Duh,sikuwah kupewa hela,sikuwah kuomba mtaji ila nilipiga kbarua nikapata 8000 (elfu nane) nikaanza biashara ya kamba za simu,nikauza kila siku napata faida 4000 -5000 nikameki mpk ikafika laki na nusu,nikaanza kununua na housing za simu,biashara ikanenepa mpk kufika laki tano,nikafungua kibanda cha mbao,nikaendelea kdgo kdgo nikapata compiter nikaanza kuweka mziki,nikakomaa kama mwaka hiv,kipimd kile kuweka mziki mmoja jero bas kwa siku napata 20k ikipungua snaa 15k,nikaanza kuweka simu moja moja huko nje ya mji,nikauza kama sina akil nzur,nikafukisha mtaji wa milion 4,kiukwel nikaingia kwenye frem,we bwana wee wacha nikomae muuza simu maaruf,nikakomaa nikawa na nyumba na kagar vitz,CHA kunisogeza mjini,nikakomaa hvyo hvyo kuja kutamalaki nina zaid ya milion 20,nikaanza kukopesha watu kwa riba,unakuja na gari na kadi nakupa hela,aisee nikapiga mihela kila siku na maisha yakawa safiii.
Balaaa lilipoanzia...
nikapata mchongo wa madin kule tanga sehem za kigongoi na kigwase,sina uzoef,siyajui madin wala sijui soko,hapa ndo penye tatizo kwa weng,naletewa madin hata kuyakagua sijui halaf naemtegemea kumbe nae hajui tunanunua mabov tu,najua tunaenda kupata hela town kumbe naenda kuumizwa,sikukata tamaa,nikafanya tena na tena lakin wap,mwsho nikakuta nimepoteza karib milion 17 bila faida,nikaona isiwe tabu,nikaanza kuchimbisha watu mm mfadhili,nikapiga piga hela ikakata,nikaangalia nyuma na kuangalia nilipo anguka nikajua ni uzoefu na utaalam wa madin sina,nikaendelea kukomaa nikauza gar,kupeleka hela mgodin holaaa,duka nimefunga,mtaji umekata,na sina mbele wala nyuma...
Mm mwanaume nilianza sifir nikapata hela sasa nikaenda kwa wakwe zangu nikawaomba nimwache mke pale miez sita kuna mahali nahitajika,kosa waliloffanya ni kukubali,bas baada ya kumwamishia mke pale na mtoto nikaondoka nikaipiga nyumba bei,nikauza kila kitu bila mke kujua,nikapata kama 22m maana niliiuza sbu ya uharaka nyumba yenye thaman zaid ya 40ml. Nikasepa zang mgodini,asee yaliyonikuta nikachanganyikiwa zaid,nikaitumbukiza hela na haikurud hata mia zaid ya maden,nikabakiwa mikono mitupu,nyumba,duka,gar,mke sina kwa kipind hcho japo mke najua nikirud ntampata. Nikamtapele jamaa mmoja laki na nusu nikakimbilia mbinga songea kulima mahind vibarua maana naona aibu ya kurud,nikapiga msimu wa kwanza nalala kwa mshakaji wng kimya kimya dunia haijui nilipo,nikaomba nami heka moja nilime mazao yangu,nikakomaa haswa asee duuuh achen asee maisha haya,bas nikapata gunia tisa nikazilipua fasta gunia moja 20k nikasepa zangu tabora,maana nina ifaham kwa kias,nikapata dili la asali,watu wana asali pa kuiuza kwa dar hawapajui nikaona fursa hii,nikawaambia mm ninamteja dar twenden,tukaja mpka dar[emoji3] [emoji3]
nilipo fufukia
,nikawapeleka kwa mshakji wakauza asali ya milio 9 kama sikosei,wakakosea wakanipa laki tano,nikawaambia kaleten nyingine najua pa kuuza bei kubwa zaid,wakaenda huko wakakusanyaaaa za nyuki wa kubwa na wadogo,kuleta mzigo nam nilikua nimepata jamaa muhindi anainunua,bas kushusha tu mzigo hela hizo,genji yangu na ujanja nikapata 2ml. Nikasema nipange chumba kulala kwa washkaji nimechoka,nikapanga chumba tabata liwit uswahilin,kila wakileta mzigo dar mm ndo mjanja wao napata laki tano mok milion,muda wote mke hajui nilipo wala namba zang hana na niliamua makusud kukaa hvyo,baada ya miaka mitatu ya asali nikajikuta nina zaid ya milion 4,nikaanza tena kurudia biashara yang ya zaman japo nilikua na mtaji lakin soko lilikua shida,nikaona niwe mbunifu zaid,nikakomaa na biashara ya kutembeza mpka nikafungua tena frem,bas bhna mungu akivyo wa ajab,naletewa simu za ishu kutoka nairob nauza jumla jumla siku mbili sina kitu,biashara ikarud kwenye mstari,nikanunua sehem kule pugu shule ya sekondar nikaanza kuinua kdgo kdgo,mpk nilipohakikisha nimepauwa ndo nikarud kumsalimia mke na mtoto,zaid ya miaka mitatu nilivyokua mkimbiz ndan ya nchi yngu. Kiukwel leo naweza kwenda popote,muda wwte,naweza kula cchte,naweza nunua ving ambavyo watu wanataman kua navyo,wala sitok jasho,nilale,niamke hela napata tu,japo uchum umebadilika lakin siwez kushindwa kuyamudu maisha kwa hali yyte kwa sasa,na mwaka jana nilitaka kujenga shule ya awali mpk sekondar sema kuna ukiritimba flan nikakutana nao nikaghairi. So anaefilisika usimcheke hata siku moja maana anauwezo wa kurud barabarani na akafanikiwa zaid.