Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Mh Mimi ndo Hadi aibu

Nakumbuka kazi yangu ya kwanza nilibahatika kupata hela fulan Nilivorudi bongo starehe zikawa nyingi bar nilikua nazizunguka utafikiri mkaguzi wa mabar,

Nakumbuka siku moja nilikua bar na jamaa mmoja ambaye simjui ila nilimkuta hapo hapo bar Sasa katika meza yetu Kuna mdada aliyekua anatuhudumia alikua na tamaa ya hela, katika kumpa pesa alijizidishia elfu 5, Mimi nikamwambia yule mshikaji kwamba yule Dem anayetuhudumia anahisi ameniibia elf 5 na wakati hiyo sio pesa,,Yule jamaa akanambia mwanangu Hio ni pesa nyingi sana ipo siku utakuja kuikumbuka (nakumbuka jamaa aliongea kwa sauti ya uchungu sana kwasababu yeye alikuaga ni miongoni mwa wale watu waliotumbuliwa bandarini), alivoongea vile Mimi nilicheka sana Tena kile kicheko Cha dharau na kumwambia Mimi elf 5 si kitu kwangu naweza kumpa hela yyte anayoitaka ( haya mazungumzo nilipofulia yalikua yanajirudia kila siku Hadi nikahisi Yule jamaa ndo alinipa mkosi)


baada ya miezi 5 ya Bata zangu pesa ikaelekea ukingoni kibarua nacho kikawa tabu kila nkituma maombi jamaa hawanijibu taa nyekundu ikawaka kichwani kwenda bank kuangalia balance ilobaki,,, lahaula nikakukuta nimebakiwa na dola 1100$ tu. Nikaanza kuishi maisha Kama mtu aliyechizika kwasababu nilijua baada ya mda mfupi nitakosa hata pesa ya kulipia visa...kwa hakika niliishi maisha magumu yalojaa stress nyingi

Mungu hamtupi mja wake kabla kibubu hakijaisha kabisa nikapata kazi na ile hela ndogo ndo nikaitumia kusafiria mpaka eneo langu la kazi

Saiv nimerudi likizo bia naiona Kama mkunungu Yan haipiti kooni kabisa nikikumbuka ule msoto hata wanawake naishia kuchati nao tu Mambo ya kuendekeza chupi na bia ni big nooooo


Ila all in all ili hela uiheshimu ni lazima ufilisike kwanza bila hvyo ni kazi bure tu utawaona wanaofilisika ni matahira wasio na hata punje za akili.
Tupende kujifunza kwa watu waliofilisika tusiwaone hawana akili Kuna mengi wanaweza wakatushauri.
 
Nilipewa kama zawadi na Mother, nianzishe firm yangu ya mambo ya Upimaji ardhi, nilinunua baadhi ya vifaa tu (kama 3 M) nikabaki na 26M, kilichomaliza hela ni 'kuhonga ' madem wa tegeta, mbezi beach, kawe,ubungo,nakumbuka Kuna demu nilimnunulia passo 5 M, na mambo mengine ya kuhonga honga na statrue nyingine hadi 26M ikaisha, nikauza vifaa vya survey vyote
ikaisha yote (3m).
Ungekua mwanangu sijui ningekufanyaje[emoji848]
 
Vitu Vikubwa nilivyojifunza kwenye huu uzi..

1.Ni bora usiwe na hela kabisa kuliko kupata ukiwa hauna wazo la biashara.

2.Ogopa Pombe na mademu + marafiki wa ghafla ukipata hela..

3.Assets ndiyo mtunzaji mzuri wa hela kuliko bank..

tatizo ni moja: utapata madini ya kutosha katika huu uzi ila sasa ikifika zam yako hata wewe mwenyewe hutaamini kilichotokea: baada ya hivi vitu kukutokea mara ya kwanza na mara ya pili hapo sasa ndo utakua umejifunza kwel maaana ile njaaa utaskia itakufunza vitu vingi sana
 
Ushauri wa maana sana huu

Umekuwa wa maana zaidi kwa kuwa umetoka kwa mwanamke

Wanaume sijui tunakwama wapi, unahonga kitu kikubwa hivyo kwa demu na hamna commitment naye yoyote (sio mke, huna mtoto naye n.k)
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hufai kufarijiwa kbs aisee...hv mnazuzuka nn kuhonga gari??yaan bora ungemfungulia biashara ila iwe yako lakini usimamiz na ww unakuwepo..akizengua unamfukuza mapemaaa!mtu wa kumnunulia gari ni wife tu!..ww hufai ht kubenbelezwa jibembeleze mwenyewe
 
Mkuu pole

Tractor vipi kwenye kuingiza kipato?

Ulikuwa maeneo gani@KANYEGELO,
Trector lipo vizuri kwenye kuingiza kipato ila kwa mimi la kwangu nalitumia msimu tu wa kilimo ni berlaus kutoka urusi mashine ya kazi ,NIPO MAENEO YA WILAYA YA BUSEGA MKOA WA SIMIYU

Kwa mwezi sikosi milion 3 au 2.5 ila sana sana nafanya biashara mwezi wa 11, mpk Aprill baada ya hapo linapakiwa tu linakuwa halina kazi
 
Mkuu pole

Tractor vipi kwenye kuingiza kipato?

Ulikuwa maeneo gani@KANYEGELO,
Tractor lenyewe ndio hili....limebaki kama ukumbusho wa pesa nilizojichanga kutoka nazo ujerumani
images.jpeg
 
Back
Top Bottom