Tulitaka kutengenezewa ukame bwawa la Mtera, tupazeni sauti tukiona ndivyo sivyo

“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
Apewe ulinzi. Kajanuari ni kamtu kabaya kana roho mbaya na chuki
 
Hivi maswi yuko wapi maana nae alipata misukosuko baada ya kupambana na wanufaika wa mgao wa umeme
 
“Kwa kina hiki cha mita 5.76 tunaweza kuzalishha umeme kwa kiwango cha juu cha megawatts 80 kwa miezi saba ijayo hata kama tone moja la mvua halitaingia kwenye bwawa la Mtera”

- Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme Mtera, Elias Mwalupilo
Kwa hili kwa kweli hapa wa kupongezwa ni Magufuli maana aliweka wazi mapema hii mbinu ya hawa majambazi.
 
Hao ndio wazalendo sasa sio yale Majizi yanayotetewa humu na kina Pasko
 
Zitto siyo mpinzani?

Uroho wa pesa kwa gharama ya maskini hauna cha upinzani au chama tawala. Kwani Magufuli alivyoingia madarakani na kuanzia kufanyia kazi yote wapinzani mliyokuwa mnapigia kelele mlimfanya nini? Si ni hao hao akina Lissu badala ya kumwona kama ally wao wakaanza kumwita eti ni dikteta uchwara? Mlimpa stress kiongozi wetu mwenye uzalendo wa ajabu sana hadi mkapelekea kifo chake halafu leo mnaanza tantalila zenu za upinzani.

Nope! Wapinzani mlituangusha na bado mnaendelea kutuangusha. Tumaini letu pekee linabaki kwa watanzania ambao Mungu ataamsha mioyo yao na kuukataa upuuzi wa aina yoyote ile na kufanya kile kilicho sahihi kwa ajili ya maslahi mapana ya Tanzania. Watanzania wa aina hii wapo kote kote kama meneja huyu wa Tanesco Mtera alivyofanya. Magufuli ameacha spirit kubwa nyuma na hii ndiyo legacy yake kuu na ya msingi.
 
Tatizo sio Makamba.
Tatizo ni CCM.
Wacha majibu ya kukariri.

CCM haiongozi wizara ya nishati, Makamba ndie anayeongoza hiyo wizara na huu mzigo lazima umuangukie yeye.

Usicheleweshe tatizo kwa kulitafutia majibu ya jumla yasiyo na maana, kwa hiyo unataka tuendelee kupigwa mpaka CCM itakapoondolewa madarakani?

Think.
 
Well done
 
Kama ni hivyo maji yapatikane juu chini yakosekane?
Kutoka Mtera hadi Kidatu pana umbali wa kutosha sana na maji yanayotoka Mtera mengi yanapotea njiani along the river kutokana na ukame mkali na jua hasa kati ya Mtera na Ruaha Mbuyuni. Lakini pia MTERA kuna reseivor kubwa (bwawa) tofauti na Kidatu. Kwa lugha rahisi MTERA inatumia maji yaliyohifadhiwa katika bwawa kuzalisha umeme. Yanayotoka baada kuzalishwa kwa umeme njiani kuna matumizi mengine ya kibinadamu ikiwemo matumizi ya nyumbani, mifugo na hata kilimo. Pia maji mengi yanapotea kupitia evaporation kutoka na jua kali.
 
Nafikiri taarifa ya awali ya TANESCO ilitaja kwamba kituo cha uzalishaji kilichoadhirika zaidi ni Kihansi. Mtera haikuguswa
 
Rais naye ni wale wale tu. Ina maana hana njia zingine za kupata ukweli kama mtangulizi wake alivyokuwa anapima mapapai, mbuzi COVID-19? Yeye akiletewa anapokea na kuhutubia tu.
Nilitaka kushangaa ukame gani wa ghafla huo,
Raisi laziam aingilie kati, vinginevyo atakua analea wahalifu.
 
Hiyo ni team Kikwete iliyoingia madarakani. Angalia jinsi biashara za lake oil zilivyoshamiri kwa miezi michache iliyopita. Nasikia mtoto wake wa mwisho kazaa na Mkwere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…