Tuliowahi kuumwa sikio/masikio tukutane hapa

Tuliowahi kuumwa sikio/masikio tukutane hapa

1.Niliwai kuingiliwa na siafu mmoja sikioni,aisee nilipata shida maana kila akitembea nahisi kama limnyama gani sijui mbaya zaidi ile miguu yake akitembea ni kama inavuta ngoma ya sikio hivi,bahati nzuri nayeye hakukaa sana naona alikua anatafuta njia atoke alipotokeza kichwa tu nilimdaka kwa hasira kumvuta nje.Nashukuru hakuuma ngoma ya sikio.

2.Sikio kupiga kelele ,yaani nikikaa sehemu tulivu nahisi kama kuna mashine inaunguruma kichwani hivi,hii imenisumbua sana nilishaweka bangi haikusaidia,nilikuja kupona baada ya kutumia dawa Fulani za asili za kutoa sumu mwilini,lakini inakera sana maana ili ukae kwa amani inabidi uwashe angalau redio tofauti na hapo ni kero hasa wakati wa kulala.
Mkuu naomba unijulishe na Mimi hiyo dawa hapa napata mziki wa hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeumwa sikio, meno, macho, ila komesha n kipanda uso (kivanga lyuva) kwa kilugha chetu, acha kabisa hii n hatari yaan unahis haswaah jicho linajiacha, pua inang'oka.
 
Habarini wana jf nimatumaini yangu mu wazima nimeona niingilie huu uzi maana namm nina tatizo la infection kwenye sikio.

Lilianza nikiwa dar nikaenda pale ekenywa akanicheki dr akaniambia inabidi ni hudhurie clinic pale kwa week sita ikianza siku niliyo enda sasa shida ikaja mm nashughuli zangu mkoani na ndizo zinanipa kidogo ulaji kumwambia dr akaniambia inabidi niendelee na clinic kwa mkoa nilipo alinambia inabidi nihudhurie bugando mwanza..sasa dhumuni lakuandika hapa nikwamba nimeshatibiwa na ma ENT wawili tofauti lakini bado sikio langu haliponi na nimetumia dawa tofauti 3 pamoja na kufnya culture lkini hali bado .. Dr alinambia ninashida inaitwa "otiti externa" kitaalam .

Ndugu zangu kwa ambao wamewahi kusumbuliwa na sikio naombeni mniambie nifanye nini maana linawasha na maumivu hadi kichwani na nyuma ya sikio asanteni..
 
Back
Top Bottom