Nina mjomba wangu mmoja hivi alikuwa anaimba imba kwenye hizi bendi za muziki kipindi hicho. Unawataja ma papaa, watu wazito alaf wanakutunza pesa ndefu. Sasa sijui alipigaje hela, ila alikuja kumiliki pesa ndefu. Mjini akawa yeye ndio Don, kila kona ana demu. Muda wote kachomekea, starehe mwanzo mwisho. Baada ya miezi kadhaa akafulia mbaya, hadi soo.
Akapotelea migodini. Huko alikaa kama miaka miwili au mitatu. Akapiga mshindo wa maana. Kurudi town ana hela chafu. Akiingia bar anatoa watu wote, anaikodi bar alaf anabaki na wapambe wake tu. Kuna siku mlevi mmoja wakati anatolewa nje kwavile bar imekodiwa na anko, yule mlevi alitukana. Anko akaomba aitiwe huyo aliyetukana. Kabla hata hajamwangalia usoni, akamuagiza mhudumu ampe yule mlevi kreti za bia sawa na urefu wake. Siku nyingine anaweza akatoa order kuwa wahudumu wote wa bar wabaki na pichu tu na sidiria. Haikupita miaka miwili akafulia mbaya.
Alivyofulia akapotea bila kujua kaenda wapi. Akaja kuibuka baada ya miaka kadhaa. Siku anakuja home kanawiri kichizi, akampa bi mkubwa (mama angu mimi) busness kadi yake ambayo inaonesha yeye ni engeneer na anamiliki kampuni ya ujenzi wa barabara (anko aliishia la saba) [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa hivi ameshaoa na ana life zuri tu. Ukimpigia simu story zake ni either yupo njiani anaenda makao makuu Dodoma au yupo njiani anatoka kule. Ukimpigia simu asipopokea, badae akikuchek utaskia alikuwa kwenye kikao na Mama ndio maana hakupokea (hapo anamaanisha mama Salma Kikwete)
Mara ya mwisho kumpigia simu aliniambia "Ngoja naingia Usalama, ntakuchek badae, siunajua ofisi za watu hizi" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mungu akupe maisha marefu anko.