Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Nlifilisika kabisa kipind cha korona biashara ilikuwa ngumu had nikauza frame kkoo, mke akaniacha , wana na baadhi ya ndugu walinicheka asa ivi nimerudi kwenye form hao hao wanaomba msaada nawazoom tu, uyo mwanamke anajifanya mwema asa ivi kunishaur sina kinyongo na mtu ila nimewajua vizur yupi wangu yupi si wangu.
Shikilia hapo hapo Mzee .....
 
Nilipewaga dola 100 zamani sana na danga limoja hivi aiseee kwa kipindi kile ilikuwa hela nzuri nikaja nikaila bila kuelewa imepita wap

Nikaja kupewa tena mil 1 na hilo hilo danga zamani kidogo nayo haikufanya la maana

Nikaja nikapata danga lingine likanipa m2 nazo nimefanyia kazi haikuzaaa

Tangu wakati huo miaka imepita sitaki tena hela za madanga, nimeolewa na ninatafuta hela kihalali.

Msiwashangae kina Wema hela za kudanga hata upewe bil 1 huwa zinayeyuka.
Huwa tunaziloga kwanza
 
Idris Sultan alipata Tsh 500m ambazo ni zaidi ya U$D 200,000. Zilienda wapi? Na kama mtu anaweza kuchezea USD 200,000 watu wanashangaa nini mtu kuchezea USD 1m? Umesema vizuri kabisa starehe hazina mwisho. Ukiwa na USD 1m, demu akikuambia umlipe 50m utaona mbona hela ndogo sana hiyo..?
zilienda huku[emoji16][emoji16][emoji16]
IMG_20220907_025748.jpg
 
Mnamo 2019 SEP hadi2020july,nilipoteza zaidi ya milioni12,nilizokopa kutoka Ajira yaserikali nikatia katika kilimo cha ufuta naununuzi waufuta,hakika nilifeli Sana kutokana namvua kunyesha sana napia kulipia garmaa zauendeshaji napia ununuzi WA ufuta kwanjia ya kangomba bei zilikuja chini,Hadi sahizi KAZI niliyonayo naioma chungu kutokana namakato ya Benki,naishi kikachelo Tu kwakubangaiza maisha ghali,majukumu yameongezeka yakifamilia hela nayoipata Kwa mwezi haikidhi mahitaji.
 
Duh,sikuwah kupewa hela,sikuwah kuomba mtaji ila nilipiga kbarua nikapata 8000 (elfu nane) nikaanza biashara ya kamba za simu,nikauza kila siku napata faida 4000 -5000 nikameki mpk ikafika laki na nusu,nikaanza kununua na housing za simu,biashara ikanenepa mpk kufika laki tano,nikafungua kibanda cha mbao,nikaendelea kdgo kdgo nikapata compiter nikaanza kuweka mziki,nikakomaa kama mwaka hiv,kipimd kile kuweka mziki mmoja jero bas kwa siku napata 20k ikipungua snaa 15k,nikaanza kuweka simu moja moja huko nje ya mji,nikauza kama sina akil nzur,nikafukisha mtaji wa milion 4,kiukwel nikaingia kwenye frem,we bwana wee wacha nikomae muuza simu maaruf,nikakomaa nikawa na nyumba na kagar vitz,CHA kunisogeza mjini,nikakomaa hvyo hvyo kuja kutamalaki nina zaid ya milion 20,nikaanza kukopesha watu kwa riba,unakuja na gari na kadi nakupa hela,aisee nikapiga mihela kila siku na maisha yakawa safiii.



Balaaa lilipoanzia...

nikapata mchongo wa madin kule tanga sehem za kigongoi na kigwase,sina uzoef,siyajui madin wala sijui soko,hapa ndo penye tatizo kwa weng,naletewa madin hata kuyakagua sijui halaf naemtegemea kumbe nae hajui tunanunua mabov tu,najua tunaenda kupata hela town kumbe naenda kuumizwa,sikukata tamaa,nikafanya tena na tena lakin wap,mwsho nikakuta nimepoteza karib milion 17 bila faida,nikaona isiwe tabu,nikaanza kuchimbisha watu mm mfadhili,nikapiga piga hela ikakata,nikaangalia nyuma na kuangalia nilipo anguka nikajua ni uzoefu na utaalam wa madin sina,nikaendelea kukomaa nikauza gar,kupeleka hela mgodin holaaa,duka nimefunga,mtaji umekata,na sina mbele wala nyuma...
Mm mwanaume nilianza sifir nikapata hela sasa nikaenda kwa wakwe zangu nikawaomba nimwache mke pale miez sita kuna mahali nahitajika,kosa waliloffanya ni kukubali,bas baada ya kumwamishia mke pale na mtoto nikaondoka nikaipiga nyumba bei,nikauza kila kitu bila mke kujua,nikapata kama 22m maana niliiuza sbu ya uharaka nyumba yenye thaman zaid ya 40ml. Nikasepa zang mgodini,asee yaliyonikuta nikachanganyikiwa zaid,nikaitumbukiza hela na haikurud hata mia zaid ya maden,nikabakiwa mikono mitupu,nyumba,duka,gar,mke sina kwa kipind hcho japo mke najua nikirud ntampata. Nikamtapele jamaa mmoja laki na nusu nikakimbilia mbinga songea kulima mahind vibarua maana naona aibu ya kurud,nikapiga msimu wa kwanza nalala kwa mshakaji wng kimya kimya dunia haijui nilipo,nikaomba nami heka moja nilime mazao yangu,nikakomaa haswa asee duuuh achen asee maisha haya,bas nikapata gunia tisa nikazilipua fasta gunia moja 20k nikasepa zangu tabora,maana nina ifaham kwa kias,nikapata dili la asali,watu wana asali pa kuiuza kwa dar hawapajui nikaona fursa hii,nikawaambia mm ninamteja dar twenden,tukaja mpka dar[emoji3] [emoji3]

nilipo fufukia
,nikawapeleka kwa mshakji wakauza asali ya milio 9 kama sikosei,wakakosea wakanipa laki tano,nikawaambia kaleten nyingine najua pa kuuza bei kubwa zaid,wakaenda huko wakakusanyaaaa za nyuki wa kubwa na wadogo,kuleta mzigo nam nilikua nimepata jamaa muhindi anainunua,bas kushusha tu mzigo hela hizo,genji yangu na ujanja nikapata 2ml. Nikasema nipange chumba kulala kwa washkaji nimechoka,nikapanga chumba tabata liwit uswahilin,kila wakileta mzigo dar mm ndo mjanja wao napata laki tano mok milion,muda wote mke hajui nilipo wala namba zang hana na niliamua makusud kukaa hvyo,baada ya miaka mitatu ya asali nikajikuta nina zaid ya milion 4,nikaanza tena kurudia biashara yang ya zaman japo nilikua na mtaji lakin soko lilikua shida,nikaona niwe mbunifu zaid,nikakomaa na biashara ya kutembeza mpka nikafungua tena frem,bas bhna mungu akivyo wa ajab,naletewa simu za ishu kutoka nairob nauza jumla jumla siku mbili sina kitu,biashara ikarud kwenye mstari,nikanunua sehem kule pugu shule ya sekondar nikaanza kuinua kdgo kdgo,mpk nilipohakikisha nimepauwa ndo nikarud kumsalimia mke na mtoto,zaid ya miaka mitatu nilivyokua mkimbiz ndan ya nchi yngu. Kiukwel leo naweza kwenda popote,muda wwte,naweza kula cchte,naweza nunua ving ambavyo watu wanataman kua navyo,wala sitok jasho,nilale,niamke hela napata tu,japo uchum umebadilika lakin siwez kushindwa kuyamudu maisha kwa hali yyte kwa sasa,na mwaka jana nilitaka kujenga shule ya awali mpk sekondar sema kuna ukiritimba flan nikakutana nao nikaghairi. So anaefilisika usimcheke hata siku moja maana anauwezo wa kurud barabarani na akafanikiwa zaid.
Hii comment yako mkuu, imehamasisha wengi. Shukrani sana
 
Mnamo 2019 SEP hadi2020july,nilipoteza zaidi ya milioni12,nilizokopa kutoka Ajira yaserikali nikatia katika kilimo cha ufuta naununuzi waufuta,hakika nilifeli Sana kutokana namvua kunyesha sana napia kulipia garmaa zauendeshaji napia ununuzi WA ufuta kwanjia ya kangomba bei zilikuja chini,Hadi sahizi KAZI niliyonayo naioma chungu kutokana namakato ya Benki,naishi kikachelo Tu kwakubangaiza maisha ghali,majukumu yameongezeka yakifamilia hela nayoipata Kwa mwezi haikidhi mahitaji.
Pole sana brother, hakuna mapambano marahisi katika kujikomboa na umaskini.
Kuanguka na kuinuka ni kwingi sana , wakati utakuja wa kuinuka tena
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hufai kufarijiwa kbs aisee...hv mnazuzuka nn kuhonga gari??yaan bora ungemfungulia biashara ila iwe yako lakini usimamiz na ww unakuwepo..akizengua unamfukuza mapemaaa!mtu wa kumnunulia gari ni wife tu!..ww hufai ht kubenbelezwa jibembeleze mwenyewe
[emoji38][emoji38][emoji38] mkuu bhana
 
[emoji2][emoji2]
Kuna vitu haviko sawa
Alipata mil300 2019, adi unakutana nae tena alikuwa na scania 23, apo ni kama mwaka nyuma ina maana 2020 hivi au 21 mwanzon, yani baada ya mwaka moja akawa na scania 23, kuna uongo apa, maana kichwa kimoja cha scania ni mil70 mpaka 300 kutegemea na aina na upya na scania na treller ni kama milion100, sasa huo uongo sijui unautetea vipi

Umu kuna uongo mwing unanukia
 
Na yawezekana pia na mshahara utakua unaingia lakini unakua diverted, atafute mwanasheria amsaidie
Mi sijasomea Sheria nachojua kama hawajakupa termination letter means wanakutambua kama mfanyakazi wao pengine ukipata mtu anaejua Sheria anaweza kukupa abc za kupata haki yako. Kila la heri mkuu
 
Nilipewaga dola 100 zamani sana na danga limoja hivi aiseee kwa kipindi kile ilikuwa hela nzuri nikaja nikaila bila kuelewa imepita wap

Nikaja kupewa tena mil 1 na hilo hilo danga zamani kidogo nayo haikufanya la maana

Nikaja nikapata danga lingine likanipa m2 nazo nimefanyia kazi haikuzaaa

Tangu wakati huo miaka imepita sitaki tena hela za madanga, nimeolewa na ninatafuta hela kihalali.

Msiwashangae kina Wema hela za kudanga hata upewe bil 1 huwa zinayeyuka.
Malinda yapo kwel
 
Asante kwa funzo mkuu
Mimi wakati tunakaribia kufunga ndoa tu na mume wangu akafukuzwa kazi ,kazi iliyokuwa ikimlipa vizuri sanaaaa weee nikakaa nikajiuliza niendelee na hii ndoa au lah maana nilikuwa nawaza mimi nafanya kazi kwa wahindi mshahara wangu hauwezi kulipa kodi ya nyumba na sisi tukala nikamuomba Mungu nikasonga mbele na ndoa aisee si mchezo yani ukipokea mshahara ushaisha unaanza upya yani kila ikifika mwisho wa mwezi ndo machungu yanaanza.
Nikapata mimba hapo mume haingizi hata senti tano ila akawa tu ni mtu mzuri hana makwazo kwahiyo tukawa tunaongea lugha moja.Wakati kwa kujifungua ukafika ile nimemaliza mwezi mimi ni HR boss wangu kanipigia simu tukaongee kwenda ananiambia inabidi tufunge ofisi hataweza kuendelea kulipa wafanyakazi hivyo ni bora alipe watu akiwa bado ana pesa aiseee tulikuwa sehemu nilikuwa sielewi nini naongea mana nilikuwa nawaza mtoto nyumbani mwenzangu bado hajapata kazi [emoji1544] nilijikaza nikamjibu boss wangu sawa mana mimi ndo natakiwa kwenda kubreak the news.

Turudi nyuma kidogo mwenzangu kuna pesa aliipataga zamani basi akanisaidia kiasi kikubwa kuanzisha biashara yangu (na hii ndo sababu niendelee mbele na ndoa mana nilishajua ni mtu wa namna gani). So wakati haya yote yakiendelea tuliyokuwa tukiiendesha kwa hasara lakini sababu nilikuwa na kazi nikawa naendesha hvyo hivyo najipiga tafu kupitia kazi yangu ya kuajiriwa basi nilivyoona familia imeongezeka nikaona sitaweza kuihudumia biashara nikataka kuifunga kumbe Mungu ananichelewesha kuifunga kwani anajua nitakosa kazi,kazi ilivyoisha bahati nzuri nilikuwa nimepata maternity yangu karibuni nikachukua kiasi nikatemgeneza ofisi kidogo na tulipofunga ofisi sababu nilikuwa maternity nilipata mishahara kama mitano hvyo plus kiiunua mgongo basi tukakaa na mwenzangu tukaenda buguruni tukanunua kila kitu cha ndani at least kitakachotupeleka kwa miezi mitatu tukiwa tunajitafuta.

Mungu ni mwema hatuna maisha kama ya zamani lakini nimewekeza akili na kila kitu kwenye ile biashara yangu na sababu nipo mwenyewe naifanya mwenyewe na pesa sasa inaendesha maisha + na mume wangu anafanya kazi zake hakosi pesa za chakula.

Tusikate tamaa na kumuomba Mungu mana kila anapokupa jaribu anakupa na mlango wa kutokea mlango ni akili zinazokuongoza kutafuta namna ya kuzitatua na tujitume na kutokata tamaa.
Na zaidi kwenye maisha kukosa ni kawaida kama sio leo ni kesho.
 
Sisi tuliwahi pitia hii situation

Ndugu walijaa sana home pale

Ukaa msoto mmoja mkali sana mzee akawa juu ya mawe for 3 damn years .

Bimkumbwa ndio anasimamia show za home .

Walipotea wote[emoji1787] marafiki wa mzee walipotea wote hawaji na magari yao home .

Mzee aliisha suruali zikawa hazimtoshi ,bia akawa anaiona chungu .

Miaka 3 baadae akapata dili fulani analofanya Hadi leo karudi stable kiuchumi Mara 2 zaidi hawaji Tena siku hizi .

Na mzee gambe zimepungua kabisa kwanza umri ushamtupa yuko around 60's huko .na uzuri wote tulishakuwa na tuna maisha yetu

Filisika akili ikukae sawa
Kwakweli ukifilisika Akili inakukaa Sawa.
 
Back
Top Bottom