Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nilishawai kufanya kazi ya marketing kwenye company moja that sitautaja jina and i was 18 than siyo siku nyingi sana, katika pita pita zangu za kazi nikakutana na mtu akanipa kazi ya tender ya 100 mil na kitu nikapata 10% yangu .. anyways nilipata
30 million.. kiukweli nikijifunza that ukipata hela without a plan it is like catching air anyways nilikuwa natamani sana gari flani i bought it and zingine nikafanya shopping no business whatsover and hela yote ikaisha.. il never forget. I learned alot from that experience...
Hela kiasi chochote ukipata bila jasho na bila kuwa na master plan ya maisha yako kuhusu maendeleo yako ya kiuchumi, pesa hiyo itapotea tu. Pesa ya wizi na dhulma ipo siku utaanguka tu. Katika uzi huu binafsi nimejifunza mengi, inabidi uwe na mpango wa matumizi na uwekezaji kabla hata hujapata pesa na siku ukipata ni kuanza kutekeleza mpango wako sio kuanza kufikiria ufanyie nn. Pia tamaa ya kutamani vikubwa hadi kudharau ulichonacho haifai kabisa
 
Ila haya maisha!...
Nilidrop chuo baada ya kuanza biashara ya dagaa nilianza na laki 9 natoa mwanza naleta Dar ndani ya mwaka nikafikisha 4m !Basi one day ziwani huko boti niliyopanda ikazama tushukuru kuna jamaa alibeba mafuta ya petroli so yale madum ndo yalituokoa.

Baada ya hapo nikaacha biashara ya dagaa nikaingia Ruvuma chimbo huko nikalima mahindi yakakubali kinoma shida soko likawa chini nikasema nipige stoo ili nisubirie price ipande ila ikawa hola!yakaa hadi yakaanza kukiwa na wadudu !nikaanza kulishia nguruwe. Wale nguruwe walikua 6 ila walijazana fasta kuja kutahamaki wako 85!Nikasema yuup hapa naenda kuwauza mjini Darisalama!Huku na kule kukayokea ugonjwa wa mafua ya nguruwe so ikapigwa stop hakuna mifugo yoyote kusafirishwa! Hapa nikichanganyikiwa ikizingatiwa chakula kilikwisha na pakupeleka hakuna!Nikaaza kuchinja na kuuza buchani lakini bado wanazengo hawakua walaji kule!

GHAFLA siku moja wakaja jamaa me fuso lao wanataka nguruwe sikujiukiza mara 2 nikawauzia wote kuja kufunga hesabu nina M27,300,000 Tsh! !!Nilisepa kiaina pale bush nikarud home kikubwa nikawajengea wazee then nikabakiwa na m9 nikasema niende ruaha mbuyuni kulima.Ku.ma.nyoko nilienda lima hela yote ikakatika kwenye kitunguu !Nikarud home kutuliza

pu. mbu huku na kule nikampiga sound ndugu yangu mmoja akanipa laki 8 nikazamia nayo machimboni huko nikapiga ponch sana ila hela ikawa inakata. Ilivyobaki laki 3 nikakimbia machimbo nikasettle mkoa flan nikawa dalali wa magari ya mizigo huku na kule within 6mth nikawa na 1m.Hapo nikaaza biashara ya mbao ndogo ndogo ,mwaka kuisha nikapata mtaji wa fuso !Biashara kuchanganya nikapata hadi mtaji wa semi.

Majanga yalianza pale nilipomwamini mteja wangu mmoja alikua mkenya !Alinipiga gari mbili nikawa vuzi kabisa na kuchanganyikiwa ju !nashukuru kuna jamaa yangu alijitokeza tukaungana tena tukagungua yard Dodoma ila tena tukaja zulumiwa na yard ikafa!Kurud home nikaanza kujipanga upya nikauza viwanja then nikarudi kwa biashara ya mbao ten .hadi leo nashukuru Mungu mambo yanaenda !
 
Niliwahi kupata milioni 120 nikiwa na umri wa miaka 26 kipindi hicho nipo mererani, nilichezea hiyo hela kwa muda wa miezi 8 nikabaki na laki mbili bank
Duh balaaa
 
Mkuu pesa haina kinga iwe kuingia au kutoka.

Kuna watu acount zilinona huku atujui ata bei soda.

Unazipanga kaa matofali ikizidi hamsini sio inaliwa bali inaenda tafutiawa miatisa hamsini ili ijae.
Upepo unapo geuka hutaamini.

Ajabu wala bata wako poa tu
Dah hapo ndo mtihani wa maisha ulipo...

Hapo ni sawa na mtu shuleni alikuwa full kujifungia na kusoma kwa bidii na kupata ufaulu wa juu kabisa (division au GPA) lakini ukija katika maisha halisia anakuja kuwa na maisha ya chini na yule ambae hakuwa akijimudu darasani au hazingatii kabisa masomo na alifeli maisha yake ni mazuri na ametoboa sana .
 
Pesa za kuhongwa zina mikosi, kama ilivyo za wizi
Yaan zinapoteaga tu ht hujui zimepoteaje. Dah nilikuwa na danga hilo lilikuwa linanimwagia mahela balaa ila sikuwahi kufanya cha maana jamani zaidi ya show off za kipuuzi tu. Baada ya kuachana nalo nikaamua na kuzaa ndio na akili ya kufanya maendeleo ikaja ila ni kwa hela zangu za halali.
 
Jamanii Pesaa ya BUMUU sio pesaa..yani unapewa kilaki 6 ndani ya week hujahonga hata.. Pesaa hunaa...!! Unaanza kushindiaa mikatee..Ivii mshahara unawezaje kutosha..!??? Discipline ya helaa wanayo wachache snaa
hahahaahaha umenichekesha sana na kunikumbusha jamaa yangu,alikuwa anashindia mikate hata haja aendi wiki nzima.

nilianza pata m1.2 mkwanja wa field chuo, niliishia nunua mashati ya chui chui tu.

nilimpiga mzungu m5 kwenye tumbaku, zilivyo isha mpaka leo sielewi na sina cha maana nilicho fanya.

now nna mipango na najichanga nifanye cha maana na mkwanja umekata, dili hakuna daa!! unaweza chizika.
 
Kiukwel leo naweza kwenda popote,muda wwte,naweza kula cchte,naweza nunua ving ambavyo watu wanataman kua navyo,wala sitok jasho,nilale,niamke hela napata tu,japo uchum umebadilika lakin siwez kushindwa kuyamudu maisha kwa hali yyte kwa sasa,na mwaka jana nilitaka kujenga shule ya awali mpk sekondar sema kuna ukiritimba flan nikakutana nao nikaghairi. So anaefilisika usimcheke hata siku moja maana anauwezo wa kurud barabarani na akafanikiwa zaid.

Mkuu pesa za riba uwe unatoa au kupokea hazijawah mwacha mtu salama hata upate kiasi gani zitakuja kukudhalilisha tu at the end[/QUOTE]
Bro labda upo sahihi ila ziliishaga zote wala sikumlaum mtu,zaid ya kitabasam na kuangalia nilipoanguka na kusonga.
 
Back
Top Bottom