Tuliowahi kuteswa na marejesho ya mkopo tukutane hapa

Mimi mkopo ulichonifanya sitokaa nikope milele mpk naingia kaburin
Nitaridhika na ninachopata
Bora sahiz nasave hela naiona aisee
Mkopo ulikuwa unifilisi kabisa
Ila afisa mkopo ni mbwa hawana huruma
Rejesho mil 5.8 kwa mwez halafu sikuwa mzoefu wa mikopo hata kunishaur nisogeze mbele mkopo ili marejesho yapungue wakashindwa wakaniacha nakufa na tai shingon mbwa wale sitowasahau kamwe
 
Aisee mkuu daah
 
Hahahah
 
Milioni 5.8 kwa mwezi parefu kinyama. Anyway, inategemea na biashara pia.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mkopo wa MGODI voda, nilikopa siku nataka kulipa mtandao ukasumbua. Nikasema itakula kwenu leo kesho yake wakaanza meseji zao Mimi nimetulia tu.

Zikapita siku kadhaa, si Kuna bwege kanipigia kwa namba 100 ananikoromea kisa 3,600. Nilichomjibu akanifungia huduma ya mpesa. Kesho yake naweka elfu 2 bila kujua kumbe kaifunga, nawapigia simu wananiambia nilipigiwa simu nikawajibu vibaya kwa hiyo niende voda shop na kitambulisho.

Nikawaambia laini ninazo nyingi sina huo muda wa mchezo, nikaitoa nikaivunja nikaweka ya tigo.
 
Kuna kikampuni hapo dodoma kinakopesha kwa dhamana ya kiwanja, chombo cha moto, ama nyumba, muhimu uwe mmiriki halali, watafute hao, uwapige hela, ukishindwa kurudisha wanachukua chako kinakuwa chao, unakuwa kama umeuza mali na kupata pesa...THE DEAL DONE, hivyo ndivyo maharamia tulifanya biashara bila kuhangaika na wateja[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…