Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Wanakosa story na we mtaongea nn ss
Tajirimsomi kuhusu wahindi nna ushahidi wa dadaangu baba mmoja mama mmoja!...

Aliwapiga wahindi kama 60m hivi, akanunua Benz, kiwanja, na furniture ndani, alichokosea na yeye mara uzalendo umemshinda akaanza kwenda na Benz lake job!

Wee navyoongea now wamemchunguza ila yy hajapelekwa mahakamani, tunachokiona sisi ni kwamba kalogwa, benz kushnei now ( alipata nalo ajali Moro) kiwanja kauza, alitaka kufanya biashara ya mbao sijui anashirikiana wa jamaa gani na alichangia 15m, huyo jamaa yake kapata ajali na vibaka wamemwibia hizo pesa!

Yaani na ana mikosi hataree!
 
Pesa ya muhindi chungu
 
Hahahaaaaa "danga", "kudanga"
 
Niliwahi kupata milioni 120 nikiwa na umri wa miaka 26 kipindi hicho nipo mererani, nilichezea hiyo hela kwa muda wa miezi 8 nikabaki na laki mbili bank
Dah....ulichezeaje chief? Huna hata cha kujivunia? ...Mimi nilijaza vitabu viwili vya passport....nikaonja ladha ya aina tofauti tofauti za rangi[emoji87]
 
Dah....utaishi miaka 100 bana? Utakitia ujinga kizazi chako[emoji87]
 
Dah... Ningekuwa mzazi wako...ningeanza kukupa bills za meal na accommodation.......utie akili [emoji41] [emoji13]
 

Upo sahihi mkuu
 
Tunakumbushana tu,

Sifa ya shida haiji peke yake yani ukiona imebisha hodi ya kwanza subiri nyingne kama kum hv mlangoni, na ndio maana mtu hasemi nina tatzo anasema nina matatizo asa ukikuta mtu ambaye akipata matatizo anauza assets huyo atakuambia nina matatizo na nusu.

Hakikisha huyu mtu hakai peke yake, wala haend dukan kununua kamba au sumu ya panya, kama una mizunguko mingi huwez kumlinda, hakikisha umeshachimba kaburi na jeneza lipo ndani na sanda yake mana lazma abipu na izrael ataenda hewan mana sikuzote hakosi bando.
 
Dooooh wewe ni mwanaume haswaa, mpambanaji wa aina yake, wengi hapa wangekua wameshakufa muda sanaaa.
 
Daaaaah hii inatosha mkuu, hope jamaa sasa iv atakua kichaa, bora ata wenzake waliuza nyumba na kukimbia yeye hakuuza na bado imebomoka.
 
Mkuu pole sanaa sanaaa, jifunze kwa wadau hapa waliorudi tena kwenye peak, kwa kusahau yote na kuanza upya, japo unatakiwa ujue itachukua muda sanaa.
 
Daaaaah hii inatosha mkuu, hope jamaa sasa iv atakua kichaa, bora ata wenzake waliuza nyumba na kukimbia yeye hakuuza na bado imebomoka.
We acha tuu jamaa alishagachanganyikiwa hata kabla ya tetemeko
 
Yeah sure mkuu
 
Asante kwa ushauri mkuu..
Mungu akubaliki sana..
Maneno mazito sana haya..
 
Mimi nimepoteza Mil. 6.6 kwenye kilimo ndani ya miezi minne mwaka huu huu (July hadi Nov)

MATIKITI: Nililima Ruvu Mnazi kilimo cha kumwagilia kiligharimu Mil. 1.6 matunda yanakibia kuvunwa ng'ombe wa wamang'ati wakapita wacha walikanyaga hatariii sikuambulia kitu.

MAHINDI YA KUCHOMA: Nililima Ruvu Mnazi heka 5 kwa kumwagilia, nilitumia almost Mil. 2.3 hv mvua za juzi kati hapa walizotabiri TMA zikaharibu kila kitu kabla sijavuna.

BAMIA na MAHINDI tena: Nikaja nikapata eneo tena Bagamoyo nikajipinda na Bamia heka 5 kwa kumwagilia tena kabla sijamaliza kumwagilia ili nipande mvua zikaanza, kila nikipanda mvua inapiga, kila nikimaliza mvua inapiga mbegu zikaoza nikaachana nalo sahv nasikilizia nilime mpunga sijui yatatokea yapi. Hapa nilitumia kama Mil. 2.7


Ila nitarudi tena sijakata tamaa, naamini ipo siku nitatusua kupitia kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…