Tuliowahi kuwasumbua mademu PM tukutane hapa

Rafikiii mimi nakuja pm hayo yote sinaaa..
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Toka niingie jf nmechat pm na wadada wawili tu! Tena hao mmoja alinifata mwenyewe na mwengine nilimchungulia kwenye daladala akikoment hapa jf nikaona id yake nikampm kumsalimia..!
Waliobaki wote ni wanaume na hawazidi hata kumi, na hao wote ni issue za biashara..! Huwa sipendi kumsumbua mtu maana mi mwenyewe sipendi kusumbuliwa..!
 
Safi sana mkuu agiza kinywaji bill ikuje kwangu usumbufu usumbufu sio mzuri
 
Haha ngoja nikuvizie
Ahahha kuna shemeji yangu mmoja yupo humu tunaitana shemeji wenyewe tupo kama ndugu sasa hivi

Tulikua tunachat pm shemeji yangu ni mstaarabu tumezoeana pm hakuna kunisumbua kuomba pic wala nini siku ya siku anataka tuonane hapo sijui anafananaje wala hajui shunie anafananaje

Nikaenda eneo la tukio nipo na rafiki yangu mmoja nikamuwahi nimekaa naangalia mlango akaniambia nipo na rafiki yangu basi kila wakiingia watu wawili naangalia mara wameingia vizee viwili nikaifunika simu yangu nikasema kama ndio yeye atapiga akome [emoji3] sipokei

Bada ya mda wakaingia wakaka wa makamo moja kwa moja alikuja kwenye meza yetu shunie shemeji yangu mm wala sikutag unajijua popote ulipo mtu ambaye sijutii kukufahamu jf Mungu azidi kukuweka tu na mautundu yako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sema mi toka nione anko wangu ana JF app kwenye simu yake nimekua makini kweli na watu wa humu. Maana ni fisi hatari na yeye
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] usiniambie kwahiyo ankole na yeye yupo humu I'd anayotumia vipi hujaimanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…