Tuliowahi kuvamiwa, kuibiwa au kutekwa na majambazi tujikumbushe

Way back miaka ya 2006 tulikua nyumba ya kupanga miaka hio kulkua na wale vibaka wahuni sura ngumu alafu wababe wanaiba hadi mchana kulikua na chuma kimoja kinaitwa Godzilla uyo alikua akipita mchana mjue usiku hakulaliki...
Akipita watoto wote ndani (ila vibaka wa zaman walikua wana sura ngumu aiseee)
Sasa siku moja tumelala usiku nyumba nzima imebaki na wamaza na sisi madogo (hakukua na mama mwenye kijana mkubwa) tunasikia mlango wa ukumbini unagongwa kinoma..
Wapangaji wote wakafolenishwa ukumbini wahuni wanapiga mibanzi wamaza kama sokweee
Wanawaambia leteni helaaa mamaza hatuna hela jaman
Sisi watoto wa kujikojolea washajikojolea mimi nmejificha chin ya mtungi wa ukumbini..
Baada ya kukosa hela wakauliza mmepika nini
Wapangaji walopika ugali wakala mibanzi tena kama ya sokwe
Mama dula alikua kapika wali mate mbele ndo akaokoa jahazi wahun wakala wali na ukoko wote tupo tunawaangalia wakamaliza wakachukua kopo la mafuta (mamujee) wakaingiza madole yao wakakomba mafuta wakasepa
 
Wahuni siyo watu
 
Mkuu walijipaka mwilini hayo mafuta
 
😂😂😂Nimecheka balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…