Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nikiwa nimemaliza chuo sina hili wala lile, niko kitaa nikijipanga, nikachangiwa na ndugu zangu mtaji wa milion 4 point something huko, niende nikafanye biashara ya mchele toka Moro vijijini kuleta mijini na kusambaza kwa bei ya jumla.

Biashara mwanzo ilienda vizuri, mwisho wateja wangu wa siku zote wakawa wakopaji wangu wakubwa, malipo yakawa ya kuzungushana, nikawa mkali kidogo ila kwa bahati mbaya pesa ikawa ndogo kwenye mzunguko wangu, sinunui tena zile kilo nilizoanza nazo kwa wakati, mambo yakawa tofauti kidogo, nikaenda weee.

Mwisho wa siku nikachanganyiwa mchele kipuuzi kabisa na mtu ambae nilikua namuamini, nikajikuta nipo na mchele wa vitumbua na jamaa yule kakimbia, hapo ndio ukawa mwisho wangu, nilifilisika kama kuku, ndugu zangu hawakunielewa tena, nilipata stress kama tani 7 hivi.

Wakati tena nikapataga milion 3 kwa enzi zile haikua haba aisee, nikawa naishi vizuri tu, hizo elf 10 kwangu zilikua buku, sina cha kujibania kwa kweli, kuja kustuka nimenunua friji na tv tu vya geto tena ka friji kale kadogoo kabisaa, hela yotee imeisha katika njia zisizoeleweka, nilichanganyikiwa tena, sina nidhamu ya fedha.

Mwisho nikarudi zangu kusoma tena chuo ndio nikaja kutoboa kwa njia zingine kabisa kwa kutumia kazi niliyosomea.

Je, wewe unakumbuka vipi? Nini kilikupata?
Hapo ilikosa kitu kimoja tu,Nidhamu ya Pesa🥱.Hapo ilikuwa bahati mbaya zaidi kama ulikuwa Ntu ya Zotoz au Ntu ya Gilasi🏃🏃
 
Mi sister angu aaah alikua anahongwa hadi mil 50, mil 20, mil kumi......Kuna rfk ake na Ridhiwani Mzungu mmja hiv kam spoil sana sister sir tupo tunatoa mimacho tu.....eeh ukimuona sa hv sister angu yani sio yule R Dangote yani hata ukimwambia ccy twende ukanispoil anakwambia mdg angu sina ubavu huo

Mim kuhongwa pesa kubwa kabisa ni mil 5 nkahongwa mara ya pili tena mil 3 nkaongezea nkafungua biashara siku ya siku nliibiwa kila kitu dukani nlikua chizi fresh
Kelsea njoo huku uone kuwa tako mtaji watu wanahongwa hadi mil 50
 
Mkuu toa darasa kidogo nini umuhimu wa kuendesha biashara kama kampuni, je mtaji unapaswa kuwa kiasi gani ili kufungua biashara, mtu ana salon anaweza kuiendesha kama kampuni?
Mtaji wowote, Ili mradi uwe na shareholder. Unaweza kumpa mtu asilimia 3% baba au mama.
LLC ni body corporate kwa hiyo itashitaki na kushitakiwa, itaweza kukopeshwa na benki.
Itakuwa na akaunti yake, TIN namba yake.
Itakuwa na assets zake na liabilities zake.
Muhimu zaidi itatofautisha kati ya wewe na biashara zako. Huu ndiyo mwanzo wa heshims ya matumizi ya hela.
Ukiwa na hela nyingi kiasi, kopa na uendeshe biashara yako kwa kutumia mkopo wa benki.
Ndiyo matajiri wanachofanya. Kopa benki, kwa kutumia LLC.
Itakusaidia kwenye Kodi. Loans don't get taxed.
 
Mi sister angu aaah alikua anahongwa hadi mil 50, mil 20, mil kumi......Kuna rfk ake na Ridhiwani Mzungu mmja hiv kam spoil sana sister sir tupo tunatoa mimacho tu.....eeh ukimuona sa hv sister angu yani sio yule R Dangote yani hata ukimwambia ccy twende ukanispoil anakwambia mdg angu sina ubavu huo

Mim kuhongwa pesa kubwa kabisa ni mil 5 nkahongwa mara ya pili tena mil 3 nkaongezea nkafungua biashara siku ya siku nliibiwa kila kitu dukani nlikua chizi fresh
Kuongwa Mali zingine siyo za kupokeaa utaishiaa kudhalilika tu unaongwa milion 59 ssiter ako rinda lake liko salama kweli samahani lkn kwa lugha hyo
 
Back
Top Bottom