Tuliowahi kuumwa sikio/masikio tukutane hapa

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
jamani kuna uzi wa jamaa kule anaelezea alikuwa anaumwa jino. Nimeona na mimi nielezee jinsi sikio la kulia lilivyochakaza!

Yaani sikio,jino,macho sio vitu vya kuchezea kabisaaa..
Mimi nilikaaa week 2 navumilia tuu. inahitaji moyo bandugu!!

Usiku nilikuwa napanda dirishani, nakaa chini, navua Nguo, navaa tena, naoga hata mara kumi! ila ndo kwanza sikio linachochea! yaani mpaka nilikuwa naimba kwaya, singeli ila wapi!!
usiku nauona una masaa 70 sijui???
Ikabidi nijisalimishe general hospital mwenyewe!
Njiani Dereva bajaji anaendesha taratiibuuuu! nikaona huyu mshenzi ataniuwa! nikakamatia chuma mwenyewe!!
Kufika hospitali nakuta madingi mawili na mtoto mmoja yupo na mamake ..yule mtoto alikuwa analia ila sauti yake ilishakauka! yule dingi mmoja alikuwa kalala chini.. mwingine yupo stoo sijui alikuwa ndo anapooza maumivu!.
Nikapewa dawa niliambiwa kuna kidonda ndani! so kama kawa usiku dozi ikaendelea! Nikawa nachukua mpira nacheza nje usiku! ila wapi!
Mpaka nilipokuja kuwekewa bangi!(msokoto) /(chiga) kwenye sikio...
Huwezi amini hiyo siku iliofuata nilijiona niko uko akhera nikiwa na mabikra 70 na mto wa pombe
Mpaka leo haliumi tena. Kweli bangi ibarikiwe!
 
Me wakati niko mdogo sana nilikua nasumbuliwa na sikio.. nakumbuka nilipewa bangi kama dawa... una chukua bangi una weka kwenye maji baada ya muda una weka yale maji kwenye sikio
Ndo hivyo mkubwa yaani
 
Mi mpaka sasa hivi sikio Lina muwasho usio wa kawaida linasumbua balaa ila nahisi Ni allergies nilienda muhimbili pale ENT kitengo Cha Koo sikio na pua wakanifanyia wax removal nikatolewa uchafu Sana..baada ya mwaka likaanza Tena kuwasha Nikaenda ekenywa hospital magomen pale nikapata Tina na kushauriwa kuwa hakikisha sikio haliingii maji hata ukiwa unaoga paka mafuta ya mgando kwa ajili ya ku protect maji kuingia
USHAURI:KAMA UNA UWEZO NUNUA PAMBA UKIWA UNAINGIA BAFUNI ZIBA MAJI YASIINGIE INAEZA KUSAIDIA MAANA MAJI NA SIKIO HAVIPATANI KABISA
 
Nimeumwa masikio yote mawili

Sikio linauma sjapata kuona, mimi usiku kucha nalia usingizi naupata saa kumi na moja alfajiri, nikaambiwa weka mafuta ya kuku wapi nijispray perfume wapi bangi sikupata nimemaliza hospital nikaenda pona kuna baba anaitwa rasheed akanambia nina kidonda akanipa dawa ndio aliniponesha na akanipiga bomba asee sitaki hata yanirudie

Mimi ni muoga wa dawa lakini kwenye sikio nilikunywa na sindano niakzivumilia ah wapi nikampataga dokta mmoja anatokea muhimbili ilibidi niweke appointment naye siku ya kwenda mama anabeba mkoba mtandio kuuvaa siwez nimeufunga kilemba dokta alikua ananiweka mapamba na madawa akitoa damu tele mama akanambia utafanywa masito tukahama hospital wallah sitasahau baada ya kupigwa bomba sijawah kuumwa tena sikio had leo
 
Mkuu rudi hospitali vinginevyo utachakaa na roho yako
 
Pole sana madam uchungu huwaga anaelewa mwenye tatizo!
 
Pole sana, mimi nilikuwa na dalili za kuumwa sikio kuna siku mzee kaniwasha kibao cha sikio nashukuru toka siku ile nilipona.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimecheka kama mazuri vile asante πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Pole sana, mimi nilikuwa na dalili za kuumwa sikio kuna siku mzee kaniwasha kibao cha sikio nashukuru toka siku ile nilipona.
 
Mpaka sasa nishachoma sindano kumi na 3, bado mama analazimisha niendelee kuchoma, mara nibadilishiwe dawa/dozi.

Nimetumia mafuta ya kuku,dawa za kuminyia ndani kwenye sikio wapi, .

Hadi kuna vidonda vimetokeza ila me ni outer ear ndo kuna matatizo ila yakianza kuuma maumivu kichwa kizima uso,meno .

Dah ni hatari nshatumia dawa kama zote ila wapi, .

Ngoja nijaribu msuba mmbichi nione .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…