Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Bwana mkubwa mi 2018 nilibeti Jackpot ya sportpesa nkapiga mil 2 na ushee. Baada ya kodi nkapata kama mil 2 na laki 6 hivi. Hela ilipukutika kama maji mkuu. Cha muhimu nilichofanyia nililipa nauli Mbeya Dar elfu 40. So hiyo hela ilinileta Dar es salaam. No cha msingi zaidi kilichofanyika kupitia hiyo hela.
 
Mimi kanuni yangu ,nikipata hela nyingi ,natenga kiasi cha kutolea wenge na kingine naficha kabisa,nikiangalia jinisi nilivokitumia ,roho ikiuma basi sigusi zilizobaki.

Mfano nimepata mil 1 za ghafla ,elf 50 natolea wenge.

Hela za ghafla ambazo kukutegemea au hujawai shika ,zinaweza kufanya ukawa mjinga au broke kuliko ulivo sasa.

#tujiandae kisaikolojia ,kwamba ,matumizi mabovu nisawa na tundu dogo chini ya tanki LA maji ,linavujiasha polepole Ila linawez maliza maji lisipozibwa


$kuna upande wa Bahati mbaya ,mazingira ya kazi au biashara ,ni kusali sana na kuchukua tahadhari na kushirikisha washauri wa masuala ya fedha na familia
 
Hua ananiambia kama kweli wewe ni mwanaume fanya niliyoyafanya au zaidi niliyoyafanya..2009 alizamia bondeni bila hata mwenyeji. Anakuambia alikula mikate mwezi anaishi stendi.
Alikaa kama mwaka na nusu huko. Alirudi yulo vizuri kuasi ila anakuambia ili laifu lisonge dona ilihusika kuuzwa
ahahahaa, mzee ni mafia
 
Mwezi wa 6 mwaka huu nlipata mlion 1.6, yani zaidi ya kulipa deni la laki 3 hizo nyingine sijui zimeenda wapi..
Pole sana.
Jaribu kuwa na mipango hata kama huna pesa. Fikiria mradi unaoweza kuufanya endapo ungepata kiasi fulani cha pesa haijalishi muda huo una hali gani.

Siyo kila mradi wafaa kuufanya.Tunaangamia kwa kukosa maarifa na papara ya kutaka ufanane na fulani badala ya kufanya jambo kwa kujiona wewe ulivyo.

Kwa kuwa huna mipango wakati huna pesa ndiyo maana leo hata upewe pesa ambayo ni bajeti ya nchi utaiharibu tu kama ulivyoharibu hiyo 1.3m.
Ukiona ugumu waulize waliofanikiwa wanaweza kukusaidia usiogope.
 
Back
Top Bottom