Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

bange sio chai🀣🀣🀣🀣
 
actually walikua sio majambaz Bali ni vibaka.Nakumbuka 2013 Arusha mitaa ya unga limited mida km saa sita usiku nimetoka zangu kuangalia mechi za Uefa champions ligi, natembea zangu barabani then nikafika mahali nikachepuka nikaingia kauchochoro flani ili niingie home. Sijatembea kitambo sana mara ghafa nimekabwa shingo. Wengine wamekaba shingo nyuma wengine kama wawili wamekuja kwa mbele wameshika visu virefu wamevilengeshea tumbon kwangu then wakasema ,"we charii toa kila kitu ulichonacho vinginevyo tunakutoboa toboa hili tumbo"......... Aisee watoto wakiarusha huwa hawaongei mara mbili. Nikawaambia chukueni chochote mtakachokikuta mfukon.... Wakachukua elfu kumi iliyokuwepo pamoja na simu.

Vile visu vilikua virefu sana kiasi kwamba wakitoboa tumbo lazima vitokee mgongoni
 
Simuonei mwizi huruma[emoji23][emoji23]
 
Walikuona jini au?
 
Kwa hiyo wezi wakaibiwa Fatuma lao
 
Wahuni wakikuwahi inabidi uwe mpole tu [emoji28]
 
Pole sana .Mimi mitaa hiyo ya ungalimited miaka ya 2010 siku ya jumapili nikaamua kwenda kusali kanisa Moja huko unga limited .Wakati huo naishi sinoni karibu na faya na ni mgeni Arusha Nina miezi kadhaa Wala sijui mitaa ya unga limited ni nuksi.Sasa nikaondoka na jirani yangu mida kama saa tatu hivi tuende taratinu kwa miguu ,kipindi hicho simu aina ya blackberry ilikiwa hot sana nikaibeba jirani akaniambia iache nikamsikiliza, nikachukia kisimu changu Cha tochi nikahamishia line yangu tukaenda tukafila kanisani salama.Muda wa kurudi kumbuka mm nilikuwa bachelor nikanunua nyama robo nikabakiwa na chenji kama 3000 tukawa tunarudi na kihand bag changu nimetia kile kisimu Cha tochi na vile vichange.Sasa tunaongoza njia tukafika kwenye kidaraja kama Cha machuma hivi unga limited na Kuna migomba mingi mingi pembezoni tukaona vijana wakubwa tu wanaogelea mtoni yaani wako watupu kama nyani ikabidi tushangae .Mida hiyo ni kama saa saba mchana na jua linawaka .Ghafla tukamwona kijana mmoja yupo smart kiaina anakija mbele yetu huku anatabasamu,basi mm Nikajua anamjua yule nilikuwa naye kumbe na yeye anajuwa yule kijana ananijuwa mm tukawa tunazidi kukaribiana nae .Alitufikia akasalimia vizuri tu tukaitikia akaniambia sisteri naomba handbag Yako nikamjibu kimzaha kaka kirahisi hivyo?Akasema unataka mpaka udhurike ndo utoe ?Nikabaki nashangaa.Yule mwenzangu kumbe ashastukia tumevamiwa akaniambia mpe haraka huku amepaniki hatari basi Nikabaki sielewi nn kinaendelea.Ghafla yule kijana akatoa sime,sijui panga refu hatari kwenye mfuko wa suruali Sasa hapo ndo sijui suruali ilikiwa imechanwa mifukoni au lilikaaje mfukoni ,Sasa na lile jua la mchana lile panga lilikuwa linametameta kwa namna lilivyonolewa.Hapo akili fasta ikanijia nikamwambia kaka ulisema unataka handbag hii hapa nikampa mwenyewe fasta,akapokea Wala hakukimbia akufungua akaniuliza sista na kupendeza kote ndo una simu kama hii? Nikamjibu maisha kaka basi akachukua simu akanirudishia line akachukua zile hela akanirudishia funguo zangu huyo akashukia kule mtoni taratibu.Tuliondoka kimya kimya mpaka tunafika hakuna anayeuliza mwingine nn kimetokea.Yaan ungalimited sitak hata kupasikia.
 
dah huu uzi umenikumbusha tukio gumu saana maishani mwangu , ni 2016, tarehe saba 7/8/2016, nimetoka zangu bank ilikuwa nmb mwanjelwa nimechukua zangu kama milion moja narudi zangu njombe, by that time nina smartphone nokia , nimependa zangu daladala nitoke nje ya hapo nitafte mahali pa kulala., likaja wazo nikalale sai nikashuka ilipo mfikemo hotel kwa sasa , ili nivuke barabara wakaja jamaa wawili wakaniambia kwa upole usivuke tupe hizo pesa, ukipiga kelele tunakua , dah wakaniambia twende huku ukibisha tunakuua wanaonyesha pisto wakanitaka nifuate uchochoro aisee sikumbuki walinipiga na nini nilopoteza fahamu hadi 8, nipo rufaaa wananiambia umepigwa na nondo na umeletwa na wasamaria wema , mzee sina hata mia wala simu ,namshukuru sana dada moja nurse alinisaidia sana na she my sister hadi leo, ila wale jamaa nimewasahe kwa sababu siwafahamu so hata nikiwachukia hainisaidii kitu,wale watu wema walionipeleka hosptal MUNGU wangu awaongezee uhai mrefu huko waliko ,lile tukio limeniacha na tatizo hadi leo pua zangu hazinusi kabisa labda harufu ya bangi ndio naipatta nikipita kw wala ganja huwa najua nje ya hapo dah sinusi, niliambiwa kuna matibabu ya tatizo la pua nafuatilia nijaribu kutibiwa ,
 
Dah,siku yangu imekuwa fupi ghafla 🀣🀣🀣
 
Waende huko Mara walete upuuzi watachezea wajute
 
Eeeeh pole aiseh
 
Maskini pole Sana Sai ndo mitaa ya home hiyo so walikukuta Sae?

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Yan vibaka ni watu wa ajabu saana. Anakutana na mdada anahangaika kutumia nguvu kubwa kumuibia, ya nini yote, toa amri tu leta simu,leta pochi imeisha hiyo. Mimi kipind cha nyuma kuna siku nimetoka kazin mida tu ya SAA moja na nusu usiku

Yan akichokifanya yule mwehu alinipiga roba Na bonge mtama looh Mimi chini nikavunja miwan yangu ya macho ya gharama, kilichofata pale kwa uoga nikatoa tu kila kitu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…