Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

hiyo milion 1.3 alikupa nani?
 
Starehe mnazipenda ila mwisho wake MBAYA. Wengi wameteketea kwa kuendekeza UMALAYA.

Ishi vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi na umrudie Muumba wako.

___________________________________________________________

Nikiwa na miaka 24 pindi tu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu niliingia mtaani, akilini na moyoni nikiwa na hari ya kuanzisha kampuni yangu. Ndoto niliyokuwa nayo tokea naingia form 3 ambapo niliacha masomo ya sayansi na kufwata kile moyo ulichoniambia KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.

Basi bana mwaka wa kwanza ukaisha nipo kitaa, moja haisimami mbili haikaii. Mwaka uliofwata nikiwa mtaani, nikaaanda mpango wangu biashara (ambao kwa sasa nikiusoma naona makosa mengi sana) nikaongea na wadau wawili watatu kupata mtaji wa biashara. Mungu si athumani wala hadija nikafanikiw kupata mtaji wa shillings 60,000,000.

Nikaingia kwenye biashara ya ununuzi (ulanguaji al-maarufu KANG'OMBA) korosho huko Mtwara wilaya ya Masasi. Simu wa kwanza mambo yalienda vizuri hela ilirudi. Nikaamua kwenda Uganda kufanya utafiti biashara ya mchele kule sasa mambo ndipo yaliponiendea kidogo kombo maana nilianza kupoteza taratibu pesa.

Long story short, nilikuja kupoteza pesa Million 60 shwwaaaaaa zikapotea zoootee kwenye korosho pale mzee baba (sijui huko alipo ni kiongozi wa malaika au anapigwa kama ngoma au ameenda kuwa umbwa marekani) aliposema serikali inaubavu wa kununua korosho (nyooo walijuta kilichowakuta)

Nimekaa miaka 5 kitaa sina uelekeo zaidi ya kuwa chawa kwa mwanangu wa ukwelii . Ila nilichojifunza ukianguka chukua mda kunyanyuka angalia mazingira ulipodondokea ukiwa bado chini,yatadhmini mazingira husila kisha ndio unyanyuke.

IMEKUWA MAUMIVU MAZITO ILA AKILI YA KUYASHINDA NILIJAALIWA NA MUNGU
 
Pole mkuu,vita bado inaendelea
 
Uyu C Hamis Kweli!!!?😮😮😮
 
2017 hapo nikiwa bado nipo chuo na penzi limekolea kwa mpenzi wa Maisha yangu. Ananipa mtaji wa sh laki 1 na 50 nikanunua dagaa Nyasa wale ili niwe nauza Dar.

Kabla ya hiyo biashara nilishafanya biashara kama kuuza sabuni na yebo yebo nilikua napeleka Masasi na Mwanangu James Ila akaja nidhulumu nikapotezea.

Basi bwana kwenye Maisha yangu sikuwahi kuwaona dagaa nyasa hapo kabla so Mara ya kwanza nikawaona nilipoenda songea nikawapenda.. Hivyo nikamuomba mchumba anisaidie mtaji ili niwalete Dar niuze kweli nikachukua sampuli dumila 10 nikaja nao dar kisha nikaenda kwenye magenge makubwa yale kuwapelekea wengi walikataa ikabidi niwape bure kisha wauze kama watanunulika basi tufanye biashara hapo baadae bado walikataa[emoji16] Ila magenge manne yakakubali nikaacha na namba za simu basi hazikuzidi siku 3 nikapigiwa simu tukaongee.

Basi bila hiyana nikajivuta tukakubaliana niwe napeleka mzigo nawaachia wanauza ukiisha Nafuata pesa.. Aisee nakiri wazi Moja Kati ya biashara ambayo siwezi isahau ni ile ilikubali nikawa napata mshiko wa maana(kiuanafunzi) Maisha yakabadilika japo mwanafunzi kusafiri Mara kwa Mara nikichukua mzigo wa laki 2 faida laki 2 ikaja mpaka Kule nilipokua nanunua wakawa wananipa mzigo kwa Mali kauli kutoka na mzunguko mkubwa.kufipisha stori niliweza kumiliki 3M+ bank zilizotokana na biashara ile nikiwa mwanafunzi na pikipiki(bodaboda) pia geto Kali Lakini vilipotea ndani ya wiki Moja tu baada ya kutapeliwa kwa mtu niliyemuamini kupita kiasi.

Shukrani kwa brother wangu alinihifadhi kwake na kunifariji maana ningejitundika kwa mawazo ule mwaka 2018 nilipoteza kila kitu mwishowe hata shule ningepoteza. Nilikuja kuinuka tena 2019 mwishoni Ila nikaja kupigwa na kitu kizito kwa uchawi qmmake ile unapika chakula Asubuhi mchana kimechacha Maisha ni Vita.
 
😂😂😂😂
 
Nmependa mbinu yako ya kuwaachia mzigo ukikubali mfanye biashara big up mwamba.
 
Pole sana mkuu mi mwenyewe nimeingizwa town juzi tu mwezi august na mwanangu sana baada ya kumaliza chuo hata sikuamini ila namshukuru Mungu saiv nishajipata.

Ukianguka unaamka unakimbia.

japo umenichekesha sana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Pole sana mkuu mi mwenyewe nimeingizwa town juzi tu mwezi august na mwanangu sana baada ya kumaliza chuo hata sikuamini ila namshukuru Mungu saiv nishajipata.

Ukianguka unaamka unakimbia.

japo umenichekesha sana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji16][emoji16] tujuze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…