha pili nyuma ya driver nikamwambia driver kwa sauti kata kulia pita ya Dodoma, driver akauliuliza nimsikilize nani? Nikamwambia Mimi, mkuu wa msafara akasema nyoosha halafu akaniuliza kwanini umesema hivyo ile sauti ya kufoka nikamjibu Barabara zote mbili tutaanguka hii ya Dodoma tutapata msaada hii ya usandawe nani atatusaidia? Kanijibu hoja dhaifu driver nyoosha, nikamwambia Dada naogopa ajali Mimi nalala nisione tunavyoanguka, Dada akasema usiseme hivyo mdogo wangu nikamwambia kweli dada, nikalala muda mrefu baadae nikastuka nikamuuliza Dada hatujaanguka? Akaniambia wewe, nikamuomba nikae upande wa dirishani aliponipisha nikamwambia nalala Mungu atunusuru jamani, nikalala kama saa tatu usiku hivi nikastuka usingizini gari inayumba vibaya sana mara tukaanguka ni kiza kinene, mvua inanyesha na tupo porini peke yetu watu wakatokea madirishani maana mlango upo kwa chini Mimi nikawa nimebanwa kidogo na kiti cha mbele yangu halafu na ule usingizi nikaamua nilale tu, kule nje wakagundua sipo ikabidi waanze kuniita kuchungulia Giza nikawaambia sitoki wakanibembeleza nikatoka nina hasira ile mbaya siongei na mtu. Mkuu wa msafara akamfuata driver anataka kumpiga Mimi nikamwambia nilikwambia tukiwa Singida ukanidharau hakuna msaada hapa nyanyueni gari tuondoke, ikabidi wafanye hivyo huku wanalalamika maumivu Bahati nzuri iliwaka tukaondoka kweli Mungu ni Mkubwa yaani ukiona hiyo gari huwezi Kuamini kama itatembea na haikuua Ila majeruhi, kufika Dodoma tukabadilishiwa usafiri. baada ya muda nikawa na maumivu ya mgongo, hizi zingine ambazo ni mbaya zaidi kwangu nazihifadhi Ila Mungu ni Mkubwa kisichokuwa kikupate hakikupati
Mh..[emoji102] [emoji102]
 
nilicheka sana siku moja deiwaka kapewa akalaze hiace mida ya saa 4 usiku.
kapiga kona kubwa kuingia kushoto kumbe bodaboda inakuja ikagonga upande wa kushoto pembeni dereva ile helmeti ikachomoka ikaingia ndani ya hiace kwa wenge dereva akajua kichwa cha bodaboda kimekatika na ile helmeti ilikuwa nyekundu afu usiku jamaa akapata mawenge kila akiangalia pembeni yake anajua kichwa anazidi kukanyaga mafuta hadi mafuta ya gari yakaisha akaona haitoshi akashuka akakimbiaa hahaha
Mkuu tuache kidogo. .[emoji23] [emoji23]
 
Mpaka leo huwa naikumbuka Jumamosi ile niliopata ajali.Kiufupi nilipanda pikipiki bahati mbaya hakuwa ameiwasha na tuko kwenye mteremko mkali,dereva nikamuuliza nini hiyo maana nilisikia ilivyokata break hakunijibu. Pikipiki ilikuwa kwenye mwendo balaa,baada ya dk kama 2 dereva akaanza kupiga kelele sister tunakufaaa pale ndio aliponitisha zaidi pikipiki ilikosa direction ikawa ninachira zigzag,barabara ni very rough imechimba kabisa mifereji ktktk kwasababu ya mvua za mwaka huu(nadhani haikuwa dalili njema kwa wizara ya madini (makinikia).

Niliangalia
mwisho wa barabara kuna miti minene imepanda kimkingamo,ilikuwa tuivae bila ubishi nikaamua kuruka nijiokoe tu,hasa nilipowakumbuka wanangu bado wadogo nikachukua maamuzi ya kuruka,the rest nilijikuta hospitali mwili wote una damu hasa usoni.

Imagine nikaja kushonwa saa7 usiki toka 8:33 nilipoanguka.Daktari aliniambia yaani wewe kuruka ndo imekuwa pona yako ile miti ulikuwa unaenda kuivaa., mawili mimi wa nyuma kuangukia mgongo na kuvunjika mgongo au kufariki maana miti ilikuwa imebabana asingeweza ikwepa.

Nashukuru sikuvunjika na ruka yangu ndo ikawa pona yangu,na nikamsaidia dreva nae aanguke mbele yangu,nae aliumia ila sio sana.

Je, wewe uliewahi kupata ajali huwa unaiongeleaje?

Poleni wote mliowahi kuajalika na kupata ulemavu na kupoteza ndugu, mimi niliponea chupuchupu ila ningeganda kusubiri miujiza walah hata ishu ya MAKINIKIA nisingeijua wala madini ya TL nisingeyasikia.

My take madereva kuweni makini
Thanks GOD
Duh pole sana mke wangu kipenz, sijui leo hii ningekuwa nafurah na nan kama ungetangulia mbele za hak
 
Duh pole sana mke wangu kipenz, sijui leo hii ningekuwa nafurah na nan kama ungetangulia mbele za hak


hahaha mpk leo huwa siamin km nilipona ! yaan nahis nna mwili mzuri tu kwa jinsi nilivyookuwa na leo hii !asalaale! asante sana mume wangu kipenz
 
26/12/2014 jion samojaa kasoro moshi 2arusha tumetoka kulaa skukuu tupo na korola familia ya wanaume 4 na mwanamke mmoja mchepu wa mmoja wetu. Me nmekamatia steling wengine wamekamatia kata za kitu pendwa cha moshi, tumekaribia kia sasa magari simengi mchepu wenyewe umetoroka kwao. Imagine unapigiwa cm kwao unasema upo round about ya kijenge afu kwao ninjiro na sisi ndo hataa KIA hatujafikaa. Ile jam jam yamagari ikatokea jamaa aliyeko mbele yangu anaprimio new model akatanua kihere changu name nikafuata shughuli ikaanzia hapoo. Nkakanyagaa zutu weee nkicheki kushoto magari mengi yako spid sioni hata gap lakujichomeka nikajipa moyo tuu. Bahati Nzuri walevi wangu nao wakakaa kimya tuu yule waprimio akajitahid akamaliza msururu kama gari nane hivii kama sikosei akarud kushoto. Nikabaki mimi pakuchomeka cpaoni gari pulling hainaa nkasema hapaa nimekwisha. Nikakazaa nikabakiza fuso sasa ndo lamwisho honiii nyingi hataa nihurumiwe nipate kagap wap ghaflaa kuna escudo inakujaa mbelee nikasemaa tumeishaa sasaa jamaa anaekuja namuwashia taa japo atanue kidogo nipenye ndo kwanza kaweka gari yake katikat ya chaki na taaa kawasha fulu. Kucheki kushoto niko usawa wa tairi lambele la fuso nikawaza nikibana kushoto tumeisha nikasema ngoja nimkazie anaekujaa atapisha chaaaaa!!!!! Jamaaa kakomaaa kitendo chakufumba macho nakufumbua huyu hapaa sikuweza kuangalia fuso tenaa ila nadhan alituhurumia akapunguza mwendo. Jamaa wa escudo nikapindisha usukan kichele tuu alivyopita na huo ubavu nakwakuwa nilikata kushoto gari ikavuta upande kuirudisha kuliaa tairi ya nyuma kushoto ikaliaa gari ikatoka nje ya bara baraa nikajaribu kushika brake ikanyanyuka upande nikaachia,nikagusa zutu kidogo ile fuso ikasimama na msururu wote nao ukapaki wanatizama kitakachojiri waje kuokota mizoga ya binadamu. Namshukuru MUNGU mpaka Leo kwa anaepajua lile eneo la kia kwa nyuma kuko tambarare kiasi na hakuna miti wala ngema yoyote nikacheza nayo nikairudisha lami nikasimama pembeni ya bara baraa. Ile mawenge tukashuka wote tunalikimbia gari tumeloa mbegee vumbi lakutoshaa. Watu wanashangaa tumeponaje yule wa escudo hatukumuona tena. Tukabadil tairi tukaendelea tukapita KIA salama hapoo me nimegoma kuendesha akachukua mwenzangu nae alikuwa yuko mafuta kidogo kichwani. Ndo tunaanza panda kamlima cha pale katiti gari ikapoteza nguvu mwisho ikazima. Tukahangaika bila kujua kumbe kwenye purukushani ya mwazo kulitoboka uko chin oil ikaisha na gari ilikuwa ingine imechemka na maji yaliisha mawenge yetu tukajua rejeta ndo imezingua tukaijaza mbegee piga start kitu ikanock ingine kilichofuata kuomba msaada kutoka town wakuvutwa. ishaingia sanne kasoro ucku Magar hayasimami ovyo kuofia wakora. Wakaja washkaji na rvr kutuvuta shughuli ingine ikaanzia hapo kwanza wamelewa wanatuvuta sisi wanakimbiaa balaa na wana over take ni ucku gari yetu inategemea hand brake ndo isimame yan pombe zilikata zote. Kufika usa kidogo tuvae daraja kuchezesha gari yetu inayovutwa tari ya nyuma kushoto ikajibamiza kwenye kingo za daraja na kamba ikakatikaa wanao tuvuta hawajua wanatembea tuu. Tukawapigia cm wakapiga cha nyoro kutufuata kumbe ile tairi ilojibamiza rim ikapinda ikawa inatoa upepo kichele bwanaa wee walev wanaotuvuta wakasema tufunge kamba shala shalaa tuwahi tufike mjini kablaa haijaisha upepo mziki ukaanzaa tenaa satano unusu tunaingiza gari gerij sakina tumechoka. Sitokaa nisahu nilikaa mwezi siwez kuendesha gari na mpaka Leo niko na heshima na gari bora niendeshwe
ahaaaaaa umenichekesha usiku huu
 
we
Uzi wa kijinga huu Sijapatapo kuona.

Ajali badala kumshukuru Mungu upo salama nyie mnatangaza hapa.

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliiondokewa na ndugu, jamaa, marafiki, watoto, wazee wao kwenye ajali?

Mnapeleka ujumbe upi kwa wale waliolemaa maisha kwa ajali?

Huu uzi ufutwe, ni upumbavu wa hali ya juu kuuwacha hapa.
we bibi acha nongwa hii jf sio ile ya enzi zenu
 
Back
Top Bottom