Tulitaka kutengenezewa ukame bwawa la Mtera, tupazeni sauti tukiona ndivyo sivyo

Mungu anawaona na tamaa za dunia,wengine ni wazee kabisa
 
Sasa watanzania wenzangu mnapaswa kukiri kuwa ni jambo la afya kuwa na wapinzi bungeni japo 40%.

Hata kama mnataka CCM itawale milele, chagueni wabunge wengi wa upinzani.

Hili suala la umeme na figisu zinazo endelea utaona wabunge wetu wa CCM wana nyamazia tu.

Na nyie wabunge wa CCM endeleeni kuwa puuza raia, ipo siku hamjui mtaharibu vipi, raia wanaweza kukosa uvumilivu msijisahau mkiwa katika huo umoja wenu.

Watanzania wengi bado wanaipenda amani. Siku wakitafsiri kuwa kukosa umeme labda na maji kunachangiwa na maamuzi bungeni hamtajua moto ulianzia wapi.
 
Swali dogo kwa wataalamu haiwezekani katika mfumo wa mabwawa kuweka pump kadhaa kubwa kurejesha Sehemu ya Maji katika bwawa la Akiba baada matumizi ikihitajika?
Sina uhakika sana na wala siyo Mhandisi, baadhi ya nchi wanafanya hivyo
 
Iko hivi, baadhi ya watu maana ya kazi iendelee ni kuendeleza yale mambo mabaya ya kuumiza wananchi. Walianza na tozo, wamachinga, baadaye wakataka kuanza na maji na umeme, wakamdanganya rais kumuambia eti kuna ukame etc na yeye rais akaingia mzima mzima kukubali propanganda zao, hatimaye wananchi wakapiga kelele. Lengo kubwa hasa ni kuhakikisha rais Samia anakosa muelekeo ili ikifika 2025 wananchi wawe na malalamiko mengi kiasi kwamba wao kwa wao waseme eti ulishindwa kuendesha nchi wananchi hawakutaki tupishe. Sijui kwa nini asingetembelea nyota ya Dkt Magufuli????
 
Aibu kwa Taifa ,tutaendelea kuwa tegemezi mpaka kufa kwetu kama akili ndio hii
 
Wawe wapinzani wawe nani tunataka watu wenye uchungu na nchi yao basi! Kipindi cha JK ili bwawa la Mtera lilifungwa kabisa, halikuwa linazalisha ata Megawati 1 ya umeme katika Megawati 80 na wapinzani wlaikuwepo bungeni na si mnadai ndiyo kulikuwa na uhuru wa kutoa maoni? Kuna upinzani ulimsikia akilisemea ilo? Baada ya kuja JPM ndo tukajua kuwa kumbe kuna issue hii inaendelea!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda fedha za kampeni 2025 safari hii zimeanza kukusanywa mapema.
 
Na huko tuzomeeni tu,wamalize kwanza JNHP
 
mafisadi kwa kipindi hiki wanapaswa kutumia akili kubwa la sivyo watakua wakiumbuka kabla hawajafikia lengo.
 
asingekua waziri wa mchongo angeshaondolewa, yote yanayoendelea pale wizarani yana baraka za wakubwa.
Pamoja na mchongo huyu mama japo ana madaraka makubwa ila zile weaknesses za kike zinadhihirika kwake kwamba hii jinsia bila kushauriwa na mwanaume haiwezi kufanya jambo lolote kubwa ikiwa peke yake.

Sometimes akili yake inamwambia kabisa kwamba mgosi hafai ila hana uhakika kama anachowaza ni sahihi mpaka aombe ushauri kutoka kwa wanaume kwanza(japo kikawaida sana inadhihirika ni sahihi mgosi anacheza deal zake pale wizarani) so inabidi aitishe ushauri kutoka kwa wanaume ambao baadhi ni chawa wa Makamba nao wanamjaza kwamba Makamba anafanya vizuri.

Tungekuwa na kiongozi makini mwanaume saizi tungekuwa tunazungumza mengine hapa.
 
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
Mita 5.76 ni bwawa gani hilo mkuu, nakumbuka 2015 nilipita Mtera Dam maji hamna ila tope na viboko wakihangaika kutafuta hifadhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…