Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Wanakosa story na we mtaongea nn ss
Tajirimsomi kuhusu wahindi nna ushahidi wa dadaangu baba mmoja mama mmoja!...

Aliwapiga wahindi kama 60m hivi, akanunua Benz, kiwanja, na furniture ndani, alichokosea na yeye mara uzalendo umemshinda akaanza kwenda na Benz lake job!

Wee navyoongea now wamemchunguza ila yy hajapelekwa mahakamani, tunachokiona sisi ni kwamba kalogwa, benz kushnei now ( alipata nalo ajali Moro) kiwanja kauza, alitaka kufanya biashara ya mbao sijui anashirikiana wa jamaa gani na alichangia 15m, huyo jamaa yake kapata ajali na vibaka wamemwibia hizo pesa!

Yaani na ana mikosi hataree!
 
Pesa ya muhindi chungu
 
Nilipewaga dola 100 zamani sana na danga limoja hivi aiseee kwa kipindi kile ilikua ela nzuri nikaja nikaila bila kuelewa imepita wap
Nikaja kupewa tena mil1 na hilo hilo danga zamani kidogo nayo haikufanya la maana
Nikaja nikapata danga lingine likanipa m2 nazo nimefanyia kazi haikuzaaa
Tangu wakati huo miaka imepita sitaki tena ela za madanga,nimeolewa na nina tafuta hela kialali
Msiwashangae kina wema hela za kudanga hata upewe bil 1 huwa zinayeyuka
Hahahaaaaa "danga", "kudanga"
 
Niliwahi kupata milioni 120 nikiwa na umri wa miaka 26 kipindi hicho nipo mererani, nilichezea hiyo hela kwa muda wa miezi 8 nikabaki na laki mbili bank
Dah....ulichezeaje chief? Huna hata cha kujivunia? ...Mimi nilijaza vitabu viwili vya passport....nikaonja ladha ya aina tofauti tofauti za rangi[emoji87]
 
Wengi wa watu walipitia mafanikio makubwa sana na tunajuta...Anasa na starehe nzuri ni zile unakula na familia ukubwani maana hapo ndipo umuhimu wa pesa na uhitaji wa pesa unapoonekana...vijana hakikisheni mnaweka pesa zenu kwenye Asset na sio Liabilities....nunua viwanja kadri uwezavyo...wekeza kwenye mashamba hata kama ulimi sasa hivi... kula bata kwa akili sio kwa sifa ili watu wakuone...wanaokusifia sasa ukifilisika haohao wanakucheka na kukudharau.
Dah....utaishi miaka 100 bana? Utakitia ujinga kizazi chako[emoji87]
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Dah... Ningekuwa mzazi wako...ningeanza kukupa bills za meal na accommodation.......utie akili [emoji41] [emoji13]
 
Kati ya watu usiotakiwa waamini na kuwasaidia, ni watu wanaokuwa karibu na wewe ukiwa na hela....
Siku zikiisha watakusema na kukuona haufai.....
Sidhani nitakuja saidia mtu maana wengi wao wanakugeuka na kukusema vibaya mambo yakienda ndivyo sivyo....
Bora hiyo hela ukaipeleke kanisani kuliko kumpa ndugu mnafiki pale ukifuli

Hao unaocheka nao na kula nao raha ndio watakucheka baadae....

Upo sahihi mkuu
 
Tunakumbushana tu,

Sifa ya shida haiji peke yake yani ukiona imebisha hodi ya kwanza subiri nyingne kama kum hv mlangoni, na ndio maana mtu hasemi nina tatzo anasema nina matatizo asa ukikuta mtu ambaye akipata matatizo anauza assets huyo atakuambia nina matatizo na nusu.

Hakikisha huyu mtu hakai peke yake, wala haend dukan kununua kamba au sumu ya panya, kama una mizunguko mingi huwez kumlinda, hakikisha umeshachimba kaburi na jeneza lipo ndani na sanda yake mana lazma abipu na izrael ataenda hewan mana sikuzote hakosi bando.
 
Dooooh wewe ni mwanaume haswaa, mpambanaji wa aina yake, wengi hapa wangekua wameshakufa muda sanaaa.
 
Daaaaah hii inatosha mkuu, hope jamaa sasa iv atakua kichaa, bora ata wenzake waliuza nyumba na kukimbia yeye hakuuza na bado imebomoka.
 
Miaka 3 iliyopita nililima eka 40 za mpunga na 30 za mahindi nilipokuja kuuza mazao niliingiza faida ya mil 55 ukitoa na pesa ya mtaji.
Leo tar 1 nina laki moja tu..wanawake sio viumbe vya mchezo na kazi nimefukuzwa..niliowasaidia wamenitupa.
Nimejifunza mistake zote nilizofanya ila nikikumbuka naumia mno..kwa vile nina nguvu sina ulemavu naendelea kupambana.
Nimerudi home kwa wazazi maana hali ni tete ninaweza kuwa tahaira
Mkuu pole sanaa sanaaa, jifunze kwa wadau hapa waliorudi tena kwenye peak, kwa kusahau yote na kuanza upya, japo unatakiwa ujue itachukua muda sanaa.
 
Daaaaah hii inatosha mkuu, hope jamaa sasa iv atakua kichaa, bora ata wenzake waliuza nyumba na kukimbia yeye hakuuza na bado imebomoka.
We acha tuu jamaa alishagachanganyikiwa hata kabla ya tetemeko
 
bt I agree huwez kupata heshima na pesa kama hujawahi firisika one of my broo aliachiwa kila facilities baada ya mzee kupoteza akiwa na miaka 18 alikuwa mdosi pesa ikaisha lakin ilipoisha alisimama tena na hadi saiz ni tegemeo la familia na biashara anazi run ipasavyo mm binafsi ninaogopa sana pesa ambayo consumption yake niya short run
Yeah sure mkuu
 
Pole sana kaka,huwa tunajifunza tunapoanguka japo kwa maumivu makali sana,hela yako yoyote iweke sehemu ambayo ukiitaka lazima ikupe ugumu wa kuichukua ila ukiiweka sijui bank huku ukitembea na ATM Card mfukoni jua hiyo siyo yako,pia usimkopeshe mtu hata kama ndugu pesa yako iweke kwenye assets japo ukiwa na shida maisha utayaona magumu lakini at least utajifariji kwamba unacho kitu umekiweka mahali.maisha yanatisha sana aisee vijana ambao hamjapitia magumu mengi ktk maisha yenu mnaopita ktk uzi huu someni between the lines kinachoandikwa humu maana sio masihara cos kama bro hapa alipoteza 4mill 2yrs nyuma akala msoto huo akitokea mmoja wetu akaipoteza kama hiyo Tanzania ya leo hakuna namna itamfanya asifungwe kamba au asipelekwe Mirembe.shida zisikie kwa mwenzako na hazizoeleki tuwe serious na maisha.
Asante kwa ushauri mkuu..
Mungu akubaliki sana..
Maneno mazito sana haya..
 
Mimi nimepoteza Mil. 6.6 kwenye kilimo ndani ya miezi minne mwaka huu huu (July hadi Nov)

MATIKITI: Nililima Ruvu Mnazi kilimo cha kumwagilia kiligharimu Mil. 1.6 matunda yanakibia kuvunwa ng'ombe wa wamang'ati wakapita wacha walikanyaga hatariii sikuambulia kitu.

MAHINDI YA KUCHOMA: Nililima Ruvu Mnazi heka 5 kwa kumwagilia, nilitumia almost Mil. 2.3 hv mvua za juzi kati hapa walizotabiri TMA zikaharibu kila kitu kabla sijavuna.

BAMIA na MAHINDI tena: Nikaja nikapata eneo tena Bagamoyo nikajipinda na Bamia heka 5 kwa kumwagilia tena kabla sijamaliza kumwagilia ili nipande mvua zikaanza, kila nikipanda mvua inapiga, kila nikimaliza mvua inapiga mbegu zikaoza nikaachana nalo sahv nasikilizia nilime mpunga sijui yatatokea yapi. Hapa nilitumia kama Mil. 2.7

Ila nitarudi tena sijakata tamaa, naamini ipo siku nitatusua kupitia kilimo.
 
Back
Top Bottom