Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Anzisha kampuni(LLC).
Hiki ni kitu unachotakiwa kuwa nacho kama wewe ni mtu wa biashara.
Always uwe ume-register kampuni BRELA.
Mkuu toa darasa kidogo nini umuhimu wa kuendesha biashara kama kampuni, je mtaji unapaswa kuwa kiasi gani ili kufungua biashara, mtu ana salon anaweza kuiendesha kama kampuni?
 
Ulifika fedha kiasi gani ukapoteza, hiyo itanipa msingi wa ushauri.

Unanikumbusha ipo siku nauguliwa na mtu kisha nampigia simu mtu ninaemuamini nikope laki 2 nimtibu mgonjwa ananijibu hana kitu ilihalu nilikuwa na uhakika anayo, nilikaa sehemu nililia sana, nikajisemea hela nilizokuwa nazo mimi wa kukopa mtu leo laki mbili nimtibie mtu ninyimwe.

Anyway yule mgonjwa akafa.
Pole mkuu
Hebu elezea ilikuwaje ukafilisika?
 
Weka pesa bank na utumie kwa malengo maalum, sio tu kutumia.. Hapo kwenye kuweka pesa bank zile pesa ambazo una malengo nazo za muda mrefu unatakiwa kuziweka kwenye acc ya fixed.. Account ya fixed itakulimit kuchukua pesa ktk kipindi Fulani. Unaweza kukubaliana na. Kuingia mkataba na bank uchukue pesa zako baada ya miaka 3 huku pesa hizo zikiongezeka kwa asilimia Fulani kwa kuwa bank watakuwa wanaziingiza kwenye mzunguko wa biashara na wote kufaidika.. Mwisho kabisa, Epuka kutembea na. Pesa nyingi bila kuwa na lengo la matumizi Fulani kwakuwa utatamani Kila ukionacho.
Wazo bora, ila hapo kwenye acc ya fixed mimi ningeshauri liquid fund ya utt.
 
Ulifika fedha kiasi gani ukapoteza, hiyo itanipa msingi wa ushauri.

Unanikumbusha ipo siku nauguliwa na mtu kisha nampigia simu mtu ninaemuamini nikope laki 2 nimtibu mgonjwa ananijibu hana kitu ilihalu nilikuwa na uhakika anayo, nilikaa sehemu nililia sana, nikajisemea hela nilizokuwa nazo mimi wa kukopa mtu leo laki mbili nimtibie mtu ninyimwe.

Anyway yule mgonjwa akafa.
Pole sana
 
Mimi wakati tunakaribia kufunga ndoa tu na mume wangu akafukuzwa kazi ,kazi iliyokuwa ikimlipa vizuri sanaaaa weee nikakaa nikajiuliza niendelee na hii ndoa au lah maana nilikuwa nawaza mimi nafanya kazi kwa wahindi mshahara wangu hauwezi kulipa kodi ya nyumba na sisi tukala nikamuomba Mungu nikasonga mbele na ndoa aisee si mchezo yani ukipokea mshahara ushaisha unaanza upya yani kila ikifika mwisho wa mwezi ndo machungu yanaanza.
Nikapata mimba hapo mume haingizi hata senti tano ila akawa tu ni mtu mzuri hana makwazo kwahiyo tukawa tunaongea lugha moja.Wakati kwa kujifungua ukafika ile nimemaliza mwezi mimi ni HR boss wangu kanipigia simu tukaongee kwenda ananiambia inabidi tufunge ofisi hataweza kuendelea kulipa wafanyakazi hivyo ni bora alipe watu akiwa bado ana pesa aiseee tulikuwa sehemu nilikuwa sielewi nini naongea mana nilikuwa nawaza mtoto nyumbani mwenzangu bado hajapata kazi [emoji1544] nilijikaza nikamjibu boss wangu sawa mana mimi ndo natakiwa kwenda kubreak the news.

Turudi nyuma kidogo mwenzangu kuna pesa aliipataga zamani basi akanisaidia kiasi kikubwa kuanzisha biashara yangu (na hii ndo sababu niendelee mbele na ndoa mana nilishajua ni mtu wa namna gani). So wakati haya yote yakiendelea tuliyokuwa tukiiendesha kwa hasara lakini sababu nilikuwa na kazi nikawa naendesha hvyo hivyo najipiga tafu kupitia kazi yangu ya kuajiriwa basi nilivyoona familia imeongezeka nikaona sitaweza kuihudumia biashara nikataka kuifunga kumbe Mungu ananichelewesha kuifunga kwani anajua nitakosa kazi,kazi ilivyoisha bahati nzuri nilikuwa nimepata maternity yangu karibuni nikachukua kiasi nikatemgeneza ofisi kidogo na tulipofunga ofisi sababu nilikuwa maternity nilipata mishahara kama mitano hvyo plus kiiunua mgongo basi tukakaa na mwenzangu tukaenda buguruni tukanunua kila kitu cha ndani at least kitakachotupeleka kwa miezi mitatu tukiwa tunajitafuta.

Mungu ni mwema hatuna maisha kama ya zamani lakini nimewekeza akili na kila kitu kwenye ile biashara yangu na sababu nipo mwenyewe naifanya mwenyewe na pesa sasa inaendesha maisha + na mume wangu anafanya kazi zake hakosi pesa za chakula.

Tusikate tamaa na kumuomba Mungu mana kila anapokupa jaribu anakupa na mlango wa kutokea mlango ni akili zinazokuongoza kutafuta namna ya kuzitatua na tujitume na kutokata tamaa.
Na zaidi kwenye maisha kukosa ni kawaida kama sio leo ni kesho.
Aisee kuna mwanawake wakuoa!
 
Nikiwa nimemaliza chuo sina hili wala lile, niko kitaa nikijipanga, nikachangiwa na ndugu zangu mtaji wa milion 4 point something huko, niende nikafanye biashara ya mchele toka Moro vijijini kuleta mijini na kusambaza kwa bei ya jumla.

Biashara mwanzo ilienda vizuri, mwisho wateja wangu wa siku zote wakawa wakopaji wangu wakubwa, malipo yakawa ya kuzungushana, nikawa mkali kidogo ila kwa bahati mbaya pesa ikawa ndogo kwenye mzunguko wangu, sinunui tena zile kilo nilizoanza nazo kwa wakati, mambo yakawa tofauti kidogo, nikaenda weee.

Mwisho wa siku nikachanganyiwa mchele kipuuzi kabisa na mtu ambae nilikua namuamini, nikajikuta nipo na mchele wa vitumbua na jamaa yule kakimbia, hapo ndio ukawa mwisho wangu, nilifilisika kama kuku, ndugu zangu hawakunielewa tena, nilipata stress kama tani 7 hivi.

Wakati tena nikapataga milion 3 kwa enzi zile haikua haba aisee, nikawa naishi vizuri tu, hizo elf 10 kwangu zilikua buku, sina cha kujibania kwa kweli, kuja kustuka nimenunua friji na tv tu vya geto tena ka friji kale kadogoo kabisaa, hela yotee imeisha katika njia zisizoeleweka, nilichanganyikiwa tena, sina nidhamu ya fedha.

Mwisho nikarudi zangu kusoma tena chuo ndio nikaja kutoboa kwa njia zingine kabisa kwa kutumia kazi niliyosomea.

Je, wewe unakumbuka vipi? Nini kilikupata?
Mi sister angu aaah alikua anahongwa hadi mil 50, mil 20, mil kumi......Kuna rfk ake na Ridhiwani Mzungu mmja hiv kam spoil sana sister sir tupo tunatoa mimacho tu.....eeh ukimuona sa hv sister angu yani sio yule R Dangote yani hata ukimwambia ccy twende ukanispoil anakwambia mdg angu sina ubavu huo

Mim kuhongwa pesa kubwa kabisa ni mil 5 nkahongwa mara ya pili tena mil 3 nkaongezea nkafungua biashara siku ya siku nliibiwa kila kitu dukani nlikua chizi fresh
 
Back
Top Bottom