1.Niliwai kuingiliwa na siafu mmoja sikioni,aisee nilipata shida maana kila akitembea nahisi kama limnyama gani sijui mbaya zaidi ile miguu yake akitembea ni kama inavuta ngoma ya sikio hivi,bahati nzuri nayeye hakukaa sana naona alikua anatafuta njia atoke alipotokeza kichwa tu nilimdaka kwa hasira kumvuta nje.Nashukuru hakuuma ngoma ya sikio.
2.Sikio kupiga kelele ,yaani nikikaa sehemu tulivu nahisi kama kuna mashine inaunguruma kichwani hivi,hii imenisumbua sana nilishaweka bangi haikusaidia,nilikuja kupona baada ya kutumia dawa Fulani za asili za kutoa sumu mwilini,lakini inakera sana maana ili ukae kwa amani inabidi uwashe angalau redio tofauti na hapo ni kero hasa wakati wa kulala.