Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Dooooh mkuu una moyo, mim ningechukua hao ng'ombe wa mang'ati... Mkuu labda kilimo kimekukataa acha tu
 
Tafuta kitabu kinachoitwa ''The anatomy of failure'' cha Praise George. Utajifunza mengi sana mle. Soma piakingine cha The Law of Success by Napoleon.
Utagundua why people fail.
Ahsante Mkuu, Ila unapowasoma wahusika na matukio mbalimbali yaliyowatokea ni exprience nzuri kuliko mawazo ya mtu mmoja yaliyowekwa kwenye kitabu,Mwandishi anaweza asipate exprience tofauti tofauti kama Live exprience toka kwa wahusika, Hii inavutia sana na wasio na uwezo wa kununua vitabu wanajifunza kwa gharama nafuu na uhalisia sana, wengi wamekuwa sio wachoyo kwenye kufunguka.
 
Hakika wewe ni mpambanaji, Nimeikubali spirit uliyonayo katika kupambana, unaweza kufanya chochote kikafanikiwa kwa kuwa hali yako ni juu sana, HONGERA.
 
Pole, hilo ni funzo kubwa sana naamini sasa hivi utakuwa ni mwalimu mzuri kwa wenzako
 
Siku za hivi karibuni nilipata pesa nyingi sanaaaa....ila nilichojifunza ni kuwa na discipline ya matumizi. Matumizi yasizidi kipato. Bora ushinde njaa siku moja ila usile pesa ya mtaji.
Hahahahahahah nimejifunza nidhamu hii baada ya kupoteza mtaji wangu wote wa mchele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…