Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahahaaaaugumu wa maisha unafany watu wawe vichaa
Wahuni siyo watuNakumbuka ilikuwa 2013, bana wee sitaka nisahau maishani mwangu.
Nakumbuka nilipiga kazi kwenye biashara yangu, nikajikusanyia pesa nzuri tu sio chini ya million 2, ghetto nilipapendezesha vizuri sana.
Chumba changu kilikuwa pembezoni na mto Arusha eneo nililopewa na wazazi wangu pamezungukwa na miti na migomba mingi sana, kuna msitu mmoja mzuri sana kama ulaya vile.
Sasa kipindi hicho nilikuwa nimenunua bonge la speaker, daily nilikuwa nakula reggae na nyimbo za hiphop za chuga, nilikuwa na computer ya dell desktop, kipindi hicho ukiwa na computer mtaa mzima unakuheshimu.
Ilikuwa majira ya saa 9 usiku, nikiwa nimelala gheto, ghafla nikasikia mlango umepigwa jiwe fatuma kwa watu wanaojua jiwe fatuma ni nini watakuambia, walikuwa kama 7 hivi wameshika marungu na mapanga wengine wananimulika na torch machoni yani kama movie vile..
Jamaa wakaniambia toa ulichonacho, nikawaambia sina chochote zaidi ya hivi vitu vya gheto, hakuna!! toa pesa ulizonazo mara mabapa ya mgongo kwa sana, nikawaambia sina pesa, kuna jamaa akawaambia huyu mpaka akatwe ndo atoe pesa, daah jamaa akanikata na panga mgongoni, nikaona niwape hela zao waondoke.
Jamaa wakanipa kichapo cha maana, wakabeba computer, nguo, viatu vyote, speaker na pesa zote nilizosave wakaondoka zao.
Nilichojifunza, simuonei mwizi huruma nikishajua ameiba kweli, yani atakula vitofali mpaka ajute kwanini kaiba..
Hayo ni yangu yalionikuta enzi hizo je nyie kiliwakuta kipi, nakaribisha mchango wenu kwenye huu uzi.
ONE TIME,
ONE FOR THE ROAD..
APPROXIMATELY ONCE AGAIN..
,
hahaaaaMbona hujatolewa kwenye taarifa ya habari?
Fatuma zipo mpaka sasa mzee2013 mbona juzi tu we kweli dogo, acha kudanganya watu mwaka huo hakukuwa na mambo ya fatuma. Tafuta uwongo mwingine.
27 walidedi mmoja akawa bubu. Bastola ilikuwa na risasi 74 kama ya RamboWengi walidedi kuna mmoja tu ndo iliishia skioni akawa bubu
😂😂Yan mi skutaka kuwauliza wamelibebaje...ni za kichwa tu
😂😂😂Kumbe ulifariki kakaIlikuwa mwaka juzi tu hapo walikuwa watano hivi nikatembeza kichapo hadi tukafariki wote!,siku hizi nikikutana nao heshima!
walikuwa chai
Chai yenyew haina hata tangawiz,😂walikuwa chai
Umesahau sukariChai yenyew haina hata tangawiz,😂
Kwa taarifa yako Acha upumbavu kila kitu kiko connected na brain kama hujui.Mishipa ya fahamu ,kivipi ili mtu asikie ianzie kwa ubongo ,Kwan anaesikia kwanz ni sikio ?
YeehKwa taarifa yako Acha upumbavu kila kitu kiko connected na brain kama hujui.
Mkuu umesoma anatomy 👍Hio sehem inaitwa broca's area ndo inahusika na kuzungumza (regardless unasikia ama hausikiii)
Hyo 27 umeitoa wap?27 walidedi mmoja akawa bubu. Bastola ilikuwa na risasi 74 kama ya Rambo
Enheee, namm ndo nilimgonga hapohapo
Mkuu walijipaka mwilini hayo mafutaWay back miaka ya 2006 tulikua nyumba ya kupanga miaka hio kulkua na wale vibaka wahuni sura ngumu alafu wababe wanaiba hadi mchana kulikua na chuma kimoja kinaitwa Godzilla uyo alikua akipita mchana mjue usiku hakulaliki...
Akipita watoto wote ndani (ila vibaka wa zaman walikua wana sura ngumu aiseee)
Sasa siku moja tumelala usiku nyumba nzima imebaki na wamaza na sisi madogo (hakukua na mama mwenye kijana mkubwa) tunasikia mlango wa ukumbini unagongwa kinoma..
Wapangaji wote wakafolenishwa ukumbini wahuni wanapiga mibanzi wamaza kama sokweee
Wanawaambia leteni helaaa mamaza hatuna hela jaman
Sisi watoto wa kujikojolea washajikojolea mimi nmejificha chin ya mtungi wa ukumbini..
Baada ya kukosa hela wakauliza mmepika nini
Wapangaji walopika ugali wakala mibanzi tena kama ya sokwe
Mama dula alikua kapika wali mate mbele ndo akaokoa jahazi wahun wakala wali na ukoko wote tupo tunawaangalia wakamaliza wakachukua kopo la mafuta (mamujee) wakaingiza madole yao wakakomba mafuta wakasepa
😂😂Aliepigana na wezi Hadi wakafariki wote ndo sijaelewa aje atupe ushuhuda mbinguni kupoje😂😂😂Umesahau sukari
😂😂😂Nimecheka balaaWay back miaka ya 2006 tulikua nyumba ya kupanga miaka hio kulkua na wale vibaka wahuni sura ngumu alafu wababe wanaiba hadi mchana kulikua na chuma kimoja kinaitwa Godzilla uyo alikua akipita mchana mjue usiku hakulaliki...