Tuliowahi kutuma SMS kimakosa kisha zikatutia aibu na kashikashi tuje hapa

Dah Mimi ilinipata hi niliitwa na jamaa Sasa nikawaza natokaje home nikamzuga baba angu mdogo (Marika yetu yalikuwa sawa) nikamwambia twende nisindikize ntakutoa

Sasa tukarudi late mzee keshafunga mlango bamdogo akagonga mzee akafungua akawaka kidogo Sana na hakuwa na wasi wasi kwakuwa nilikuwa na bamdogo
Sasa nikawa naandika massage kumtumia jamaa kumshukuru kwa muda mzuri tuliokuwa nao na kumweleza jinsi bamdogo alivyouwa Soo ile massage ikaenda kwa baba arooooo kilichotokea Siri yangu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23]hii umetungaa

Serious man, yani nimerudi home nimekaa dining kuna sms ya wife ilichelewa kufika so ikafika wakati nipo pale mezani....wakati namtumia sms mtoto Nasra kumbe namwandikia wife ile nakuja kushtuka nishaisend...halaf ilikua sms ya kawaida hata kudelete huwezi
 
Sorry nje ya mada kidogo ila scenario zinafanana sana, jamaa yangu 1 ana mambo mengi sana kama unga wa ngano.. juzi kati niilimuomba ile video ya bi dada Meny,, hasa badala anitumie inbox kumbe anaipost status (afu kideo yenyewe ndo ile bi dada anakatikia mkunyenge) jamaa kaipost watu wana i view mwana hana hata habari anashangaa simu ya mzee wake inaingia si muda bi mkubwa wake nae kampigia.. Sms za ndugu zake ma aunt, wajomba ndio usipime.. Mwana alienda chooni kuharisha ghafla aka delete acc ya whatsapp huko huko toilet
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hii noma aisee

Daaaah aibu lake si mchezo. Ilo kama ni mimi ningewekwa na kikao
 
Nakumbuka ilikua niko chuo mwaka wa pili, nilikua na appointment na demu ili niwe nawe faragha usiku huo. Sasa niliaga nyumbani kua naenda kumsalimia rafiki yangu anaumwa. Sasa wakati demu yupo njiani ana kuja. Nikamwambia atamikuta stand na nimechukua gest ya jirani na stand. Sasa kutuma nikakosea ikaenda kwa mdogo wangu wa kike na anajua kua niliaga naenda kulala kwa rafiki yangu. Basi ile natoka akanambia kaka safari njema. Daaahh nikabaki nazuga tu, aibu kibao, demu yupo njiani katoka mkoa mwingine kurudi haiwezekani.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we jamaa tupe mrejesho ilikuajee
 
Ilinimutaga hiyo, kuna demu nilikua nina mahusiano nae na nilikua nampenda sanaa, siku akakosea sms ya jamaa yake mwingine akatuma kwangu. Nilichofanya ni kumtafuta kwa namba nyingine nikamwambia nimeibiwa simu, ila nikipiga haipokelewi, ili asijue kua nimeiona sms yake, na yeye wala hakusema kua alikosea sms ilipita kama wiki 2 hiv tukaja kuonana na nina simu ileile, alikua mpoleee na mm wala sikumuuliza
 
Mtakuwa mnaishi uzunguni...
 
Mwaka 2008 hiyo nipo 6, tulikuwa tunakaa hostel na madogo wa O level humo ndani kulikuwa na makuzi hatari, hiko kipindi Xtreme ndio imepamba moto. Siku hiyo jpili tunasubiri msosi mchana kila mtu yupo dekani kwake, mara kidogo tukamuona mshikaji karuka kutoka juu dekani mpaka chini simu akairusha kitandani

Tukamuuliza vipi!? Akanipa simu niisome hizo texts zake, kuna namba mpya ikawa imeingia hakuitambua.

No mpya: hujambo?
Jamaa; sijambo, habari yako
No mpya; salama za siku
Jamaa; salama
Jamaa; nani mwenzangu?
No mpya; ur mom
Jamaa; hebu kuwa serious, nani wewe!?
No mpya; ur mom
Jamaa; sasa nikusave Ur mom au Mkumer!?


Ikaingia sms inamwambia"Umelaaniwa we mtoto yaani unaniita mimi mama yako Mkum*!!!? Na usirudi nyumbani mbwa we, utafute pa kwenda. Kumbuka hiyo likizo ya Dec ilikuwa inakaribia.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Goite
 
Dah aise umenichekesha sana!
Pole mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…